Tafuta

Ziara ya Papa Asti:sintofahamu ni ugonjwa mbaya sana!

Ni hatari hata kwa imani yetu,ambayo inanyauka na kubaki na nadharia,lakini sio kwa matendo ya dhati, kwa sababu hakuna kuhusika ,hakuna kupiga hatua mbele kwanza,hakuna kuthubutu.Kwa maana hiyo imani inageuka kuwa ya wakristo wa maji juu ya waridi,ambao wanasema kuamini Mungu na kupenda amani,lakini hawasali wala kutunza jirani.Ni katika mahubiri ya Papa Dominika Novemba 20 katika ziara ya Kichungaji Asti.

Na Angella Rwezaula, - Vatican,

Katika Dominika ya 34 na ambayo inafunga mwaka wa kanisa na Siku Kuu ya Kristo Mfalme wa Ulimwengu, tarehe 20 Novemba 2022, Baba Mtakatifu amekuwa katika ziara ya kichungaji katika Jimbo katoliki la Asti, kaskazini mwa Italia ikiwa ni eneo la kukumbuka  mahali wazazi wake hasa baba yake alipozaliwa na baadaye akahamia nchini Argentina. Jumamosi 19 Novemba 2022, alimtembelea binadamu yake Carla Rabezzana anayeishi mjini Portacomaro, ili kumpongeza na kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 90 ya kuzaliwa. Lakini pia hata kuwaona ndugu zake wengine wengi ambao alikutana nao kwa karibu. Kwa njia hiyo katika kuadhimisha Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Asti Papa ametoa mahubiri yake. Kabla kuanza mahubiri lakini ameleza walivyoona kijana Stefano anaomba kupewa huduma ya kuhudumia altareni katika mchakato wake kuelekea ukuhani. Papa ameomba wasali kwa ajili yake ili aendelee mbele katika wito wake na kuwa mwaminifu. Lakini pia hata kusali kwa ajili ya Kanisa hilo la Asti ili Bwana atume miito ya kikuhani, kwa sababu kama walivyoona, walio wengi ni wazee kama Papa na inahitajika mapadre vijana kama baadhi ya wengine wanaofanya vizuri. Kwa hiyo ni kusali kwa Bwana ili aweze kubariki ardhi hiyo. Baada ya kusema hayo Papa ameendelea  na mahubiri.

Kwa kuanza amesema katika ardhi hizi Baba yangu aliondoka kuhamia nchini Argentina, na katika ardhi hizo aliweze kuzalisha mfumo mzuri hasa, kujishughulisha na watu, na hivyo nimekuja kutembelea ladha ya mizizi. Lakini hata  kwa mara nyingine tena Injili inatupeleka kwenye mizizi ya imani. Yenyewe inajikita kwenye ardhi kavu ya Kalvario, mahali ambapo mbegu ya Yesu kwa kufa, ailichanua tumaini, kwa kupandwa katika moyo wa ardhi, alitufungulia njia ya Mbingu, kwa kifo chake alitupatia maisha ya milele, kwa njia ya mti wa msalaba, alituletea matunda ya wokovu. Tutazame kwa maana hiyo Yeye aliyesulibiwa. Sentensi moja tu inaonekana msalabani: "Huyu ndiye Mfalme wa Wayahudi" (Lk 23:38). Hiki hapa ndicho cheo: Mfalme. Hata hivyo, tukimtazama Yesu, wazo letu la mfalme linabatilishwa. Wacha tujaribu kuibua kufikiria mfalme: tutafikiria juu ya mtu mwenye nguvu aliyeketi kwenye kiti cha enzi na alama ya thamani, fimbo mikononi mwake na pete zinazometa kati ya vidole vyake, wakati anatamka maneno mazito kwa raia wake. Hii, kwa ufupi, ndiyo taswira tuliyo nayo akilini. Lakini tukimtazama Yesu, tunaona kwamba ni kinyume kabisa.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Yesu hakuketi kwenye kiti cha enzi cha starehe, bali ananing'inia kwenye mti; Mungu ambaye “anawaangusha wenye nguvu katika viti vyao vya enzi” (Lk 1:52) anafanya kazi kama mtumishi aliyesulubiwa na wenye nguvu; kupambwa tu kwa misumari na miiba, kuvuliwa kila kitu lakini tajiri katika upendo, kutoka kwa kiti cha enzi cha msalaba hafundishi tena umati kwa neno lake, hauinui mkono wake tena kufundisha. Anafanya zaidi: hanyoshei mtu yeyote kidole, lakini anafungua mikono yake kwa kila mtu. Hivi ndivyo Mfalme wetu anavyojidhihirisha: kwa mikono wazi, a brasa aduerteNi kwa kuingia ndani ya kumbatio lake tu ndipo tunapoelewa: tunaelewa kwamba Mungu alikwenda mpaka pale, kwa kitendawili cha msalaba, kwa usahihi kukumbatia kila kitu kuhusu sisi, hata kile kilichokuwa mbali sana naye: kifo chetu, maumivu yetu, umaskini wetu na udhaifu wetu. Alifanyika mtumishi ili kila mmoja wetu ajisikie kama mwana; alijiruhusu kutukanwa na kudhihakiwa, ili katika kila unyonge pasiwepo hata mmoja wetu awe peke yake tena; alijiruhusu kuvuliwa, ili mtu yeyote asijisikie kuvuliwa utu wao; alipanda juu ya msalaba, ili kwamba katika kila msalaba na kila  historia kuna uwepo wa Mungu.

Tazama Mfalme wetu, Mfalme wa ulimwengu kwa sababu alivuka mipaka ya mbali ya ubinadamu na kuingia kwenye matundu meusi ya chuki, na kwa kujiacha ili aangaze maisha na kukumbatia kila uhalisia.  Baba Mtakatifu Francisko ameomba kusheherekea huyo mfalme. Na swali la kujiuliza kuhusu  Mfalme wa Ulimwengu je ni Bwana wa Maisha yangu? Jinsi gani ninaweza kumwadhimisha Bwana kwa kila jambo ikiwa hawi hata Bwana wa Maisha yangu? Kwa maana hiyo Papa ameomba  tukazie tena macho yetu  kwa Yesu msulibiwa. Tazama Yeye hatazami maisha yake kwa muda kidogo tu na kisha basi,  yeye hajikiti kuwa na mtazamo wa kukimbia kama mara nyingi tunavyo fanya sisi kwake, lakini yeye yupo pale akiwa na mikono yake iliyo wazi … a brasa aduerte,  kwa kukueleza kwa ukimya kwamba hakuna yeyote kwake ni mgeni, si kwamba hataki kumkumbatia, kukuinua na kukookoa jinsi ulivyo, kwa historia yako, makosa yako na dhambi zako. Anakupatia uwezekano wa kutawala maisha, ikiwa unakata tamaa kwa upendo mnyenyekevu ambao anapendekeza, lakini ambao halazimishi, kwa upendo wake ambao daima anakusamehe,  daima anakuinua na daima anakurudishia hadhi.

Ndio wokovu unakuja kutuacha tupendwe na Yeye, kwa sababu ndio hivyo tu, tunaweza kukombolewa dhidi ya  utumwa wa umimi wetu, woga wetu wa kuwa peke yetu, wa kujifikira kushindwa. Baba Mtakatifu Francisko ameomba kujiweka mara nyingi mbele ya Msalaba, kujiachia kupendwa  kwa sababu mikono yake iliyo wazi iweze hata kutukumbatia sisi huko mbinguni, kama vile mnyang’anyi. Tuhisi kuambiwa ile sentensi pekee ambayo Yesu alisema akiwa  juu ya Msalaba kwamba “Leo hii utakuwa nami mbinguni”(Lk 23,43). Hiyo ndiyo Mungu anataka kuwaambia, kila mara tunaojiachia tutazamwe na Yeye. Na kwa njia hiyo tunatambua kwamba hakuna  chuki isiyo tambulika, iliyo juu mbinguni, yenye nguvu, bali Mungu yuko karibu, mwororo na mwenye rehema ambaye mikono yake imefunguliwa ikifariji na kubembeleza. Huyo ndiye Kiristo mfalme. Baada ya kutazama, je tunaweza kufanya nini? Baba Mtakatifu ametoa swali na kujibu kwamba Injili inapendekeza mbele yetu njia mbili. Mbele ya Yesu kuna anayefanya kutazama na ambaye anahusika. Watazamaji ni wengi, kiukweli andiko linabainisha kwamba watu walikuwa wanatazama. Hawakuwa watu wakatili, walikuwa waamini, lakini kwa kuona msulibiwa walibaki watazamaji: hawakufanya kwenda hatua mbele kuelekea  kwa Yesu aliko,  walitazama kutokea mbali, wakidadisi  na kutokujali, bila kuhusika kiukweli, bila kujiuliza wanaweza kufanya nini.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Na watakuwa walitoa maoni, walitoa hukumu zao, na mapendekezao yao, na mwingine labda kwa kulalamika, lakini wote walibaki kutazama kwa mikono yao na mikumbatio ikefungwa, Na hata karibu na msalaba kuwa watazamaji; wakuu wa watu ambao wanataka kuona tamasha katili la mwisho usio na utukufu wa Yesu; askari ambaye wanataka aweze kummaliza; mmoja wa majambazi ambaye anabebesha hasira yake Yesu. Wamcheka na kumdhihaki na kutoa nyongo zao. Watazamaji wote hao wanashikirishana wimbo kwa maana andiko linarudia mara tatu “ ikiwa wewe ni  mfalme, jiokoe (Lk 35.37.39). Jiokoe mwenyewe kiukweli ni kinyume na kile ambacho Yesu anatenda, kwa sababu hajifikiri mwenyewe bali kuokoa wao. Hata hivyo baba Mtakatifu amebainisha kwamba lakini kujikoa mwenyewe, inaambukiza: wakuu wa maaskari kwa watu, wimbi la ubaya linafikia karibu wote.  Lakini tufikirie jinsi ambavyo ubaya unaambukiza na kufanana n aule ugonjwa tunaposhikwa na kuambukiwa kwa haraka. Na kwa sababu watu wale wanazungumza ya Yesu lakini hayaendeni hata wakati wa Yesu. Wanakuwa mbali na wanazungumza.

Papa Francisko amesema huo ni ugonjwa mbaya sana wa sintofahamu. Kwa kusema  hainihusu. Sintofahamu kuelekea Yesu na hata kuelekea kwa wagonjwa, kwa maskini, na mafukala wa nchi. Papa amependa kuwauliza watu, hasa wao kwa kuwa anajua kwamba wanatoa sadaka kwa masikini, lakini je wanapokuwa wanaitoa sadaka hiyo wanamtazama mtu huyo machoni? Je, wana uwezo wa kuangalia machoni pa huyo mwanamume au mwanamke maskini anaye waomba sadaka? Je, wanapotoa sadaka kwa maskini, wanawapatia  sarafu au wanawagusa mkono wao? Je, wana uwezo wa kugusa mkono wa wanadamu hao? Papa aliomba wasitoe jibu, lakini kila mmoja afanye tafakari, kwa sababu kuna sintofahamu nyingi. Watu wengi huzungumza juu ya Yesu lakini matendo yao hayaendani na Yesu. Na huo uambukizo hatari wa kutojali ambao hutengeneza umbali na huzuni. Ni ambukizo la kifo cha sintofahamu. Wimbi la ubaya linaenea daima hivyo, kwa kuanza kuelekea na umbali kutazama bila kufanya lolote, bila kutunza, kinyume chake ni kujifikiria binafsi, kujitunza na tabia ya kugeuza kisogo. Ni hatari hata kwa imani yetu, ambayo inanyauka na kubaki na nadharia, lakini sio  kwa matendo, kwa sababu hakuna kuhusika ,  hakuna kupiga hatua mbele kwanza, na hakuna kuthubutu. Kwa maana hiyo inageuza kuwa wakristo kama maji juu ya waridi, ambao wanasema kuamini Mungu na kupenda amani, lakini hawasali na wala kutunza jirani.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Lakini pia kuna wimbi zuri la wema. Kati ya watazamaji wengi, mmoja anahusika kama vile jambazi. Watazamaji wanamcheka Bwana, Yeye anazungumza na kumwita kwa jina Yesu. Wengi wanamtupia hasira zao, yeye anakiri makosa yake kwa Kristo, wengi wanasema jiokoe mwenyewe, Yeye anasali  kwamba “Yesu nikumbuke mimi”, (42). “Yeye aliomba Bwana hilo tu. Ni sala nzuri hiyo. Ikiwa kila mmoja anaweza kuisali kila siku ni njia nzuri, njia ya utakatifu wa kusema Yesu nikumbuke”, ameshauri Papa Francisko. Kwa njia hiyo mnyang’anyi anageuka kuwa mtakatifu wa kwanza, anakuwa karibu na Yesu kwa haraka na Bwana anamchukua daima kwake. Injili sasa inazungumza  kuwa ni Mnyanga’nyi mwema ambapo kwetu sisi  inatusaidia ili kutukaribisha kushinda ubaya na kuacha kuwa watazamaji tu. Je ni kuanzia wapi? Kuanzia na kuaminiana. Kwa kumwita Mungu kwa jina, kama alivyo fanya jambazi ambaye mwisho wa maisha yake alipata imani jasiri kama ya watoto, ambao wanaamini, wanaomba na kusisitiza. Na kuamini kunasaidia kujua makosa, yeye analia lakini si kwa ajili yake binafasi bali ni mbele ya Bwana. Hata sisi tunayo imani hiyo tuipeleke kwa Yesu kile ambacho kimo ndani au tunafikiria mbele ya Mungu,  labda kidogo kitakatifu na ubani? Anayefanya uzoefu wa kuamini anajifunza kusali, anajifunza kupeleka kwa Mungu kile anachoona, mateso ya ulimwengu, watu ambao anakutana nao; kumweleza kama alivyofanya jambazi  kamba “nikumbe Bwana! Hatuko duniani kwa ajili ya kujikoa wenyewe, bali kwa ajili ya kupeleka kaka na dada kwenye mkumbatio wa mfalme.  Kuomba, kwa Bwana kunasaidia kufungua mlango wa mbingu. Lakini sisi je tunasali sala kwa kumwomba? Papa ameuliza 

Mfalme wetu kutoka msalabani anatutazama kwa mikono iliyo wazi. Ni sisi ambao tunapaswa kuchagua ikiwa tunataka kuwa watazamaji au wahusika. Tunaona leo hii mizozo, kupungua kwa imani, ukosefu wa ushiriki… je tunafanya nini? Sisi Tunaishia kufanya nadharia ya kuhukumu au tunajifunga kibwebwe, tunachukua maisha kwenye mikono yetu, tunaweza kwa kuwa na sababu za ndio ya sala na ya huduma? Wote tunafikiria kujua ambacho hakiendi katika jamii, katika ulimwengu hata katika Kanisa, lakini je tunafanya lolote? Tunachafua mikono yetu kama Mungu aliyeambwa misumari kwenye msalaba au mikono yetu iko kwenye mifuko tunatazama? Leo hii wakati Yesu amevuliwa juu ya msalaba, anatoa kila pazia kwa Mungu na kuharibu sura zetu za uongo kwa ufalme wake na kutazama yeye ili kupata ujasiri wa kujitazama sisi wenyewe kuwa kwenye mchakato wa njia ya kimwamini, ya kumwomba na kuwa watumishi ambao wanatawala naye. Papa amehitimisha kwa kusisitiza kusali mara kadhaa kwa siku kwa kuomba Bwana atukumbuke katika ufalme wake.

mahubiri ya Papa
20 November 2022, 12:58