Ziara ya Papa Asti.Vijana msipoteze wakati katika anasa na mtindo wa mwisho

Mara baada ya misa takatifu iliyoadhimisha katika Kanisa Kuu la Asti Italia,Papa ameshukuru makaribisho,amekumbusha Siku ya Vijana Kijimbo na kuhimiza kuiga mfano wa Mama Maria aliyeamka na kwenda haraka:Ameomba kusali kwa ajili ya Ukraine pia hata kuwaombea waathirika wa moto katika kambi la wakimbizi huko Gaza nchini Palestina.

Na Angella Rwezaula, – Vatican.

Katika hitimisho la Maadhimisho ya Misa katika kanisa Kuu la Asti nchini Italia na kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu awali ya yote amependa kumsifu Askofu kwamba ujasiri wa kusema kwamba Asti ni mwanzo wa Ulimwengu. “Inahitajika ujasiri”... wote wamecheka, lakini akiendelea amependa kushukuru Jimbo, Wilaya na mji mzima wa Asti, kwa makaribisho yenye shangawe ambayo wamemwonesha. Amewashukuru Mamlaka yya rais na kidini kwa maandalizi ambayo yamewezesha kutimiza shauku yake ya ziara. Kwa wote Papa ametaka kusema imekuwa vizuri kukutana nao na anawatakia mema.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Wazo na mkumbatio maalum wa Papa  amependa kuwageukia vijana na kuwashukuru kufika kwao wengi. Mwaka jana katika siku kuu ya Kristo Mfalme ilianzishwa maadhimisho katika Makanisa mahalia Siku ya vijana duniani.  Kauli mbiu inayoongoza hiyo ni sawa sawa na ile ya Siku ya vijana duniani ijayo huko Lisbon chini Ureno 2023, ambapo Papa amepyaisha mwaliko wake wa kushiriki kwamba  "Mariamu aliamka na kwenda kwa haraka" (Lk 1,39).  Mama alifanya hivyo akiwa kijana, na anatueleza kuwa siri ya kubaki kijana iko hapo katika maneno mawili, kuamka na kwenda. Papa amesema anavyopenda kufikiria Mama alivyokwenda kwa haraka na hasa hiyo haraka ambayo mara nyingi anasali kwa Mama Maria kwamba aharakishe kusulihisha tatizo.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Kuamka upesi na kwenda: hakuna kusimama na kujifikiria binafsi, kwa kupoteza maisha katika anasa au katika mtindo wa mwisho, lakini kwa kutazama juu,  na kujikita katika  mchakato wa safari, kwenda nje ya hofu binafsi ili kuweza kutoa msaada kwa wengine wenye kuhitaji. Leo hii wanahitajika vijana kweli, wakakamavu na wenye maamuzisi kujifananisha, kwa sababu sio watumwa wa simu za mkononi, lakini kwa kubadilisha ulimwengu kama Maria, kwa kumpeleka Yesu kwa wengine, kwa kuwatunza wengine, kwa kujenga jumuiya ya kidugu kwa wengine kwa kuibua ndoto za amani.

Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti
Ziara ya kichungaji ya Papa Francisko huko Asti

Baba Mtakatifu Francisko amesema kwamba kipindi chetu tunaishi ukame wa amani. Tufikirie maeneo mengi ya ulimwengu, ni tauni ya vita, kwa namna ya pekee katika nchi inayoteseka Ukraine. Tuwe na la kufanya nakuendelea kusali kwa ajili ya amani! Tusali hata kwa ajili ya familia waathiriwa sana wa moto uliojitokeza siku za hivi karibuni katika kambi ya wakimbizi hukuo Gaza nchini Palestina, mahali ambao wamekufa hata watoto kadhaa. Bwana awapokee mbinguni wale wote waliopoteza maisha na kuwafariji watu wale ambao wamejaribiwa namna hiyo kwa miaka ya mzozo. Na tumwombe sasa Malkia wa amani, Mama, ambaye ni msimamaizi wa  Kanisa kuu hilo. Na kwake Papa amemkabidhi familia zote, wagonjwa na kila mmoja wao, wasiwasi wao na yote yaliyo mioyoni mwao.

Papa wakati wa sala ya Malaika wa Bwana huko Asti
20 November 2022, 12:53