Tafuta

Majilio ni safari ya maisha ya kiroho, inayomwandaa mwamini kumpokea Mtoto Yesu anayezaliwa kati yao. Majilio ni safari ya maisha ya kiroho, inayomwandaa mwamini kumpokea Mtoto Yesu anayezaliwa kati yao.  

Kipindi Cha Majilio Jiandaeni Kumpokea Mwana wa Mungu, Mfalme wa Amani

Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 14 Desemba 2022 amewakumbusha waamini kwamba, Majilio ni safari ya maisha ya kiroho, inayomwandaa mwamini kumpokea Mtoto Yesu anayezaliwa kati yao. Huyu ndiye Mwana wa Mungu aliyehai; Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele na Mfalme wa Amani. Jiandaeni zaidi kiroho!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Majilio ni kipindi cha upendo, matumaini, furaha na amani inayobubujika kutoka kwa Kristo Yesu na Kanisa lake. “Kwa kuadhimisha kila mwaka liturujia ya majilio, Kanisa linahuisha kule kumngojea Masiha, likijiweka katika ushirika wa maandalizi marefu ya ujio wa kwanza wa mwokozi, waamini wakiamsha upya tamaa ya ujio wake wa pili.” (KKK 524). Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano tarehe 14 Desemba 2022 amewakumbusha waamini kwamba, Majilio ni safari ya maisha ya kiroho, inayomwandaa mwamini kumpokea Mtoto Yesu anayezaliwa kati yao. Huyu ndiye Mwana wa Mungu aliyehai; Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele na Mfalme wa Amani.

Kristo Yesu ni Mwana wa Mungu na Mkombozi wa Ulimwengu
Kristo Yesu ni Mwana wa Mungu na Mkombozi wa Ulimwengu

Waamini wanakumbushwa kamba, Kipindi cha Majilio ni muda muafaka wa kukesha katika: Tafakari ya Neno la Mungu, Maisha ya Sala na Sakramenti za Kanisa mambo yanayomwilishwa katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili, kielelezo cha imani tendaji. Kipindi cha Majilio iwe ni fursa ya kusimama kidete katika maisha ya Kikristo, kwa kutoa kipaumbele cha pekee kwa maskini na wahitaji zaidi, wanaobisha hodi katika malango ya nyoyo za waamini wakihitaji kuonjeshwa faraja. Na kwa njia hii, anasema Baba Mtakatifu Francisko waamini wataendelea kujikita katika maisha yao kwa kufanya mang’amuzi mintarafu tunu msingi za maisha ya Kiinjili, daima wakikesha katika hali ya unyenyekevu na uwajibikaji wa pamoja. Majilio ni kipindi cha kujenga na kudumisha umoja na mshikamano wa udugu wa upendo.

Majilio kiwe ni kipindi cha mshikamano wa upendo na udugu
Majilio kiwe ni kipindi cha mshikamano wa upendo na udugu

Kwa namna ya pekee kabisa, Baba Mtakatifu amewapongeza na kuwashukuru watu wa Mungu nchini Poland ambao wameendelea kujipambanua kwa kuwasaidia waathirika wa vita nchini Ukraine pamoja na waathirika wa majanga asilia, sehemu mbalimbali za dunia. Kwa hiyo Yesu akasema nao tena akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu ye yote akinifuata hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru yenye kuleta uzima.” Yn 8:12. Baba Mtakatifu anakiri kwa kusema kwamba, kwa hakika watu wanahitaji mwanga wa amani kutoka Bethlehemu alikozaliwa Mtoto Yesu. Huu ni mwaliko kwa waamini kumwomba Mwenyezi Mungu ili aweze kuwakirimia zawadi ya amani ya kudumu, inayomwajibisha mwanadamu kuilinda, kuitetea na kuidumisha.

Kipindi cha Majilio
14 December 2022, 14:03