Papa amemkumbuka Papa Benedikto XVI:anamshukuru Mungu kwa ukarimu wake!
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko ameadhimisha Masifu ya Kwanza ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama Mtakatifu wa Mungu katika Kanisa kuu la Mtakatifu Petro Vatican na kwa kuhitimisha kwa wimbo wa mwisho wa Te Deum wa shukrani, Jumamosi jioni tarehe 31 Desemba 2022, siku ambayo amefariki Papa Mstaafu Benedikto XVI na katika mahubiri yake amemkumbuka “kwa hisia kali na shukrani kwa Mwenyezi Mungu ya kumtoa zawadi kwa Kanisa na kwa ulimwengu, kwa mema yote yaliyofanywa, na zaidi ya yote kwa ushuhuda wake wa imani na sala, hasa katika miaka hii ya mwisho ya maisha yake ya kustaafu”. Mada iliyoongoza mahubiri ya Papa Fransisko ni fadhila ya wema na ukarimu ambao si wema wa Kikristo peke lakini pia kiraia ambao unaweza kufanya ulimwengu kuwa wa kindugu zaidi. Papa Francisko kwa maana hiyo akianza mahibiri yake amesema “Alizaliwa na mwanamke( Gal4,4). Ilipotimia wakati, Mungu alijifanya mtu hakuja ulimwenguni kwa kuanguka kutoka juu mbinguni; alizaliwa na Maria. Hakuzaliwa katika mwanamke bali na mwanamke. Ni jambo tofauti kwani ina maana ya kusema kuwa Mungu alitaka kuchukua mwili kutoka kwake. Hakumtumia, lakini aliomwomba ile ndio ya kukubali. Na hapo akaanza pole pole mchakato wa mimba ya ubinadamu usio na dhambi na uliojaa neema na ukweli, uliojaa upendo na uaminifu. Ubinadamu mzuri, mwema na wa kweli, sura na mfano wa Mungu, lakini wa mwili wetu ulitolewa kwa Maria; hakuna kama yeye aliwahi kusema ndio, kwa uhuru, kwa kujitoa bure, katika heshima na katika upendo.
Hii ni njia ambayo alichagua Mungu ili kuingia ulimwenguni na katika historia, na huo ndio mtindo. Na mtindo huo ni muhimu kwa namna yake alivyokuja. Umama wa kimungu wa Maria, umama wa ubikira, umama unaozaa, ni njia ainayoonesha heshima kubwa sana ya Mungu kwa ajili ya uhuru wetu. Yeye ambaye alituumba pasipo sisi, hawezi kutuokoa pasipo sisi ( Mt. Agostino, CLXIX, 13).) Mtindo wake wa kuja kutuokoa ni njia ambayo hata hivyo inatualika kuifuata, kwa ajili ya kuendelea pamoja Naye ili kusuka ubinadamu mpya, huru, na uliopatanishwa. Ni mtindo,na namna ya kuhusiana kwetu ambako kunatokana na fadhila nyingi za kibinadamu, za kuishi vema na kwa hadhi. Moja ya fadhila hizi ni ukarimu, kama mtindo wa maisha ambayo yanasaidia udugu na urafiki kijamii (Fratelli tutti 222-224). Baba Mtakatifu Francisko amebaninisha kuwa: “Kwa kuzungumzia juu ya ukarimu, katika wakati huu wazo kuu lilikwenda kwa “Mpendwa Papa Mstaafu Benedikto XVI ambaye leo asubuhi ametuacha. Kwa hisia kali tunamkumbuka kwa namna hiyo mtu mkuu na mkarimu. Na tunahisi katika moyo wa shukrani kubwa: shukrani kwa Mungu kwa kumtoa kwa ajili ya Kanisa na Ulimwengu; shukrani kwake, kwa wema wote alioutimiza, hasa kwa ushuhuda wa imani na sala, hasa katika miaka ya mwisho wa maisha ya ndani. Ni Mungu peke yake anajua thamani na nguvu yake ya maombi na sadaka zake alizotoa kwa wema wa Kanisa”, Papa amethibitisha.
Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema: “ Jioni hii ninataka kupendekeza ukarimu hata kama fadhila za kiraia, kwa kufikiria kwa namna ya pekee Jimbo letu la Roma”. Ukrimu ni mktadha muhimu wa utamaduni wa majadiliano, na majadiliano ni muhimu kwa ajili ya kuishi kwa amani, kama ndugu ambao si kwamba wanaelewana daima, ni kawaida, lakini ambao wanazungumza, wanasikilizana na wanatafuta kuelewana na kuingilia kati pamoja. Ni kufikiria tu kwamba ulimwengu ungekuwaje bila mazungumzo ya uvumilivu kwa watu wengine wakarimu ambao walijaribu kuunganisha familia na jumuiya. Majadiliano yasioisha na jasiri hayafanyi habari kama migongano na migogoro, licha ya hayo yanasaidia kifaragha ulimwengu kuishi vizuri (Ft 198). Kwa hiyo ukarimu ni sehemu ya majadiliano. Sio suala la sheria na wala masuala ya kauli mbiu, mtindo wa uhakika… hainamanishi hili kwa kuzungumzia ukarimu. Kinyume chake ni fadhila za kurudisha na kufanyia matendo kila siku, kwa kwenda kinyume na fikira za mitindo ya kisasa, na kufanya jamii yetu kuwa ya kibinadamu. Kiukweli, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa, madhara ya ubinafsi, kuhusu hutumiaji hovyo, huko machoni pa wote. Na madhara makubwa zaidi ni kwamba wengine, ambao wanaotuzunguka, wanaeleweka kama vizingiti vya utulivu wetu, na katika usalama wetu. Wengine, wanatusumbua, wanatupotezea muda wetu na rasilimali za kuweza kufanya kile tunachotaka na kupenda. Jamii ya kibinafsi na inayotumia hovyo inakuwa na uchokozi, kwa sababu wengine ni washindani wa kushindana nao (FT 222). Pamoja na jamii hizi zetu na hata katika hali ngumu zaidi, kuna watu ambao wanajionesha kama vile kuna uwezekano wa kuchagua ukarimu na hivyo mtindo wao wa maisha unageuka kuwa mtindo huo katikati ya giza.
Baba Mtakatifu Francisko katika tafakari yake ameendelea kukazia kwamba Mtakatifu Paulo katika Barua yake kwa Wagalatia iliyosomwa katika liturujia hiyo, alizungumzia juu ya matunda ya Roho Mtakatifu,na kati ya matunda hayo anataja kwa neno la Kigiri chrestotes (taz 5,22). Kwa hiyo ukarimu ndio tunaweza kuutegemea kama mtindo wa wema, ambao unasaidia na kufariji wengine kwa kuzuia kila dharau na ugumu. Mtindo ambao unaweza kutumika kwa jirani kwa kufanya kuwa makini bila kumkwaza kwa maneno au kwa ishara, kwa kutafuta kupunguza uzito wa mwingine, kwa kumtia moyo, kumpa nguvu, kumfariji na kamwe kutomdhalilisha, au kumdharau(Ft 223). Ukarimu ni dawa dhidi ya baadhi ya magonjwa ya jamii yetu: dhidi ya ukatili, ambao kwa bahati mbaya unaweza kuharibu, kama vile sumu katika moyo na kuweka sumu katika uhusiano; dhidi ya wasiwasi na haraka nyingi ambazo zinatufanya kujifikiria binafsi na kuwabagua wengine. (Ft 224). Magonjwa haya, ya maisha yetu ya kila siku, yanatufanya kuwa washambuliaji na wasio na uwezo wa kuomba ruhusa, au hata samahani, au hata kusema neno dogo tu la “Asante”. Na ndivyo hivyo inapotokea katika njia, au dukani, au katika ofisi tunapokutana na mtu mkarimu tunabaki tumeshangaa, na utafikiri ni muujiza mdogo, kwa sababu kuwa ukarimu kwa sasa sio jambo la kawaida. Lakini shukrani kwa Mungu wapo bado watu wakarimu, ambao wanajua kuweka pembeni wasi wasi wao ili kutoa umakini kwa wengine, kutoa zawadi ya tabasamu, neno la kutia moyo, kwa kusikiliza mwingine mwenye kuhitaji msaada na hata kujieleza vya kutosha( FT).
Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo Papa amekazia kuwa kurudisha ukarimu kama fadhila binafsi na ya kiraia, inaweza kusaidia na sio kidogo kuboresha maisha katika familia, katika jumuiya na katika miji. Kwa maana hiyo mwaka huu mpya wa Jiji la Roma. Amependa kutoa matashi mema kwa wote ambao wanaishi humo kukua katika fadhila hiyo ya ukarimu. Uzoefu unafundisha kuwa ukarimu ikiwa unakuwa mtindo mmoja wa maisha, unaweza kuunda kuishi vema, kwa kuweka ubinadamu ule uhusiano wa kijamii na kuyeyusha ushambuliaji na sintofahamu. Papa akitazama picha iliyokuwa imepambwa kwenye Kanisa, Papa: “Ameomba kutazama picha ya Mama Bikira Maria. Leo na kesho, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, tunaweza kumuheshimu katika picha ya Mama wa Karmine wa Avigliano huko Potenza”. Tusidharau fumbo la Mama wa Mungu! Tuache tushangazwe na uchaguzi wa Mungu, ambao ungeonekana katika ulimwengu kama mitindo elfu ikionesha ukuu wake na kinyume chake alipendelea kufanyika mwili kwa uhuru kamili katika umbu la Maria, alipendelea kuumbika kwa miezi tisa kama mtoto na hatimaye kuzaliwa kwake, kuzaliwa na mwanamke. Hatuwezi kwa haraka kukaa na kutafakari yote kwa sababu ni suala muhimu sana la fumbo la wokovu. Kwa maana hiyo ni kutazama katika kujifunza mtindo wa Mungu, heshima yake isiyo na kikomo kwa namna ya kusema ukarimu wake kwa sababu katika umama wa Kimungu wa Bikira Maria kuna njiia kwa ajili ya ulimwengu wa kibinadamu zaidi.