Papa Francisko:amani na kusitisha silaha inawezekana
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Alhamisi tarehe 8 Desemba katika Siku Kuu ya Bikira Maria Mkingiwa wa dhambi ya Asili, Papa Francisko amewasalimia waamini na mahujaji waliofika kuanzia na warumi na wengine wote. Kwa namna ya pekee salamu zake zimeelekezwa kwa Harakati ya Wakristo wafanyakazi na wawakilishi wa Rocca di Papa na miengieyao ambayo itawasha nyota za siku Kuu ya kuzaliwa kwa Bwana katika mlima wa eneo lao.
Amekumbusha jinsiambavyo katika Siku Kuu ya Mkingiwa kiutamaduni Chama Katoliki cha matendo ya vijana wanapyaisha wajibu wao tena. Wazo lake limewaendea vyama vyote vya majimbo na maparokia, akiwatia moyo wa kuendelea mbele kwa furaha na huduma ya Injili na kwa Kanisa.
Papa ametoa taarifa ya kwenda mchana katika Kanisa la Bikira Maria Mkuu na kusali mbele ya Picha ya Bikira Maria afya ya Warumi na baadaye kwenda kwenye Uwanja wa Hispania ili kutimiza tendo la kiutamaduni kwa ajili ya heshima na maombi chini ya Picha ya miguu ya Mkingiwa. Kwa maana hiyo aliwaomba waamini wote kuungana naye "kiroho katika ishara hiyo ambayo inaelezea ibada ya kimwana kwa Mama yetu ambaye kwa maombezi yake, tunamkabidhi shauku ya ulimwengu wa amani, kwa namna ya pekee kwa nchi inayoteseka sana ya Ukraine."
Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema “Ninafikiria maneno ya Malaika kwa Bikira: “Hakuna lisilowezekana kwa Mungu” (Lk 1:37). Kwa msaada wa Mungu, amani inawezekana; na kupokonywa silaha kunawezekana. Lakini Mungu anataka mapenzi yetu mema. Mama Yetu atusaidie tuongekee ishara za Mungu”. Amewatakia kila mmoja siku kuu njema ya Mkingiwa na kuwatakia safari mje ya majio kwa wote lakini basi wasisashu kumwombea.
Katika habari za saa chache zilizopita zinabainisha juu ya shambulio la kombora la Urusis lililopiga kituo cha usafiri cha mji wa kusini wa Mykolaiv, hapakuwapo na waathirika. Aidha, makombora ya Kirussi katika eneo la Dnepropetrovsk yaliendelea usiku kucha, hasa kwa Nikopol, Nikolay Lukashuk, mwenyekiti wa baraza la kikanda la Dnepropetrovsk, aliripoti katika Telegram. Kulingana na Kituo cha Kitaifa cha Upinzani cha Jeshi la Kiukreni, kilichoripotiwa na Kyiv Independent, mamlaka ya uvamizi ya Urussi inawaondoa kwa nguvu wagonjwa raia kutoka hospitali katika sehemu inayokaliwa ya mkoa wa Lugansk, hata kama bado hawajamaliza matibabu.