Papa Francisko:hakuna kitu kinachopotea kwa amani.Kitu chochote kinaweza kuwa na vita
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Kitabu chenye kichwa:“Waraka kuhusu amani Ukraine”,kilichoandikwa na Francesco Grana toleo la Terra Santa, ambacho kinakusanya hotuba za Baba Mtakatifu kuhusu migogoro ya Ulaya,dondoo za kitabu zimetolewa na gazeti 'Il Fatto Quotidiano' wakati huo huo katika utangulizi wa kitabu hicho Baba Mtakatifu anaandika kuwa: “Sijawahi kuona mahali ambapo Bwana alianza miujiza bila kuumaliza vizuri”. Tangu zamani miaka mingi iliyopita niliposoma na nilirudia kusoma mara kadhaa liwaya ya “I promessi sposi di Alessandro Manzoni”, yaa ahadi za wenzi iliyoandikiwa na Alesaandro Manzoni, daima nilitafakari kwa muda mrefu kuhusu sentensi hiyo. Ni sentensi ya tumaini, wakati tukianza mchakato wa safari kuekelea Jubilei ya 2025, ambayo kauli mbiu nilipendelea ijikite labda katika fadhila hiyo ya kitaalimungu: “Wahujaji wa matumaini.” Papa Mtaafu Benedikto XVI alitupatia waraka wa kushangaza kuhusu matumaini, uitwao ‘Spe salvi’, (Nov30,2007 katika tumaini tulikombolewa.
Yeye anaandika kuwa “ukombozi, wokovu, sio ukweli peke yake tu kwa mujibu wa imani ya kikristo, bali ukombozi ulitolewa kwa maana kwamba alitupatia tumaini, tumaini moja la kuaminika, katika fadhila ambazo tunaweza kukabiliana na wakati wetu uliopo, ambao wakati wenyewe mgumu, unaweza kuuishi kwa kukubali ikiwa unatupeleka kuelekea hatima na ikiwa hatima hiyo tunaweza kuwa na uhakika, na ikiwa hatima hiyo ni kubwa namna ya kuhalalisha ugumu wa mchakato wa safari. Haya ni matukio ambayo kila mmoja wetu yamepata katika maisha yetu na ambayo huturuhusu kukabiliana na anguko letu la kila siku, tukiwa na uhakika kwamba Bwana hutushika mkono na kutuinua juu kwa sababu hataki tubaki chini. Mara nyingi nimekumbusha “kwamba inaruhusiwa kumtazama mtu kutoka juu tu ili kumsaidia kuinuka na hakuna cha zaidi. Ni katika hilo tu ndipo inaruhusiwa kumtazama kutoka juu hadi chini. Lakini sisi Wakristo tunapaswa kuwa mtazamo kama wa Kristo, ambaye anakumbatia kutoka chini, ambaye huwatafuta waliopotea, kwa huruma. Huu ni, na lazima uwe, mtazamo wa Kanisa, daima, kuwa na mtazamo wa Kristo, sio mtazamo wa kulaani."
Vita vya Ukraine, ambavyo mara baada ya kuibuka, vilihoji kila mmoja wetu, hasa kwa kufikiria kwamba, baada ya miaka ya kushangaza ya janga la uviko, wakati ambapo hapakukosa shida na majanga mengi na hatimaye tulikuwa ndio tunatoka katika awamu yake kali zaidi, kwa nini hofu ya mzozo huu usio na maana na wa kufuru umefika, kama vile kila vita? Je, tunaweza kusema kwa ujasiri juu ya vita vya haki? Je, tunawezaje kusema kwa ujasiri juu ya vita vitakatifu? Sisi, watu wa Mungu tunaotangaza Injili ya Mfufuka, tunao wajibu wa kupaza ukweli huu wa imani. Mungu ni Mungu wa amani, upendo na matumaini. Mungu ambaye anataka sisi sote tuwe ndugu, kama vile Mwanawe Yesu Kristo alivyotufundisha. Vitisho vya vita, vya kila vita, huchukiza jina takatifu zaidi la Mungu. Na vinamchukiza hata zaidi ikiwa jina lake linatumiwa vibaya ili kuhalalisha mauaji hayo yasiyosemeka. Kilio cha watoto, wanawake na wanaume waliojeruhiwa na vita kinapanda kwa Mungu kama maombi ya shauku kwa moyo wa Baba. Je, tutalazimika kushuhudia misiba mingapi zaidi kabla wale wote wanaohusika katika kila vita hawajaelewa kwamba hii ni njia ya kifo tu inayowadanganya baadhi tu kwamba wao ndio washindi? Ili iwe wazi: kwa vita sisi sote tumeshindwa! Hata wale ambao hawakushiriki katika hilo na ambao, kwa kutojali kwa woga, wamesimama karibu na kutazama utisho huu bila kuingilia kati kuleta amani.
Sisi sote, kwa nafasi yoyote ile, tuna wajibu wa kuwa watu wa amani. Hakuna aliyetengwa! Hakuna mtu ana haki ya kuangalia upande mwingine. “Katika ulimwengu huu wa utandawazi tumeangukia katika utandawazi wa kutojali. Tumezoea mateso ya mwingine hayatuhusu sisi hatujali wala hayatuhusu! Kwa maana hiyo inarudi picha ya Manzoni isiyo na jina. Utandawazi wa kutojali unatufanya sisi sote 'kutotajwa', kuwajibika bila jina na bila uso. Katika mkesha wa kuzuka kwa Vita vya Pili vya Ulimwengu, Mtumishi wa Mungu Papa Pio XII alikumbusha ulimwengu kwamba “hakuna kitu kinachopotea kwa amani. Kitu chochote kinaweza kuwa na vita. Ebu basi watu warudi tena kuelewana. Waanze tena mazungumzo. Kwa kujadiliana kwa nia njema na kwa kuheshimu haki za kila mmoja wao, wataweza kuona kwamba mazungumzo ya dhati na yenye ufanisi kamwe hayazuiwi katika mafanikio ya heshima”. Baba Mtakatifu Francisko aidha anandika: Ninamshukuru sana Francesco Antonio Grana kwa sabab amekusanya miito yangu yote ya amani nchini Ukraine. Vile vile ninashukuru gazeti , ‘il fattoquotidiano’ kwa sababu, tangu mwanzo wa mzozo huu, daima limekuwa likitoa mwangwi mpana kwa maneno yangu haya. Kama walivyo kwa wanaume na wanawake wengine wengi ambao wamekuwa wabebaji wa ujumbe huu, mara nyingi kwa uthabiti na kwa ukimya.
Kile mlicho nacho mikononi mwenu ni maandishi ambayo yanakusanya kile ambacho katika miezi hii ya vita kimetoka moyoni mwangu nikiona picha za mkasa huu mkubwa na kusoma habari za kutisha za migogoro hiyo na mingine mingi ulimwenguni ambayo mara nyingi husahaulika. Aina ya shajara ya vita ambayo ninawapatia wasomaji kwa matumaini kwamba hivi karibuni itakuwa shajara ya amani na juu ya yote onyo kwa kila mtu kutorudia matukio kama haya tena. Ni Waraka mmoja wa kweli kuhusu na kwa ajili ya amani nchini Ukraine na katika kila sehemu nyingine ya dunia. Wakati tunaendelea kuombea amani nchini Ukraine, bila kuchoka, hatupaswi kuzoea vita hivi kama vingine. Hatupaswi kuruhusu mioyo na akili zetu kusinzia katika uso wa marudio haya maovu, makubwa sana dhidi ya Mungu na dhidi ya mwanadamu. Hatupaswi, kwa sababu yoyote ile duniani, kuzoea haya yote, karibu tuchukue kwa uzito vita hivi vya tatu vya dunia ambavyo kwa kiasi kikubwa vimekuwa, mbele ya macho yetu, vita kamili ya tatu ya dunia. Tuombe amani! Tunafanya kazi kwa ajili ya amani! kwa uhakika kwamba Bwana Yesu, Mfalme wa Amani, ataipatia nchini Ukrane na ulimwengu mzima, hasa pale ambapo milipuko mingi ya vita bado inaendelea, mapambazuko ya asubuhi ya Pasaka.