Tafuta

2022.12.03 Papa amekutana na waliotoa zawadi ya Mti wa mapambo  na Pango kwa ajili ya Noeli vilivyo pambwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican. 2022.12.03 Papa amekutana na waliotoa zawadi ya Mti wa mapambo na Pango kwa ajili ya Noeli vilivyo pambwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican. 

Papa Francisko:Katika kufurahia Noeli tugundue kwa upya udogo wa Mungu!

Papa akikutana na ujumbe kutoka Sutrio,Rosello na Guatemala kwenye Ukumbi wa Paul VI,ambao walishiriki zawadi ya mti wa mapambo,utengenezaji wa Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli mwaka huu,amewaalika kutafakari juu ya umuhimu wa ukimya,ambao husaidia kuwa karibu na Mungu.Ni vema kugundua kwa upya udogo wa Mungu.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican, tarehe 3 Desemba 2022 na ujumbe uliotoa zawadi ya Pango na Mti wa kupambwa kwa ajili ya Siku Kuu ya Kuzaliwa kwake Bwana Wetu Yesu Kristo 2022, ambapo mkutano huo umefanyika katika, siku ambayo waliwakilisha pango likiwa limemalizika kutengenezwa na mti huo uliowekwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, pamoja na Pango lilopambwa kwenye Ukumbi wa Paulo VI. Baba Mtakatifu amewasalimia kwa upendo huku akianzia na Askofu wa Trivento na paroko wa Sutrio, kwa uwepo wa Askofu Mkuu wa Udine na kumshukuru kwa maneno yao ya ukarimu. Hakusahau kuwasalimia mamlaka ya kiraia waliokuwapo kwa namna ya pakee Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje  nchini  Guatemala, na Mkuu wa Mkoa wa Friuli Venezia Giulia, Mkaguzi wa Mkoa wa Abruzzo na Mameya wa Sutrio na Rosello.

Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli
Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli

Baba Mtakatifu Francisko aidha amewashukuru kwa zawadi ya ishala hizo muhimu za siku kuu ambazo amesema kwamba zitatazamwa na idadi kubwa ya wanahija kutoka sehemu mbali mbali za dunia. Amependa kuelekeza aidha wazo maalum kwa mafundi ambao wametengeneza sanamu za pango; kwa vijana wa kituo cha “Quadrifoglio” cha Rosello, walioandaa sehemu ya mapambo kwa ajili ya mti; na wale ambao walikuza miti huko Palena, mikubwa na midogo ambayo imeletwa katika mazingira mbali mbali ya Vatican. Utambuzi wa Baba Mtakatifu pia umewaendea mafundi na wakuu wa serikali tawala jijini Vatican ambao wanaongozwa na Kardinali Fernando Vergez na Sr.  Raffaella Petrini.

Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli
Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli

Akianza ufafanuzi wa ishara hizo, Papa amesema kwamba mti na pango ni ishala (Simbol) ambazo hadi leo hii zinaendelea kushangaza wadogo na wakubwa. Mti na taa zake zinakumbusha kuwa, Yesu anakuja kuangazia giza zetu, maisha yetu ambayo mara nyingi yamejifunga ndani ya kivuli cha dhambi, hofu na uchungu. Na ishara hizo zinashauri tafakari za kina, kama vile mti na jinsi ambavyo watu wanahitaji mizizi. Kwa kuwa ni katika kusimika mzizi kwenye ardhi nzuri, ndipo inabaki na msimamo na kukua hadi kukomaa, kwa kuvumilia pepo ambazo zinayumbisha na kugeuka kuwa kitu chenye msimamo mwema kwa yule anayetazama. Baba Mtakatifu kwa kuongeza amesema, lakini bila mizizi, yote hayo hayawezi kutokea kwa sababu bila msingi thabiti ni kubaki kuyumba yumba. Ni muhimu kuhifadhi mizizi, katika maisha kama ilivyo hata katika imani. Kwa mtazamo huo Mtakatifu Paulo alikumbusha msingi ambao maisha yanasimika mizizi  ili kubaki kidete kuwa “Wenye kujengwa katika Kristo (Kol 2,7). Na ndiyo kweli mti wa Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana ambao unakumbusha kubaki tumesimikwa katika Yesu Kristo”, amesisitiza Papa.

Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli
Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli

Kwa upande wa Pango amesema linazungumza wazi juu ya kuzaliwa kwa Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu ili kuwa karibu na kila mmoja wetu. Katika urahisi wake, pango linatusaidia kupata ukweli wa utajiri wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana na kututakasa na mantiki nyingi zinazochafua mazingira ya Siku kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana. Katika urahisi wa udogo na kifamilia, pango linakumbusha Noeli tofauti na ile ya kutumia hovyo na biashara; ni kitu kingine, kwani linatukumbusha jinsi gani ilivyo vema kuhifadhi vipindi muhimu vya ukimya na sala katika siku zetu ambazo mara nyingi zimegubikwa na uharaka wa kufanya. Ukimya unasaidia kutafakari Mtoto Yesu; unasadia kugeuka kwa undani na Mungu, na kwa urahisi wa mtoto aliyezaliwa; kwa unyenyekevu na upole wa kitoto kilicholala, na kwa upendo wa mavazi yaliyomfunika.

Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli
Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli

Baba Mtakatifu Francisko amerudia tena kuwa Mizizi na kutafakari ni mambo mawili muhimu kwani mti unatufundisha juu ya mizizi, na Pango linatualika kutafakari kwa kina, kwa maana hiyo amewaomba wasisahau mitazamo hiyo miwili ya kibinadamu na ya Kikristo. “Na ikiwa kweli tunataka kusherehekea Noeli,  hebu tugundue tena mshangao na mshangao wa udogo kupitia Pango, udogo wa Mungu, anayejifanya mdogo, ambaye hakuzaliwa katika uzuri wa kuonekana, lakini katika umaskini wa zizi. Ili kukutana naye ni lazima tumfikie huko, alipo; na tunahitaji kujishusha, tunahitaji kujifanya wadogo, tuache ubatili wote, ili tufike pale alipo”. Na sala Baba Mtakatifu ameongeza “ndiyo njia bora ya kusema asante mbele ya zawadi hiyo ya upendo isiyo na malipo, kusema asante kwa Yesu ambaye anataka kuingia katika nyumba na mioyo yetu.

Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli
Wawakilishi wa zawadi ya Mti na Pango kwa ajili ya Siku Kuu ya Noeli

Ndiyo, Mungu anatupenda sana kiasi kwamba anashiriki ubinadamu wetu na maisha yetu”. Baba Mtakatifu amesema “Hatuachi peke yetu, yuko upande wetu katika kila hali, katika furaha na maumivu. Hata katika nyakati mbaya zaidi, Yeye yuko pale, kwa sababu Yeye ni Emanueli, Mungu pamoja nasi, nuru inayoangazia giza na uwepo mwororo unaotusindikiza katika safari”. Baba Mtakatifu Francisko amepyaisha shukrani kwa zawadi za Kuzaliwa kwa Bwana, mti na pango na kwa kuwatakia kila mmoja wao, familia zao na jumuiya zao Siku Kuu njema  ya Noeli, akiwakabidhi kwa ulinzi wa Bikira Maria, Mama wa Mungu na Mama yetu. Kwa kuhitimisha amewaomba nao wasisahau kusali kwa ajili yake.

Hotuba ya Papa kwa watoa zawadi ya Pango,mti na mapambo ya siku kuu ya Noeli
03 December 2022, 15:40