Papa Francisko kwa Kikosi cha Zimamoto: Ninyi ni Kama Wasamaria Wema
Na Angella Rwezaula;– Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 10 Desemba 2022 amekutana na Kikosi cha Zima moto na uokoaji wa umma Kitaifa nchini Italia wakiwa na familia zao na mamlaka ya nchi takribani watu elfu tatu katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. Katika hotuba yake amewashukuru wote waliokuwapo, ikiwa ni pamoja na Bi Laura Lega Mkuu wa kikosi cha zima moto, uokoaji wa umma na idara ya ulinzi wa raia kwa hotuba yake kwa niaba ya wote. Katika mkutano huo amesema umempatia fursa ya kuelezea shukrani zake kwa kile wanachowakilisha na kile wanachofanya katika huduma ya pamoja, iwe huduma ya kila siku na hata katika dharura kubwa. Kati hizo Papa amekumbuka hata ya hivi karibuni ya maporomoko ya kisiwa cha Ischia, lakini pia wote wanajua uingiliaji wao mwingi katika huduma za matetemeko ya ardhi. Papa amebainisha alivyoweza kujionea mwenyewe wakati wa kutembelea baadhi ya maeneo nchini Italia na wema ambao walifanya kwa watu na urithi wa mazingira na historia ya kisanii katika hali kama hizo.
Kazi ya kimkakati kuhakikisha usalama
Kazi yao ya kimkakati na nguvu nyingine ni sura ya kuhakikisha hali za usalama na utulivu kwa maisha ya umma na zaidi kama walivyosema kwamba wakati wanapaswa kuwasaidia watu kuwaweka katika usalama kuna mikasa na hatari. Kujitoa kwao kwa maana hiyo ya uharaka, shauku, uwezekano wa kujisadaka ni mambo yanayoeleweka na watu wanawapongeza, amesisitiza Papa. Hata katika kesi nyingine na utume wao kuna hatarisha za maisha yao. Kwa maana hiyo utume wao ni uchaguzi binafsi na wa utambuzi ambao unahalalisha uwajibikaji wa kulinda watu na jumuiya wakati wa kuhitaji. Katika matazamio ya kikristo shughuli yao kwa namna ya pekee inajikita katika simulizi ya kiinjili kuhusu Msamaria aliyekuwa njiani na kukutana na mtu aliyeibiwa na kujeruhiwa na kwa ukarimu alimkaribisha, akamfunga majeraha na kumpandisha juu ya mnyama wake na kumpeleka katika nyumba ya wageni atunzwe. (Lk 10,33-35). Kifungu hicho Papa amesema ni kuelezea wazo mbadala wa kimya ambao tunapaswa kutumiza ili kujenga upya ulimwengu huu ambao unatia huruma. Mbele ya uchungu na majeraha mengi, njia moja ya kuondokana ni kuwa kama Msamaria mwema (Ft 67). Mtu huyo alionesha upendo na uwezekano wa kumsaidia aliyekuwa njiani na uhitaji mkubwa sana.
Kutojali na kugeuza visogo mbali
Na hii wakati wengine wengi kwa sababu ya kutojali au kwa ugumu wa mioyo yao wanageuza visogo vyao mbali. Msamaria mwema pia anatufundisha kwenda zaidi ya dharura na kutayarisha, na tunaweza kusema, ni masharti ya kurudi katika hali ya kawaida. Kiukweli, baada ya kutoa huduma ya kwanza, alimpeleka mtu aliyejeruhiwa hotelini na kumkabidhi kwa mwenye hoteli ili apone. Mhusika mkuu wa mfano huu anatuonesha huruma na upole wa Mungu; anatuambia kuwa udugu ni jibu la kujenga jamii bora, kwa sababu mgeni ninayekutana naye akiwa amejeruhiwa njiani ni ndugu yangu. Na wao kama, Wazima moto, wanawakilisha mojawapo ya maneno mazuri zaidi ya utamaduni wa muda mrefu wa mshikamano wa watu wa Italia, ambao una mizizi yake katika kujitolea kwa kiinjili.
Kutokana na hilo Papa amewaomba watunze na kuulinda urithi huo wa kimaadili na wa kiraia, na kwanza kabisa kuukuza katika maisha yao binafsi. Kwa hakika, taaluma yao ni mojawapo ya fani ambazo zina tabia ya utume: utume wa huduma kwa watu wakati wa shida, kuanzia katika dharura ndogo hadi kubwa zinazoweza kutokea; utume wa huduma kwa utu wa watu, ambao kamwe haupaswi kuachwa wakati wa shida; dhamira ya huduma kwa manufaa ya wote ya jamii ambayo, hasa wakati wa shida, kama vile ambayo tunapitia, inahitaji nguvu za akili timamu, zinazotegemeka na zinazofanya kazi katika kujificha.
Baba takatifu Franciso amesema, Noeli inakaribia na hivyo ni siku kuu ambayo kwa kila hali inachukua thamani ambayo ameewaomba kufanya: ukaribu, upendo, huruma; Mshikamano, huduma na udugu. Na haya yote yalifunuliwa kwetu, hayakuandikwa katika kanuni ya kutunzwa, bali yameandikwa katika mwili wa Mwana wa Adamu, Yesu. Hili ndilo jambo jipya la Kikristo ambalo halikomi kutushangaza: Mungu alikuja kutuokoa kwa kujifanya mtu mwenyewe, kama sisi. Alifanya kile wanachofanya: alikuja kusaidia katika hatari, kuokoa, na alifanya hivyo kwa njia nzito zaidi, akijua kwamba alipaswa kutoa maisha yake ili kuokoa wote. Yeye ni Msamaria Mwema wa wanadamu. Maadhimisho haya makuu ya Kikristo yawe fursa kwa kila mtu kugundua na kujionea jinsi Mungu anavyompenda mwanadamu, kila mwanadamu!
Katika hayo Papa Francisko amepyaisha shukrani kwa huduma yao ya thamani. Asante sana! Na wakati mwingine, ikiwa nina kitu cha kuwatamani ni kwamba wawe na kazi na kila wakati wapate kwenda huko. Bikira Maria aliyekwenda kwa haraka kwa binamu yake Elisabeth kumsaidia (Lk 1,39), wao daima wanakwenda kwa haraka wakati kuna dharura na hivyo Bikira awe ndiye mfano wao. Amewakabidhi kwa maombezi ya msimamizi wao Mtakatifu Barbara , amewabariki kwa moyo na familia zao, na wakati huo kuwaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.