Papa Francisko:tumkabidhi Mkingiwa sala kwa ajili ya amani nchini Ukraine
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana Baba Mtakatifu Francisko katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Dominika tarehe 4 Desemba 2022, amewasalimia wote kutoka Italia na sehemu mbali mbali: familia, parokia, vyama na kila mtu huku kwa kutazama bendera, zilizokuwa zinapepea kwenye uwanja kama vile za wahispania, wapoland, waargentinaa na wengine wengi, amewakaribisha, kwa namna ya pekee wanahija kutoka Madrid, Salamanca, Bolaños de Calatrava na La Solana.
Katika kuwasalimia wapoland, Baba Mtakatfu amependa kuwashukuru kwa wale wanaosaidia Siku ya Maombi na ukusanyaji wa fedha za Mfuko kwa ajili ya Kanisa Barani Ulaya Mashariki. Shukrani pia kuwapokea chama cha Matendo Katoliki na Askofu wao Spinillo; kama vile salamu kwa waamini wa Palermo, Sutrio na Saronno, vile vile vijana wa kipaimara wa Pattada, imbo katoliki la Ozieri, na wa parokia ya Mtakatifu Enrico, Roma.
Baba Mtakatifu Francisko hatimaye amewatakia wote Dominika njema na kuwaombe wawe na mwendelezo mwema wa mchakato wa safari ya Majilio. Hata hivyo Papa amewakumbusha jinsi ambavyo Alhamisi ijayo tarehe 8 Desemba 2022 ni siku kuu ya Bikira Maria Mkingiwa wa Dhambi ya asili. Kwa njia hiyo amesema “kwa njia ya maombezi yake, tumkabidhi sala kwa ajili ya amani, hasa kwa ajili ya nchi inayoteseka ya Ukraine. Amewaomba wasali kwa ajili yake na kuwaaga wawe na mlo mwema!