2022.12.18 Papa Francisko na watoto wanahudumiwa katika Zahanati ya Mtakatifu Marta Vatican. 2022.12.18 Papa Francisko na watoto wanahudumiwa katika Zahanati ya Mtakatifu Marta Vatican. 

Papa Francisko na Zahati ya Mtakatifu Marta:tusisahu watoto wa Ukraine!

Siku moja baada sherehe ya kuzaliwa,Papa ameshiriki sherehe ya kiutamaduni na wanaofanya kazi katika zahanati ya watoto,Vatican kwa msaada wa vifaa,matibabu na kiroho.Kulikuwa na baadhi ya familia za Ukraine wenyeji wa Roma,ambapo ametoa mwaliko kukumbuka wanaoteseka kwaa vita pia katika sehemu nyingine kwa ukosefu wa haki.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Siku moja baada ya siku kuu yake ya Kuzaliwa, Dominika tarehe 18 Desemba 2022 ameweza kushiriki kusherehekea na wale wanaofanya kazi katika kituo cha zahanati ya  watoto ya Mtakatifu Marta mjini Vatican kwa msaada wa vifaa, matibabu na kiroho. Pia mbele ya baadhi ya familia za Kiukreni ambazo ni  mwenyeji jijini  Roma, ambapo Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amewakumbuka na kuomba kuwasaidia wale wote wanaoteseka kutokana na vita,  pia katika sehemu nyingine nyingi za dunia , kutokana na ukosefu wa haki.

Papa asheherekea na watoto wanahudumiwa katika zahanati ya Mtakatifu Marta Vatican.
Papa asheherekea na watoto wanahudumiwa katika zahanati ya Mtakatifu Marta Vatican.

Baba Mtakatifu amewashukuru kila mmoja wao, kwa uwepo wao hapo na kwa siku hiyo ya furaha ambapo inawaanda kufikia Noeli.  Papa amebainisha kwamba “Na hatupaswi kusahau watoto wa Ukraine, na hakika msiwasahau! alionesha ishara kwa wale waliokuwa wanawakilisha na kusema “Amani”;  hapo, ninaona  kuna bendera ya Ukraine”.

Papa amesheherekea na watoto wanahudumiwa na zahanati ya Mtakatifu Marta Vatican.
Papa amesheherekea na watoto wanahudumiwa na zahanati ya Mtakatifu Marta Vatican.

“Watoto wengi wanateseka na vita; na pia wanateseka katika sehemu nyingine kutokana na dhuluma. Bwana awapatie furaha hii ya kusherehekea Noeli  namna hii, sisi sote kwa amani, tuwafikirie pia wale wanaoteseka na tuwaombee, sote kwa pamoja”.  Kwa maana hiyo Papa ameongeza  kuwashukuru na pia kuwaomba waendelee na tamasha lao.

18 December 2022, 15:53