Papa Francisko:'Noeli hii ni ya huzuni,Noeli hii ni ya Vita'
Na Angella Rwezaula; – Vatican
Hii ni Noeli ya kusikitisha, Noeli ya vita. Kuna watu wanakufa kwa njaa”. Papa alisema hayo katika mahojiano yaliyofanyika na mtaalamu wa mambo ya Vatican Fabio Marchese Ragona, katika vyombo vya Habari ya Mediaset na ambayo yaliweza kutangazwa baadaye Dominika usiku tarehe 18 Desemba 2022. Katika mahojiano hayo ya kipekee Papa aliomba wahausika wa vyombo vya Habari hasa wawe na na moyo mkuu na wasiende kufanya maamuzi kana kwamba hakuna kilichotokea. Kutojali ni moja ya mambo ambayo tunapaswa kupambana nayo sana na kama waandishi wa habari wana dhamira ya kuamsha mioyo ili wasiangukie katika utamaduni huo wa kutojali.
Kushuka kwa idadi ya watu Italia
Baba Mtakatifu Francisko alizingumza mambo mengi na miongoni mwa mada nyingine zilizoguswa, ni pamoja na ile ya majira ya kushuka kwa idadi ya watu nchini Italia ambapo alisema: “Mtoto ni tishio kwa wakati huu. Lakini tuko wapi? Mtoto anapaswa kuwa baraka. Ndio maana nadhani inabidi tuanze tena. Ninawambia, Waitaliano tafadhali muwe na watoto. Nchi inahitaji watoto tafadhali. Ubinafsi uwe mdogo”.
Mpango wa Upapa kwa maamuzi ya makardinali
Hii ndiyo milinganisho ya Papa, katika mkesha wa kumbukumbu ya miaka kumi kwamba: “Mimi nilipochaguliwa, nilichukua kama programu mambo yote tuliyosema na makadinali katika mikutano ya kabla ya mkutano kwa ajili ya kuchagua Papa ambaye angefuata na alikuwepo pale, lakini hakuna aliyekuwa anajua yeye ni nani. Kwa maana hiyo nilichukua hatua hii kama mchakato wa safari ya kwenda mbele. Pia kuna mambo ya kufanya, lakini ni kuendelea mbele. Ni vizuri kwa sababu makadinali waliokuwa hapo walinisaidia sana kufanya mabadiliko hayo. Mojawapo ya vitu mnavyoviona sana, ambavyo sio muhimu sana bali mnaloliona zaidi ni kusafisha uchumi, kuepuka mambo mabaya kiuchumi. Sasa taasisi hiyo iko imara. Baraza la Uchumi lilikutana siku hizi na linafanya kazi vizuri. Wametoa dalili za kuliendeleza hilo. Nilianza kufanya, kwa msaada wa kila mtu, kile ambacho makadinali walikuwa wameomba”.
Kila kitu kifanyika kwa roho ya kimisionari na kutangaza Injili
Baba Mtakatifu alisema kwamba lakini, zaidi ya yote, roho ya kimisionari, roho ya kimisionari katika kutangaza Injili. Hii ni muhimu kwa sababu tunaweza kuwa na curia iliyopangwa vizuri, parokia iliyopangwa vizuri, jimbo lililo na mpangilio mzuri, lakini ikiwa hakuna roho ya utume, ikiwa hakuna sala, mambo hayawezi kwenda vizuri na kwa sababu maombi ni muhimu.
Mabadiliko ya kiuchumi Vatican
Baadaye katika mabadiliko ya kiuchumi jijini Vatican, Papa alimpongeza Kardinali George Pell, aliyeanzisha mageuzi ya kiuchumi mjini Vatican kwamba baadaye ilimbidi akae karibu miaka miwili huko Australia kwa kashfa waliyomfanyia na ambayo hakuwa na hatia baada ya yote, lakini walimfanya kuwa mbaya, maskini na yeye aliweza kuacha utawala huo, ljapokuwa Kardinali George Pell, ndiye aliyeweka mpango wa jinsi gani tunavyoweza kusonga mbele. Yeye ni mtu mkubwa na tuna deni kwake kwa mambo mengi.”
Vita ya tatu duniani imegawanyika vipande vipande
Papa Francisko alisema kwa sasa tunaishi vita ya Tatu ambayo imemegeka vipande vipande, kwa mfano nchini Ukraine, lakini hata katika nchi ya Yemen, Siria, Myanmar na kwingineko ulimwenguni kama alivyozoea kuelezea. Hata hivyo alisisitiza kwamba vita hivi vya sasa nchini Ukraine vimepelekea ongezeko la bei na jambo ambalo linatishia ni lile la tabia ya sintofahamu na kashfa kwa yule ambaye hatazami hali halisi ya yule anayeteseka, kwa sababu ameteleza kuanzia na dhambi ya ufisadi.
Kombe la dunia: washindi waishi ushindi huo kwa unyenyekevu
Kwa upande wa mchezo wa mpia na kombe la dunia, ambapo mahojiano yalifanyika kabla ya ushindi wa nchi ya Argentina, Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amewaalika watakao kuwa washindi waweze kuishi ushindi huo kwa unyenyekevu.