Tafuta

Papa Francisko:Upendo,Neno &msamaha ni mambo makuu ya Stefano

Sisi tunaweza kuboresha ushuhuda wetu kwa njia ya upendo kuulekeza kwa ndugu,kuwa waaminifu wa Neno la Mungu na Msamaha.Kwa hiyo ni Upendo,Neno na Msamaha.Ni kutoka katika tafakari ya Papa Francisko kabla ya sala ya Malaika wa Bwana ambapo kila 26 Desemba Mama Kanisa anakumbuka Mtakatifu Stefano .

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Ikiwa ni siku ya Jumatatu tarehe 26 Desemba 2022, siku ambayo Mama Kanisa anakumbuka shuhuda wa kwanza wa Ukristo Mtakatifu Stefano, na ikiwa tuko katika oktava ya sherehe za Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu, Kristo, Baba Mtakatifu Francisko ametoa tafakari yake kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, kwa umati wa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akianza tafakari yake, Papa amewatakia Siku Kuu Njema na kubainisha jinsi ambavyo Dominika tumeadhimisha Siku ya kuzaliwa kwa Bwana na liturujia ambayo inatusaidia kumkaribisha vizuri kwa kuipanua hadi tarehe Mosi Januari, kwa maana hiyo siku nane.  Inashangaza lakini katika siku hizi kuona baadhi ya majanga ya sura za watakatifu mashahidi. Kwa mfano siku hii, Mtakatifu Strefano,  ambaye ni shahidi wa kwanza mkristo, tarehe 28 Desemba ni Siku ya watoto washahidi ambao waliuawa kwa agizo la Herode kwa kuogopa kuwa Yesu angemtoa katika kiti cha madaraka (Mt 2,1-18). Kwa hiyo basi liturujia utafikiri inataka kutupeleka mbali na ulimwengu wa mataa, meza za vyakula, zawadi ambazo kwa siku hizi tunaweza kufurahia kidogo. Je ni kwa nini?

Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana
Waamini katika sala ya Malaika wa Bwana

Kwa kujibu Papa amebainisha kuwa Noeli sio liwaya ya kitoto ya kuzaliwa kwa mfalme, lakini ni  kuja kwa Mwokozi, ambaye alitukomboa na mabaya kwa kubeba mwenyewe mabaya yetu kama vile ubinafsi, dhambi na kifo. “Huo ndio ubaya wetu, ubinafsi tulio nao ndani, dhambi ambazo sisi ni wadhambi na kifo”. Na mashahidi  wanafafanua zaidi na Yesu , wanashuhudia, kaka na dada ambo walipitia maisha yao, kwa kutuonesha Yesu kuwa alishinda ubaya kwa huruma. Na hata katika siku zetu, mashahidi wako wengi ambao ni zaidi kuliko nyakati za kwanza. Leo hii tuwaombe hao kaka na dada zetu mashahidi wanaoteswa, na ambao wanashuhudia Kristo. Lakini itakuwa vizuri kwetu tujaribu kujiuliza: sisi tunamshuhudia Kristo? Na tunawezaje kuboresha hilo la kushuhudia vizuri Kristo? Anaweza kutusaidia hasa  Mtakatifu Stefano.

Awali ya yote, katika Matendo ya Mitume, tunaambia kuwa Yeye alikuwa mmoja wa mashemasi saba na ambaye Jumuiya ya Yerusalemu ilikuwa imemweka wakfu kwa ajili ya kutoa huduma katika vituo vya kutoa chakula, kwa ajili ya upendo (Mdo 6,1-6). Hii ina maana kuwa ushuhuda wake wa kwanza hakuutoa kwa maneno tu bali kwa matendo ya kutunza. Kwa wale aliokuwa anakutana nao alikuwa anazungumza kuhusu Yesu, alikuwa anashirikisha imani kwa nuru ya Neno la Mungu na mafundisho ya Mitume ( Mdo 7,53.56). Huu ndio ukuu wa ushuhuda  wa kukaribisha Neno na kuwasilisha uzuri, kusimulia jinsi ambavyo kwa kukutana na Yesu kunabadilisha maisha. Suala hilo kwa upande wa stefano lilikuwa muhimu sana kiasi kwamba hakuogopeshwa hata kutishwa na watesaji na hata alipoona mambo yake yalikuwa yanakwenda vibaya. (Mdo 7, 54). Upendo na tanganzo ndiyo mambo makuu aliyojikita nayo Stefano. Lakini ushuhuda wake mkubwa zaidi ulikuwa ni jambo kubwa,ambapo alitambua vema kuunganisha upendo na tangazo. Aliacha hivyo wakati wa kifo, kwa mfano wa Yesu alipowasamehe waliomuua (Mdo 7,60; Lk 23,34) hivyo ni Upendo,tangazo na msamaha.

Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana
Papa Francisko wakati wa sala ya Malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea na tafakari hiyo, amejibu swali  la awali kwamba: “Tazama Sisi tunaweza kuboresha ushuhuda wetu kwa njia ya upendo kuulekeza kwa ndugu, kuwa waaminifu wa Neno la Mungu na Msamaha. Upendo, Neno na Msamaha. Ni msamaha unaosema kweli unatekeleza upendo kuelekeza wengine na ikiwa tunaishi kwa Neno la Yesu. Msamaha kiukweli ni kama neno lenyewe linavyoelekeza  zawadi kubwa zaidi, zawadi ambayo tunaifanya kwa wengine kwa sababu sisi ni wa Yesu, tuliosamehewa na Yeye. Mimi ninasamehe kwa sababu nilisamehewa, na sisi tunasahau hili Papa Francisko na hivyo ameomba kufikiria kila mmoja wetu, uwezo wa  kusamehe yaani: “uwezo wangu wa kusamehe hukoje katika siku hizi ambazo labda tutakutana, kati ya wengi,na baadhi ya watu ambao hatuelewani na ambao walituhumiza, ambapo hatukuweza kamwe kushona mpasuko kwa upya uhusiano.

Sala kwa ajili ya Amani duniani wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 26 desemba
Sala kwa ajili ya Amani duniani wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 26 desemba

Baba Mtakatifu amewaalika waamini na mahujaji kwamba: “Tumuombe Yesu aliyezaliwa sasa , yale ambauyo ni mapya ya moyo wenye uwezo wa kusamehe: sisi sote tunahitaji moyo ambao unasemehe. Nguvu ya kusali kwa ajili ya yule aliyetutendea mabaya, kusali kwa ajili ya yule aliyenikwaza na kunihumiza na kupiga hatua moja ya ufunguzi  wazi na upatanisho. Na  Bwana aweze kutupatia neema hiyo”. Kwa kuhitimisha Papa amesema na Maria, Malkia wa mashahidi, atusaidie kukua katika hisani, katika upendo kwa ajili ya Neno na katika msamaha.

26 December 2022, 12:17