Tafuta

2022.12.19 Papa amekutana na wakauu na wawakilishi wa Vyama vya wafanyakazi Italia(CGIL). 2022.12.19 Papa amekutana na wakauu na wawakilishi wa Vyama vya wafanyakazi Italia(CGIL). 

Papa kwa CGIL:kazi inaruhusu mtu kujikamilisha binafsi na kuishi kindugu!

Papa amekutana na shirikisho la vyama wa wafanyakazi Italia.Katika hotuba yake amekazia juu ya ajira:“Hakuna chama bila wafanyakazi na hakuna wafanyakazi huru bila chama.Hivyo kazi hujenga jamii na wajibu wa vyama ni kuelimisha kuhusu kazi yenye hadhi.Kufanya kazi kunamruhusu mtu kujikamilisha binafsi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumatatu tarehe 19 Desemba 2022 amekutana  na shirikisho la vyama wa wafanyakazi nchini Italia (CGIL) na kumshukuru Katibu Mkuu kwa hotuba yake.  Mkutano hu ona yeye  unaounda na mojawapo ya mashirika ya kihistoria ya vyama vya wafanyakazi, amebainisha inampa fursa ya  kuelezea kwa mara nyingine tena ukaribu wake kwa ulimwengu wa kazi kwa namna ya pekee watu  na familia ambao wanaishi kwa ugumu. Akinuu kufungu cha Laudato Si, Papa amebanisha kuwa “Hakuna chama bila wafanyakazi na hakuna wafanyakazi huru bila chama. Tunaishi katika enzi ambayo, licha ya maendeleo ya kiteknolojia na wakati mwingine hasa kwa sababu ya mfumo potovu unaojiita teknolojia (taz. Laudato si’, 106-114), sehemu fulani imekatisha tamaa matarajio ya haki katika muktadha wa kazi.

Na hii inahitaji awali ya yote kuanzia na thamani ya kazi kama sehemu ya kukutana kati ya wito binafsi na ukuu wa kijamii. Kufanya kazi kunamruhusu mtu kujikamilisha binafsi, kuishi  kindugu, kukuza urafiki kijamii na kuboresha ulimwengu. Katika nyaraka mbili ya ‘Laudato si’ na ‘Fratelli tutti’ zinaweza kuwasaidia kuingia kwenye mchakato wa mafunzo ambayo  yanatoa sababu za jitihada katika kipindi ambacho tunaishi. Baba Mtakatifu amebainisha kwamba “Kazi hujenga jamii. Ni uzoefu wa msingi wa uraia, ambapo jumuiya  hupata hatima inayochukua sura, matunda ya kujitolea na vipaji vya kila mtu; jumuiya hii ni zaidi ya jumla ya fani mbalimbali, kwa sababu kila mtu anajitambua katika uhusiano na wengine na kwa wengine. Na kwa hivyo, katika muundo wa kawaida wa uhusiano kati ya watu na mipango  ya kiuchumi na kisiasa, kiungo cha kidemokrasia kinapewa maisha siku baada ya siku.

Ni kiungo ambacho hakitengenezwi mezani katika jengo fulani, bali kwa bidii ya ubunifu katika viwanda, warsha, kilimo, biashara, makampuni ya mafundi, maeneo ya ujenzi, utawala wa umma, shule, ofisi, na mengine.” Papa Francisko amesisitiza kuwa ikiwa anawakumbush maono ya dira hiyo, ni kwa sababu moja ya kazi yao ya  chama ni ile ya kuelimisha kwa maana ya kazi, kukuza udugu miongoni mwa wafanyakazi. Kwa maana hiyo wasiwasi huo wa uundaji hauwezi kuachwa. Ni chumvi ya uchumi wenye afya, wenye uwezo wa kufanya dunia kuwa bora. Hakika, “gharama za kibinadamu daima pia ni gharama za kiuchumi na  kutofanya kazi kiuchumu daima upelekea hata gharama za kibinadamu pia. Kuacha kuwekeza kwa watu ili kupata faida zaidi ya haraka ni biashara mbaya kwa jamii(taz. Laudato si’, 128).

Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo amesema karibu na mafunzo, daima kuna ulazima wa kuelezea mateso ya kazi. Utamaduni wa ubaguzi unazidi kukunjua matamvua ya uhusiano kiuchumi ambao umevamia hata ulimwengu wa kazi.  Hayo yanaonekana kwa mfano mahali ambapo hadhi ya kibinadamu inakanyagwa na ubaguzi fulani, kwa sababu gani mwanamke anapaswa apate kidogo kuliko mwanaume? unaweza kuiona katika hatari ya ujana   kwa nini chaguzi za maisha zicheleweshwe kwa sababu ya hatari ya kudumu?; au tena katika utamaduni wa kupunguzwa kazi; na kwa nini kazi ngumu zaidi bado zinaifdhiwa wa walio hafifu? Watu wengi sana wanateseka kwa kukosa kazi au kazi zisizo na heshima: nyuso na vilio vyao vinastahili kusikilizwa na kujitolea kwa chama cha wafanyakazi.

Papa Francisko kwa maana hiyo ameelezea wasiwasi wake. Kwanza juu ya usalama wa kazi. Bado kuna vifo vingi na majeruhi katika maeneo ya kazi. Kila kifo kazini ni kushindwa kwa jamii nzima. Zaidi ya kuhesabu vifo kila mwishoni mwa mwaka, Papa amesema tunapaswa kukumbuka majina kwa sababu ni watu na wala sio namba. Tusiruhusu kuwaweka sawa na faida na watu! Uungu wa fedha una dhamira ya kukanyaga yote na wote na hailindi tofauti. Hii ni kuufanya  kuwa na moyo wa maisha ya wafanyakazi na kuwaelimisha kuchukua kwa uamuzi stahiki wa sheria juu ya  usalama. Na ni kwa hekima ya mshikamano tu inawezekana kuzuia ajali zile mbaya wa familia na jumuiya.

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha wasiwasi wake wa pili kuhusu unyonyasaji wa watu utafikiri ni mashine za kuazima. Kwa mujibu wake amesema kuna mitindo mbali mbali kama vile ya wafanyakazi katika mashamba na utumwa wa wafanyakazi kwenye kilimo, au katika shughuli za ujenzi na maeneo mengi ya kazi, inayolazimisha kufanya kazi kwa masaa mengi na mchezo wa kutokuwa na mikataba, aidha dharau ya likizo za mama waliojifungua na migogoro kati ya kazi na familia. Masawali ya kujiuliza ni kwamba “Ni mapingamizi mangapi yaliyopo, na vita vingapi kati ya maskini ambao wanasumbuka kazini?. Katika miaka ya mwisho imeongezeka kile kiitwacho “wafanyakazi maskini”, watu pamoja na kuwa na kazi lakini hawawezi kutunza familia zao na kuwapa matumaini ya wakati ujao.

Shirikisho la vyama vya wafanyakazi  kwa maana hiyo wanaitwa kuwa sauti ya wale ambao hawana sauti. Hasa, Papa amependekeza kuwa makini na vijana, ambao mara nyingi wanalazimishwa kuingia katika mikataba ya hatari, isiyofaa na ya utumwa. Amewashukuru kwa kila mpango unaohamasisha sera tendaji za kazi na kulinda hadhi ya  watu. Aidha katika miaka hii ya janga la uviko, kumekuwa na ongezeka la idada ya watu ambao wanawakilisha kujiuzulu kazini. Vijana na wasio vijana ambao hawaridhiki kipata cha  taaluma  yao kutolingana na hali wanayopumua kwenye mazingira ya kazini na hivyo wanapendelea kujiuzulu. Wanatafuta fursa nyingine. Jambo hilo haimaanishi kujitenga, lakini ni hitaji la kibinadamu la kazi. Pia katika kesi kama hiyo chama cha wafanyakazi kinaweza kufanya kazi ya kuzuia, ikilenga ubora wa kazi na kuwasindikiza watu kuelekea uhamisho unaofaa zaidi kwa talanta ya kila mmoja.

Papa Francisko amewaalika kuwa walinzi katika ulimwengu wa kazi, kwa kuzaa mshikamano na kupinga utasa. Watu wana kiu ya amani hasa katika kipindi hiki cha kihistoria, na kutoa mchango kwa wote ambao ni msingi. Kuelimisha amani hata katika maeneo ya kazini ambayo mara nyingi yamegubikwa na mgogoro ambapo inawezekana kugeuka ishara ya tumiani kwa wote hasa kwa kizazi kijacho. Amewashukuru kwa yote wanayofanya na watakayo endelea kufanya kwa ajili ya maskini, wahamiaji, watu wadhaifu na walemavu , pamoja na wasio na ajira. Amesisitiza  wasiache kuwahudumia katika matunzo hata wale wasiojiandikia katika ofisi za ajira kwa sababu wamepoteza matumaini; waweke nafasi ya uwajibikaji kwa vijana. Amewakabidhi kwa ulinzi wa Mtakatifu Yosefu, ambaye alitambua uzuri na ugumu wa kufanya mema katika kazi yake na kutosheka kwa kupata mkate kwa akili ya familia.  Ameomba watazame yeye na uwezo wake wa kuelemisha kwa njia ya kazi. Amewatakia Noeli njema na utulivu kwa wote na wapendwa wao.

Hotuba ya Papa kwa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Italia
19 December 2022, 15:25