Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 31 Januari 2023 hadi tarehe 5 Februari 2023 anafanya Hija ya Kitume nchini DRC na Sudan ya Kusini. Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 31 Januari 2023 hadi tarehe 5 Februari 2023 anafanya Hija ya Kitume nchini DRC na Sudan ya Kusini.   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Hija ya Papa Francisko Barani Afrika: Haki, Amani na Upatanisho

Lengo ni kutangaza na kushuhudia Neno la Mungu, Injili ya matumaini kwa wale waliovunjika na kupondeka moyo; amani na majadiliano katika ukweli na uwazi, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu katika nchi hizi mbili. Kardinali Pietro Parolin anasema, anatarajia kumsindikiza Baba Mtakatifu Francisko katika Hija yake ya Kitume nchini DRC na Sudan ya Kusini.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 31 Januari 2023 hadi tarehe 5 Februari 2023 anafanya Hija ya Kitume nchini DRC na Sudan ya Kusini. Lengo ni kutangaza na kushuhudia Neno la Mungu, Injili ya matumaini kwa wale waliovunjika na kupondeka moyo; amani na majadiliano katika ukweli na uwazi, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu katika nchi hizi mbili. Kardinali Pietro Parolin Katibu mkuu wa Vatican akitoa tamko rasmi kuhusu hija hii ya Kitume anasema, anatarajia kumsindikiza Baba Mtakatifu Francisko katika Hija yake ya Kitume nchini DRC na Sudan ya Kusini.

Papa Nchini DRC: Haki, amani na upatanisho wa kweli
Papa Nchini DRC: Haki, amani na upatanisho wa kweli

Baba Mtakatifu Francisko pamoja na mambo mengine, anapania kuwa ni hujaji wa amani, ili kusaidia kunogesha mchakato wa upatanisho, utakaosaidia kuleta faraja kwa Makanisa mahalia na watu wa Mungu katika ujumla wake; kwa kuwatia shime wananchi kujikita katika ustawi na maendeleo yao na hatimaye, kusaidia kuragibisha kuhusu hali ya watu wa Mungu Barani Afrika katika ujumla wake. Hili ni Bara kubwa linalo paswa kupewa uzito stahiki.

Parolin Tamko

 

28 January 2023, 15:46