Tafuta

Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea nchini DRC amepata bahati ya kupitia kwenye anga za Italia, Tunisia, Algeria, Niger, Chad, Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Cameroon, Congo na hatimaye akatua nchini DRC. Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea nchini DRC amepata bahati ya kupitia kwenye anga za Italia, Tunisia, Algeria, Niger, Chad, Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Cameroon, Congo na hatimaye akatua nchini DRC. 

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Nchini DRC: Mjumbe wa Amani na Upatanisho wa Kitaifa

Baba Mtakatifu ametumia fursa hii, kuwatakia viongozi wakuu wa nchi: heri, baraka, nguvu, amani na ustawi na maendeleo na kwamba, anawabeba watu wote wa Mungu katika nchi hizi katika sakafu ya moyo wake. Anawahimiza kujikita katika mchakato wa furaha, haki na upatanisho wa Kitaifa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Yeye ni Mjumbe wa amani na upatanisho.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Hija ya 40 ya Kitume ya Baba Mtakatifu nchini DRC kuanzia tarehe 31 Januari 2023 hadi tarehe 3 Februari 2023 inanogeshwa na kauli mbiu “Wote wapatanishwe katika Yesu Kristo.” Baba Mtakatifu Francisko, Jumanne tarehe 31 Januari 2023 ameanza hija yake ya kitume Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo, DCR. Kabla ya kuondoka kutoka katika Hostel ya “Santa Martha”, Baba Mtakatifu amekutana na kusalimiana na kikundi cha wakimbizi na wahamiaji kutoka DRC na Sudan ya Kusini, waliokuwa wamesindikizwa na Kardinali Konrad Krajewski Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo. Akiwa njiani kuelekea kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Fiumicino, Baba Mtakatifu amesimama kidogo na kutoa heshima zake kwa Mnara wa Askari waliouwawa Kindu nchini DRC., kunako tarehe 11 Novemba 1961 wakati wa machafuko ya kisiasa nchini DRC. Hawa ni Askari wa kulinda amani waliotumwa na Umoja wa Mataifa kwenda nchini DRC kutuliza ghasia zilizoibuka kutokana na vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini DRC. Miezi miwili kabla ya vita ya wenyewe kwa wenyewe, yaani tarehe 17 Septemba 1961, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati ule Dag Hammarskjöld, alikuwa amefariki kwa ajali ya ndege wakati akielekea mjini Katanga, kutafuta suluhu ya mgogoro ule wa kivita.

Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi mbalimbali.
Papa Francisko ametuma salam na matashi mema kwa viongozi mbalimbali.

Ndege za kivita kutoka Italia zilitumwa kwenda kuokoa wageni pamoja na kutoa msaada wa kibinadamu kwa watu waliokuwa wameathirika kwa vita. Askari hawa wakazikwa kwa heshima zote za Kitaifa tarehe 11 Machi 1962 mbele ya Rais Antonio Segni wa Italia. Baba Mtakatifu akiwa njiani kuelekea nchini DRC amepata bahati ya kupitia kwenye anga za Italia, Tunisia, Algeria, Niger, Chad, Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, Cameroon, Congo na hatimaye akatua nchini DRC. Baba Mtakatifu ametumia fursa hii, kuwatakia: heri, baraka, nguvu, amani na ustawi na maendeleo na kwamba, anawabeba watu wote wa Mungu katika nchi hizi katika sakafu ya moyo wake. Anawahimiza kujikita katika mchakato wa furaha, haki na upatanisho wa Kitaifa kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Baba Mtakatifu Francisko katika salam zake kwa Rais Sergio Mattarella wa Italia amemwelezea kwamba, alikuwa anafanya Hija ya Kitume nchini DRC na Sudan ya Kusini, ili kukutana na ndugu zake katika imani pamoja na watu wote wenye mapenzi mema. Anakaza kusema, anapenda kuwapekelekea ujumbe wa amani na upatanisho. Baba Mtakatifu Francisko anamwomba Rais Mattarella kumfikishia salam zake kwa watu wote wa Mungu nchini Italia. Anawaombea ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Papa ametoa heshima yake kwa askari waliouwawa nchini DRC kutoka Italia
Papa ametoa heshima yake kwa askari waliouwawa nchini DRC kutoka Italia

Wakati huo huo, Rais Sergio Mattarella wa Italia amejibu salam na matashi mema kutoka kwa Baba Mtakatifu Francisko akiwa njiani kuelekea nchini DRC na Sudan ya Kusini. Anamshukuru kwa matashi mema na kusema kwamba, hizi ni nchi ambazo kimsingi “zimepekenywa” na vita pamoja na umaskini wa hali na kipato. Kumbe, hija hii ya Kitume ni fursa ya kutangaza na kushuhudia ukaribu wa Kanisa, imani na matumaini kwa watu wote wanaoendelea kujisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kunogesha tunu msingi za kijamii kwa kuheshimiana, amani, utulivu na maridhiano; tunu msingi za ujenzi wa ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Rais Sergio Mattarella amepongeza pia juhudi za majadiliano ya kiekumene yanayosimikwa katika ushuhuda; changamoto na mwaliko kwa watu wote wa Mungu nchini Sudan ya Kusini, kusimama kidete kupinga aina zote za mipasuko na kizani na kuanza kujielekeza katika mchakato wa ujenzi wa umoja wa Kitaifa, utu na heshima ya watu wote.

Papa Salam
31 January 2023, 17:03