2023.01.02 Mwili wa Papa Benedetto umewekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na watu wanaendelea kutoa heshima zao za mwisho hadi siku ya mazishi 5 Januari 2023. 2023.01.02 Mwili wa Papa Benedetto umewekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro na watu wanaendelea kutoa heshima zao za mwisho hadi siku ya mazishi 5 Januari 2023.  (Vatican Media)

Jeneza la Papa Benedikto XVI limewekwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro

Tangu asubuhi, ya Jumatatu 2 Januari 2023,watu wengi wamekwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,kutoa heshima kwa Papa Mstaafu baada ya mwili wake kuondolewa katika Monasteri ya Mater Ecclesiae na kumweka katika Altare ya Maungamo.Kwa siku tatu atakuwa hapo hadi siku ya mazishi tarehe 5 Januari 2023.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatatu asubuhi  2 Januari 2023, watu wengi wameanza kwenda katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa Msaafu baada ya mwili wale kuondolewa katika Monasteri ya Mater Ecclesiae na kumweka katia Altare ya Maungamo. Wa kwanza kuingia, saa 8.50, Katika Kanisa kuu la  Vatican  ambalo lilikuwa bado  limefungwa kwa umma na lenye taa za chini, alikuwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, pamoja naye binti yake Laura ambali walisimama kwa muda kidogo upande wa kulia, wakiwa wameshikana mikono, ili kusali na kutoa heshima kwa Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI  ambaye mwili wake unaoneshwa kuanzia Jumatatu tarehe 2 hadi tarehe 4 Januari kwa ajili ya ibada ya waamini kwenye Altare ya Maungamo, sawasawa na kilichotokea wakati wa mazishi ya Papa Yohane Paulo II.

Ni wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa Papa Mstaafu
Ni wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa Papa Mstaafu

Mara baada ya Rais Mattarella, Waziri Mkuu, Giorgia Meloni, Alfredo Mantovano, katibu wa Waziri Mkuu na Waziri wa Kilimo Francesco Lollobrigida waliwasili pia. Ishara ya msalaba, kupiga magoti kwa muda mfupi, na pia katulia kwenye moja ya benchi nne za upande. Upande ule mwingine kulikuwa na Kadinali Michael Harvey, kuhani mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo  Nje ya Ukuta Roma, na watawa fulani waliokuwa na nia ya kusali Rozari kwa sauti ya chini. Kardinali Mauro Gambetti, Mismamizi  wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro aliwasalimia waliohudhuria.

Salamu na sala kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedikto XVI
Salamu na sala kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedikto XVI

Hata hivyo Kardinali Gambeti  asubuli mapema Jumatatu 2 aliongoza ibada hiyo iliyoanza saa 7.15 hadi 7.40, baada ya kuhamishwa kwa mwili wa Papa mstaafu kutoka Nyumba ya Mater Ecclesiae, monasteri iliyozungukwa na kijani katika bustani ya Vatican ambapo Papa Mstaa Joseph Ratzinger aliichagua kuwa makazi yake baada ya kung’atuka upapa mnamo  2013. Kutoka katika  kikanisa ambalo mwili wa Papa Benedikto  ulipumzika siku nzima ya tarehe Mosi ukioneeshwa karibu na msalaba mkubwa, eneo la pango na mti wa mapambo ya Noeli, Askofu  Gänswein, Memores Domini ambaye alikuwa ni msaidizi wa Ratzinger kila siku kwa miaka mingi, wasaidizi wa zamani wa Mater Ecclesiae walisali asala fupi, kabla ya mwili wa  Papa mstaafu kuhamishiwa katika Kanisa Kuu la Kipapa, pamoja na msafara. Katika safari fupi kando ya njia ya mikondo na miti ambayo siku nzima ya jtarehe mosi, kuanzia ziara za kwanza za kibinafsi za maaskofu na makadinali, ilichukuliwa na mamia ya watu ambao hawakutaka kusubiri ufunguzi wa Kanisa Kuu Jmatatu 2 Januari, walikwenda  kufanya ibada, salamu fupi na kutoa heshima za mwisho hivi mtiririko uliodumu hadi alasiri.

Ni wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa Papa mstaafu
Ni wakati wa kutoa salamu za mwisho kwa Papa mstaafu

Wengi walirudi tena kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro  Jumamatu 2 Januari 2022 wakisubiri kwenye foleni, wakiwa wamejifunika kwa mitandio na makoti kwa sababu ya baridi. Makadirio ya kwanza yanazungumza juu ya watu 15,000. Kati ya watu elfu 30 hadi 35 wanatarajiwa kwa siku katika siku tatu za onesho la jeneza kuanzia saa  2 asubuhi hadi tarehe 4 Januari jioni (kwa hiyo kuanzia saa 3 hadi saa 1 Jioni kila siku). Gavana wa Roma, Bruno Frattasi, alikuwa tayari ametarajia kwamba tarehe 5 Januari 5, siku ya mazishi inayoongozwa na Papa Francisko, mmiminiko wa takriban watu elfu 50-60 unatarajiwa!

Ni wakati wa Kutua salamu za Mwisho kwa Papa Mstaafu
Ni wakati wa Kutua salamu za Mwisho kwa Papa Mstaafu

Wakati huohuo, kikundi cha kwanza, kilipofungua mlango, kilitembea haraka haraka hadi kufikia hatua ya katikati ya Kanisa Kuu ambapo mwili umevalishwa  mavazi mekundu ya kiliturujia, mitra nyeupe, viatu vyeusi, bila pallium au msalaba wa kichungaji. Kati ya vidole vilivyounganishwa, kuna Rozari. Kuna wale ambao wanafanya ishara ya msalaba kwa  kupiga magoti yao, wale wanaojaribu kupiga hata picha kwa smartphone zao au kuacha tu na kuangalia. Watu wengi wanasimama kwenye vikanisa vya kandoni ili kusali  Rozari au kusubiri misa kwenye vikanisa vodogo.

02 January 2023, 16:57