Papa:kufanyia mazoezi roho ya kukutana ni msingi wa kuishi kisinodi katika kanisa
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Wajumbe wa Shirikisho la Mashirika yenye Kanuni za Mtakatifu Agostino, Baba wa Kanisa, tarehe 13 Januari 2023 mjini Vatican, ambapo katika hotuba yake Papa amewakaribisha kwa shangwe katika fursa ya Mkutano wao huku akimshukuru Abate kwa maneno yake vile vile hata wakuu wa mashirika hayo na Makatibu wao. Shirikisho lao liluundwa mnamo mwaka 1959 katika enzi ya Mtakatifu Yohane XIII. Muundo huo hata kama sio wa kisheria,Papa amebainisha kuwa ni muhimu kwa ajili ya kusaidia muungano wao kati ya Mashirika ya kiagostino na ambayo yanashirikishana karama au tasaufi yenyewe. Kwa dhati lengo kuu la shirikisho ni kuunganisha matawi tofauti ya Shirika lao katika muungano wa upendo, kuuthamanisha kwa kile ambacho kinatazama ukuu wa kiroho, malezi ya vijana, malezi kudumu na uhamasishaji wa utamaduni.
Hata ikiwa kila Shirika linafurahia kujitosheleza kwake, lakini hiyo haizui Sheria za Shirikisho ili kutoa uwezo unaopendelea usawa kati ya uhuru huo na uratibu unaofaa ambao unaepuka, kwa hali yoyote, uhuru na kutengwa. Kujitenga ni hatari Papa ameonya. Ni lazima kuwa makini ili kuondokana na ugonjwa huo wa kujisholeza na wakati huo kuhifadhi kweli tunu ya umoja kati ya Mashirika tofauti. Wao wanafahamu vema kuwa wanajikuta wote kuwa katika mtumbwi mmoja na kwamba hakuna anayeweza kujenga wakati ujao kwa kujibagua au kwa nguvu zake mwenyewe, lakini kwa kutambua ukweli wa kuwa na umoja ambao daima unajifungulia mkutano, majadiliano, usikivu na msaada wa pamoja (Barua kwa watawa wote 21 Novemba 2014,11,3). “Kufanyia mazoezi roho ya kukutana ndiyo msingi wa kuishi kisinodi katika Kanisa,”
Kama ilivyo kwa kila mtindo wa maisha ya wakfu, ambayo kama wao Papa amesema wanapaswa kuhusika katika muktadha hu ona katika maeneo waliyopo na katika utamaduni, daima kwa mwanga wa Injili na mwanga wa karama yao binafsi. Uwakfu wao ni kama maji, ikiwa hayatiririki, yanaharibika, yanapoteza maana, ni kama chumvi ambayo inapoteza ladha, na haifai kitu( Mt 5, 13). Kumbu kumbu njema na yenye kuzaa matunda, ni kama ile kumbu kumbu ya torati, ina mzizi, na ya asili. “Hatupaswi kuridhika na kumbukumbu ya akiolojia, kwa sababu hiyo inatubadilisha kuwa vipande vipande vya makumbusho, labda vinavyostahili kupendeza lakini si vya kuiga; badala yake Papa ameifananisha kumbukumbu ile ya Torati ambayo kwamba hutusaidia kuishi sasa kikamilifu na bila woga ili kujifungulia katika siku zijazo kwa matumaini mapya, amesisitiza Papa Francisko.
Hata wao kama alivyoandika Mtakatifu Yohane Paulo II kwamba: “Wana historia tukufu ya kukumbuka na kusimulia”, lakini zaidi ya yote wanayo “Historia nzuri ya kujenga!” kwa maana hiyo Watazame siku zijazo, ambamo Roho anawaelekeza kufanya mambo makuu katika wao” (Wosia wa Kitume wa Maisha ya wakfu, 25 Machi 1996,110). Kanuni msingi wa maisha ya kitawa ni kumfuasa Kristo kunako pendekezwa na Injili. Kuchukua wajibu wa Injili kama kanuni ya maisha hadi kufikia kusema na Mtakatifu Paulo kuwa: “Na sasa ninaishi lakini si mimi tena, bali Kristo anaishi ndani yangu”. Kwa maana hiyo Injili iwe kiongozi wao, kwa namna ya kuweza kuwa mbali na vishawishi vya kuipunguzia katika itikadi, na hiyo kwao ibaki daima kama Roho na maisha. Papa ameongeeza kusema “Injili kila wakati inatupelekea kumweka Kristo katikati ya maisha yetu na katika utume wetu. Inatupeleka katika upendo wa kwanza”. Na kupenda Kristo maana yake ni kupenda Kanisa na Mwili wake. Maisha ya wakfu, yanazaliwa katika Kanisa yanazaliwa na Kanisa na kutoa matunda kama Kanisa.
Ni katika Kanisa, kama anavyotufundisha Mtakatifu Agostino kuwa tunamgundua Kristo kamili. “Mungu alitumba kwa ajili yake, na roho zetu hazitatulia popote hadi zipumzike kwake”(Mtakatifu AGOSTINO, Maungamo, 1,1,1). Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu Francisko, amesema, Shirikisho la Mashirika ya Mtakatifu Agostino, shughuli yao ya kwanza na kila wakati kila siku ni kumtafuta Bwana. Kumtafua katika maisha ya jumuiya, kioo cha kuwa wa Mungu na kujikabidhi kwake na ushuhuda ambao Mungu ni upendo(1Yh 4,8.16). Koinonia iwafanye wote kujisikia wajenzi, wafumaji wa udugu. Watafute Bwana katika usomaji wa bidii wa Maandiko Matakatifu, ambayo Kristo na Kanisa vinasikika. (Hotuba ya Mt Agostino.46,33). Kumtafuta Bwana katika liturujia, kwa namna ya pekee katika Ekaristi hitimisho la maisha ya kikristo, ambayo ina maana na kutimiza umoja wa Kanisa katika maelewano ya upendo(Dei Verbum,25).
Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema a kuwa kumtafuta katika mazungumzo na katika uchungaji wa kawaida, kumtafuta hata katika hali halisi ya wakati wetu, kwa kutambua kuwa hakuna kile cha ubinadamu kinaweza kutozingatiwa na kwamba kuwa huru na kila aina ya malimwengu, tunaweza kuishi, ulimwengu na chachu ya Ufalme wa Mungu. Hizo ni njia tofauti mojawapo za kutafuta, ambazo zinapendekeza mchakato wa safari ya ndani, ya utambuzi na ya upendo wa Bwana, katika shule ya Mtakatifu Agostino: “Usitoke ndani yako, ingia ndani yako kila wakati; ukweli hukaa ndani yake mtu” (Agostino: Maungamo 3,6.11). Katika nuru hiyo ya Mwalimu wa ndani anaangazia sisi hali halisi ya kisasa. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amebainisha kwamba katika mkutano kati yao na Mfuasi wa Mtume Petro wa kutazama kwa upya karama na kuimarisha zaidi umoja wa maisha kwa mfano wa jumuiya zao za kwanza za kitume (Mdo 2,42-47). Na umoja juu pia ni utangulizi wa umoja kamili na wa mwisho wa Mungu na njia ya kuelekea kwake. Papa amewashukuru tena uwepo wao na ushuhuda wao katika Makanisa na kwenye Kanisa. Mama Maria awalinde na kuwaombea. Ameawabariki kwa moyo wote wao na jumuiya zao. Amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.