Papa Francisko:dini zinachangia utamaduni wa kukutana
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican tarehe 26 Januari 2023 na Wajumbe washauri wa Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu “Wanawake Kujenga Utamaduni wa Kukutana Kiiimani” ambapo amemshukuru Rais wa Umoja wa Mashirika ya Watawa wa kike katoliki duniani. Katika hotuba yake, Papa amewakaribisha kwa namna ya pekee watoa mada ya Mkutano huo uliongozwa na mada hiyo ya wanawake ambao wanajenga utamaduni wa kukutana kidini. Amewapongeza kwa kuanzisha mpango huo.
Papa amesema sio tukio la kawaida kwa waamini wa dini 12 duniani kote kuungana na kujadiliana kuhusu masuala msingi yanayohusu kukutana na kujadili kuhusiana na kuhamasisha amani na uelewa katika Ulimwengu wetu uliojeruhiwa. Na wakati mkutano wao umejikita katika kusikiliza uzoefu na matarajio ya wanawake, na kwamba una maana kubwa tena. Kiukweli amani inapaswa kutafutwa kwa kuhusishwa pakubwa wanawake. Kwa sababu wanawake wanatoa utunzaji na maisha ulimwenguni. Ni njia kuelekea amani” (Hotuba ya Papa huko astana 15 Septemba 2022).
Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa Kanisa Katoliki limejikita katika majadiliano ya kidini na katika kuhamasisha uelewa na ushirikiano kati ya waamini wa tamaduni nyingi za kidini. Kila mmoja wa tamaduni hizi na kila mmoja wao binafsi ana utajiri wa kutoa ulimwenguni, kwa kueneza roho moja ya makaribisho, ya kutunza na ya udugu. Sehemu kubwa ya waliokuwa kwenye mkutano huo imehusika kugundua mantiki ya kike katika tamaduni zao za kidini na kuonesha zenyewe jinsi zinavyochangia utamaduni mmoja wa kukutana. Kiukweli kukaa na kusikiliza mwingine, tabia ya kukutana kibinadamu ni mfano wa tabia ya kukaribisha, ya kushinda kujipendelea na kumpokea mwingine, kwa kumpatia umakini, kutengeneza nafasi katika mzunguko binafsi. Papa ametoa onyo kuwa Shughuli za makutano na ufunguzi unaohitajika, unaanza kupotea na wakati uzoefu wake ni moja ya zawadi kubwa ambazo wanaweza kutoa katika familia zao, jumuiya za ona jamii.
Baba Mtakatifu Francisko amewatia moyo katika umuhimu huo wa kushirikiana na kushikirishana dhamiri ya uzoefu wa matendo. Hayo yanatoa nguvu na ubunifu ikiwa katika miktadha yao, inafanya kazi kwa ajili ya kutoa msaada kwa watu wengi wanaotafuta nafuu katika mateso na zaidi sana maana na mtindo katika maisha yao. Kutokana na hilo Papapa Francisko ameapongeza kwa juhudi zao na nguvu zao wanazozitoa katika kuhamasisha hadhi ya wanawake kwa namna ya pekee wasichana.