Papa Francisko,Chama cha Assifero:Thamanisheni ukaribu
Na Angella Rwezaula; -Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na chama cha Assifero, Alhamisi tarehe 26 Januari 2023 mjini Vatican ambapo ameanza kushukuru Rais wa chama hicho Bi Stefania Mchini kwa maneno yake na kuwakaribisha wanachama hao. Sababu kuu ya kukutana ni katika kuadhimishwa mwaka wa 20 tangu kuanzishwa kwa chama hicho ambapo katika kuelezea amepata kuelewa na kufahamu hali halisi yao. Amewapongeza kwa kazi yao waliyotimiza kwa miaka katika msukumo wa Kikristo, ambao umeunda shughuli yao. Kama alivyoeleza mwenyekiti wao, makundi yao ni idadi kubwa za mifuko binafsi, wanaojikita shughuli yao nchini Italia na Nchi za Nje katika miktadha mbali mbali kwa ajili ya kuhamasisha mtu na kwa ajili ya maendeleo ya mitindo ya kijamii na kiuchumi iliyo safi na mshikamano kwa kuweka mkakati wa uwezo na rasilimali. Kiukweli jambo la kwanza linaloshangaza ni matendo yao hasa utajiri wake na ukweli.
Wao ni mchanganyiko wa madhehebu mbali mbali ya kikristo na wanapeleka mbele urithi wa mzunguko wa shughuli, utaalam, na mtindo wa kazi kwa njia mbali mbali, katika mantiki tofauti. Kwa hiyo shughuli yao ni upendo kwa nyanja yote ambayo inahitaji ufunguzi wa akili na uwezo wa kushirikishana; kama ile sura ya Paulo, asemayo ‘kuwa mwili mmoja’ (1Kor 12, 1-13). Katika hilo Papa Francisko amependekeza thamani tatu muhimu ambazo wanaweza kujikita nazo kwa sababu nyingine tayari wanazo ambao ni kuhamasisha manufaa fungamani ya mtu, pili, kusikiliza jumuiya mahalia, tatu, ukaribu kwa walio wa mwisho. Akianza kufafanua awali amesema kwamba wasisahau kuhusu ukaribu ambao ni moja wapo ya sifa za Mungu: na hivyo ni ukaribu, huruma na upole. Mungu yuko hivyo katika ukaribu, mwenye huruma na mpole. Hizi ndiyo “mtazamo mitatu ya Mungu.
Baba Mtakatifu amesema kwamba Ukaribu huo unakuongoza kwenye huruma na upole. Zaidi ya yote, uendelezaji wa manufaa fungamani ya tu, ni katika vipimo vyake vya msingi ambavyo ni nyenzo, kiakili, maadili na kiroho. Kwa hakika, inastahiki kwamba usaidizi wa nyenzo unalenga kuwakomboa watu, kuwafanya wahusika wakuu wa ukuaji wao, katika ukuzaji wa ujuzi na vipaji vyao, katika ngazi ya mtu binafsi na ya jumuiya. Yote basi kulingana na kanuni nzuri za maadili, ili ukuaji wa uchumi ufanyike kwa mshikamano na haki. Unaweza kuongozwa na maneno ya Yesu aliyesema: “Mimi nimekuja ili wawe na uzima kisha wawe nao tele” ( Yoh 10:10 ).
Thamani ya pili: kusikiliza jumuiya mahalia. Papa amekumbuka alivyo ambuwa juu ya umakini huo ambao unapendekeza kama njia: kusikiliza hali halisi ya ndani. Ni muhimu sana, ili uingiliaji wao usipunguzwe katika usaidizi wa mara kwa mara, lakini kupanda mbegu kwa siku zijazo ambapo watu wanaishi, katika hali ambazo fursa inawaonesha (taz. Lk 13:18-21). Na unyenyekevu wa kusikiliza, unaoeleweka kwa njia hiyo, ni kipengele cha msingi cha kutenda kwa manufaa ya wote, hata zaidi wakati inawawezesha kuwa wasemaji wa mahitaji ya wanyonge katika taasisi za umma.
Thamani ya tatu ya ukaribu na walio wa mwisho. Baba Mtakatifu amesema Kuna msemo usemao: “mnyororo una nguvu tu kama pete yake dhaifu”. Kuwakaribiwa walio wa mwisho zaidi, kuinamia majeraha yao, kutunza mahitaji yao, ni kuweka misingi mizuri ya kujenga jumuiya zilizoungana na imara, kwa ajili ya dunia bora na kwa mustakabali wa amani. Ni Kristo mwenyewe ambaye anakuja kukutana nasi katika maskini, ili kutuonesha njia ya Ufalme wa Mbinguni, Yeye ambaye “alijifanya maskini ili atutajirisha kwa umaskini wake” (taz. 2Kor 8:9). Papa amerudia kuwakushukuru kufika kwao na zaidi ya yote kwa mema yote wanayofanya. Amewahimiza wasonge mbele kila wakati kwa shauku na busara. Amewakubariki kutoka ndani ya moyo wake. Na nakuomba tafadhali wamwombee.