Papa kwa vijana WYD:Vijana wana kiu ya kupokea uzoefu na upeo!
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa tarehe 20 Januari 2023, ametoa ujumbe wake kwa njia ya video kwa ajili ya vijana katika muktadha wa kukaribia Siku ya Vijana duniani itakayofanyikia huko Lisbon nchini Ureno kuanzaia tarehe 1 hadi 6 Agosti 2023. Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anasema: “Tunakaribia, hata kama bado miezi kadhaa, kufikia Siku ya Vijana Duniani (WYD). Lakini tayari vijana 400,000 wamekwisha jiandikisha. Nimeshangazwa na furaha ambayo watakuja vijana wengi hivyo, kwa sababu wanahitaji kushiriki. Mwingine anaweza kusema “ninakwenda kutalii”. Lakini vijana wanakuja kwa sababu, kiukweli, wana kiu ya ushiriki, ya kushirikishana, ya kusimuliana uzoefu na kupokea uzoefu kutoka kwa wengine. Wana kiu ya upeo”. Baba Mtakatifu Francisko akiwageukia vijana hao, bado amesisitiza kwamba: “Ninyi vijana ambao tayari lakini 400,000 mmejiandikisha, mna mkiu ya upeo”.
Angalieni upeo
Kwa kuongezea Papa amesema: “Katika mkutano huo, katika Siku hiyo jifunzeni kutazama daima upeo, kuangalia daima zaidi ya. Msijenge kuta mbele ya maisha yenu. Kuta zinakufunga, wakati upeo unakufanya ukue! Tazameni daima upeo, kwa macho, lakini zaidi ya yote kwa moyo! Fungueni moyo! Kwa ajili ya tamaduni nyingine, vijana wa kiume na kike wengine ambao wanakuja hata katika Siku hiyo.”
Jiandaeni kufungua upeo na moyo
Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu anawashukuru vijana na kuwaeleza tena kuwa: "Jiandaeni na hilo:kujifungulia upeo na moyo! Naasanteni kwa kujiandikisha tayari mapema zaidi kwa wingi. Ni matumaini kwamba hata wengine watafuata mfano wenu! Na Mungu awabariki na Mama awalinde. Mniombee hata mimi, kama ninavyo waombea ninyi. Na msisahau kwamba: hapana kujenga kuta, lakini ni ndiyo kufungulia upeo. Asante!