Tafuta

Papa Francisko mbele ya Picha ya Bikira Maria wa Salus Populi Romani. Papa Francisko mbele ya Picha ya Bikira Maria wa Salus Populi Romani.  (ANSA)

Papa asali mbele ya Picha ya Maria kwa ajili ya safari ya Afrika

Kama ilivyo kawaida yake,Baba Mtakatifu Francisko amekwenda katika Kanisa la Bikira Maria ili kukabidhi ziara yake ya kitume huko Congo (DR)na Sudan Kusini mbele ya Picha ya ‘Salus Populi Romani’.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Imekuwa sasa ibada ya karibu na ya kina, ambayo inafanyika kila mara wakati Baba Mtakatifu  uifanya anapojiandaa na tukio maalu ili kupanua nafasi za kazi yake ya kitume kwa siku zinazokuwa zikimsubiri, ambap kwa kukaa  kimya mbele ya Picha ya Mama Maria Afya wa Waroma katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu,  jijini Roma kabla na baada ya kurudi kutoka ziarani. Kwa hiyo ndilo tendo ambalo limelifanya tarehe 30 Januari 2023 mchana. Papa Francisko kwa mara ya 102 amerudi humo na kutulia katika sala mbele ya sanamu ya Bikira ‘Salus Populi Romani, katika Kanisa Kuu la Santa Maria Mkuu, ili “kusali na kumkabidhi kwa safari yake ijayo ya Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini kabla ya kurudi tena jijini Vatican, kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican.

Hatua mbili

Katika ziara yake ya kichungaji na kiekumene hasa hatua ya kusini mwa Sudan, itakayoanza tarehe 31 Januari 2021 asubuhi saa 2.10 wakati ndege ya Kipapa itakapoondoka kutoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Fiumicino hadi kutua baada ya takriban saa saba za safari ya ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.  Na baadaye, tarehe 3 Februari, saa 4.40, Papa Francisko  pamoja na wasaidizi wake na waandishi wa habari walioidhinishwa ndani ya ndege hiyo wataondoka kuelekea hatua ya pili ya safari, ambayo ni marudio yaliyosubiriwa kwa muda mrefu huko Sudan Kusini ambapo wanatarajiwa kufika karibia saa 9 alasiri baada ya masaa mawili, ambapo Italia itakuwa ni saa 8 kamili hivi.

Nchi mbili zinazoteseka

"Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inateseka, hasa mashariki mwa nchi, kutokana na mapigano ya silaha na unyonyaji” alisema hivyo , Papa Dominika tarehe 29 Januari wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana akiomba maombi kwa ajili ya safari yake. Na huko “Sudan Kusini, iliyosambaratishwa na vita vya miaka mingi, hawawezi kusubiri kukomesha ghasia za mara kwa mara ambazo zinalazimisha watu wengi kuishi bila makazi na katika hali ya shida kubwa” aliongeza Papa. Kwa nchi zote mbili, ujio wa Papa Francisko ka hakika huleta matumaini ya upatanisho mpya.

Sala ya Papa kabla ya ziara ya kitume
30 January 2023, 17:18