Tokeo la Bwana,Papa:Tumwabudu Mungu na sio miungu ya uongo!

Katika Misa ya maadhimisho ya Tokeo la Bwana(Epifania),Papa katika mahubiri yale anaoneesha mahali ambapo kama Mamajusi na hata sisi tunaweza kukutana na Bwana katika:aswali yetu yasiyotulia;hatari ya safari na mshangao wa kuabudu.Kwa hiyo:“Tumwabudu Mungu na sio miungu ya uwongo zinazotupotosha kwa mvuto wa ufahari na mamlaka.

Na Angella Rwezaula; - Vatican

Mnamo tarehe 6 Januari 2023, Mama Kanisa ameadhimisha Siku Kuu ya Onesho la Bwana au Epifania, ambalo ni tukio linalokumbusha wataalamu na wasomi wa nyota waliotoka Mashariki ya mbali kwenda kuulizia mfalme aliyezaliwa kulingana na walivyokuwa wamejifunza. Kwa hiyo katika Misa iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko akisaidiana na Kardinali Antonio Tagle, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican. Akianza mahubiri yake amesema: “Kama nyota inayochomoza(Hes 24,17), Yesu anakuja kuangaza watu wote na kutoa giza za ubinadamu. Kwa Mamajusi walioinua mtazamo wao mbinguni hata sisi tujiulize, “Yuko wapi aliyezaliwa?(Mt 2,2). Ni eneo gani ambalo sisi tunaweza kwenda kumwona na kukutana na Bwana wetu. Kutokana na uzoefu wa Mamajusi, tunaelewa kuwa eneo la kwanza ambamo Yeye anapenda kutafutwa ni katika wasiwasi wa maswali. Uvutiwaji wa wataalamu hawa kutoka Mashariki ya ambali, unatufundisha kuwa imani haizaliwi kutoka na ujuzi wetu au sababu za kinadharia, lakini ni zawadi ya Mungu. Neema yake inmatusaidia kufanya mazoezi ya kujipanua na kutoa nafasi ya maswali muhimu ya maisha, maswali ambayo yanafufanya kuondokana na majivuno ya kuwa kila kitu ni sawa na kujifungulia wazi kwa yale yaliyo nje yetu.

Misa ya Siku Kuu ya Tokeo la Bwana Epifania 6 Januari 2023
Misa ya Siku Kuu ya Tokeo la Bwana Epifania 6 Januari 2023

Kwa Mamajusi, mwanzoni walikuwa na wasi wasi huo kama  wa yule anayejiuliza. Wakazi wenye kuwa na shauku isiyo na mwisho na  waliokuwa wakichunguza anga na kuacha washangazwe na nuru kali ya nyota, wanawakilisha namna hiyo ya umakini wa aliye juu ambamo ni roho katika safari ya uzalendo na utafiti usio na kikomo katika moyo wetu. Kuhusiana na nyota, kwa dhati iliacha katika moyo wao binafsi swali hili: Yuko wapi aliyezaliwa? Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa mchakato wa safari ya imani huanza wakati na neema ya Mungu, inaachiwa nafasi ya  kutotulia na kutufanya tuwe kidete. Tunapoacha kujiuliza maswali, na ikiwa hatutosheki na mazoea yetu ya utulivu lakini tunajikita katika kuthubutu kwenye changamoto za kila siku: ikiwa tunaacha kuhifadhi nafasi moja au nyingine na tunaamua kukaa katika nafasi za starehe za maisha, matendo ya uhusiano na wengine, ya kugundua mshangao, wa yasiyotarajiwa,  mipango ya kupeleka mbele, na ndogo ya kutimiza, ya hofu za kukabilianana , ya mateso yanayochimba mwili.

Katika muda huu ndani ya moyo wetu, maswali yanayoibuka ni mengi sana, ambayo yanatufungua katika utafutaji wa Mungu: Je furaha yangu iko wapi? Maisha kamili ya kufuata yako wapi? Huko wapi upendo ule ambao hauishi, hauzimiki, na ambao hauvunjiki hata mbele ya ulegevu, kushindwa na kusalitiwa? Ni fursa ngapi zimejifichika nyuma ya migogoro yangu na mateso yangu? Kila siku hali ya hewa tunayopumua hutoa “vitulizo vya roho”, viboreshaji vya kutotulia kwetu na kuzima maswali haya yawepo: kuanzia utumiaji hovyo hadi kufikia ushawishi wa raha, kutoka katika mijadala ya kuvutia hadi miungu ya  uongo wa ustawi; kila kitu kinaonekana kutueleza: usifikiri sana, basi, furahiya maisha! Mara nyingi tunajaribu kuuweka moyo katika sehemu salama ya faraja, lakini kama Mamajusi wangefanya hivyo hawangekutana na Bwana kamwe. Mungu, kwa upande mwingine, hukaa katika maswali yetu yasiyotulia; ndani yake tunamtafuta kama vile usiku unavyotafuta alfajiri, Papa amefafanua. Akiendelea Papa amesema Yeye yuko katika ukimya ambao unatusumbua mbele ya kifo na mwisho wa kila Maisha makubwa: Yeye anahitaji haki na upendo ambao tulio nao ndani. Yeye ni Fumbo Takatifu ambalo linakuja kukutana na kile ambacho ni kinyume kabisa kumbu kumbu kamili na zilizomwilishwa na haki, mapatano na amani ( Card. C.M.Martini kukutana na Bwana mfufuka. Moyo wa Roho ya Mkristo 2012, 66).  

Misa ya siku kuu ya Tokeo la Bwana Epifania
Misa ya siku kuu ya Tokeo la Bwana Epifania

Kwa maana hiyo eneo la kwanza ni wasi wasi wa maswali. Usiogope kuingia katika hali hii ya kutotulia ya maswali: ni njia hasa zinazotupeleka kwa Yesu”, Papa ameelekeza. aidha  amebainisha kuwa “Eneo la pili " ambalo tunaweza kukutana na Bwana ni hatari ya safari. Maswali, hata yale ya kiroho, yanaweza kusababisha kufadhaika na ukiwa ikiwa hayatatuweka njiani, ikiwa hayaelekezi mwendo wetu wa ndani kuelekea uso wa Mungu na uzuri wa Neno lake. “Hija yao ya nje alisema Papa  Benedikto XVI kuwa ilikuwa kielelezo cha kuwa kwao ndani ya safari, ya hija ya ndani ya mioyo yao.”(Mahuburu ya Epifania 6,Januari 2013). Mamajusi kiukweli, hawakusimama kutazama mbinguni na kutafakari mwanga wa nyota, lakini walianza mchakato wa safari ya nguvu na hatari ambayo haikuwa inaashirika njia salama na ramani iliyowazi. Walitaka kugundua ni Mfalme gani wa wayahudi, na ni wapi amezaliwa ili waweze kumwona. Kwa maana hiyo waliomba Herode mfalme ambaye naye aliitishwa viongozi wa watu na waandishi waliokuwa wamesoma maandiko Matakatifu. Mamajusi wako katika safari, ambapo kwa sehemu kubwa ya maneno yanayolezwa matendo yao, ni maneno ya mwendo. Na ndivyo hivyo kwa ajili ya imani yetu, kwani bila mchakato wa safari endelevu na mazungumzo yanayoendelea na Bwana, bila kusikiliza Neno, bila kuvumilia haiwezekani kukua.

Inatosha kuona wazo kuhusu Mungu na baadhi ya sala ambazo zinazungusha dhamiri; inahitaji kujifanya mfuasi wa Yesu na Injili yake, kuzungumza na Yeye yote katika sala, kumtafuta katika hali za kila siku na katika uso wa ndugu. Tangu Ibrahimu ambaye alianza safari katika ardhi isiyojulikana hadi kwa mamajusi ambao walizunguka nyuma ya nyota, hivyo Imani ni safari,  hija, historia moja ya kuweza kuanza kwa upya mchakto  wa safari. Tukumbuke hili: imani haiwezi kukua ikiwa inabaki imesisimama; hatuwezi kupunguzia kwenye ibada binafsi au kuiwekea vizingiti katika kuta za makanisa, lakini inahitaji kuipeleka nje, kuiishi kila wakati katika mchakato wa safari kuelekea kwa Mungu na ndugu. Tujiulize: Je niko ninatembea kuelekea kwa Bwana wa maisha, kwa sababu awe Bwana wa maisha yangu? Yesu wewe ni nani kwangu? Unanituma kwenda wapi unaniomba nini katika maisha yangu? Ni chaguzi gani unanialika kufanya kwa wengine.

Misa ya siku kuu ya Epifania iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro 6 Januari.

Hatimaye baada ya kutotulia kwa maswali na hatari za kutembea, ndiyo eneo la tatu ambalo tunaweza kukutana na Bwana ni mshangao wa kuabudu. Baba Mtakatifu amefafanua kuwa mwisho wa safari ndefu na nguvu ya utafutaji, Mamajusi waliingia katika nyumba, “ waliona mtoto na Mama yake, walisujudu na kuabudu”. Huo ndio uamuzi stahiki wa kutotulia kwetu, wa maswali  yetu, michakato yetu ya kiroho na mazoezi ya imani ambayo lazima yatokee katika kuabudu Bwana. Hapo ndipo panapatikana kitovu hai kwa sababu yote yanazaliwa hapo; kwa sababu ni Bwana ambaye huamsha ndani yetu hisia, ya kutenda na kufanya kazi. Hakuna maana ya kujiinua sisi wenyewe kichungaji ikiwa hatutamweka Yesu katikati, tukimsujudia. Hapo tunajifunza kusimama mbele za Mungu sio sana kuuliza au kufanya jambo fulani, lakini kunyamaza kimya tu na kujiachia wenyewe kwa upendo wake, ili tuweze kuvutwa na kuzaliwa upya kwa huruma yake. Yote yanazaliwa na kuhitimishwa hapo, kwa sabahu mwisho wa kila kitu siyo kufikia matazamio binafasi na kupokea utukufa binafai, lakini ni kukutana na Mungu na kuacha kukumbatiwa na upendo wake, ambao unatupatia msingi wa  tumaini letu, ambalo linatukomboa na ubaya, ambao unatangulia upendo kwa wengine, ambao unatufanya kuwa watu wenye uwezo wa kujenga ulimwengu wa haki na udugu. Kama Mamajusi, tusujudu tujikabidhi kwa Mungu katika mshangao wa kuabudu.

Tuabudu Mungu na sio ubinafsi; tuabudu Mungu na sio miungu ya uongo inayotuadaa na kutuongoza katika hali ya  ufahari na madaraka; tuabudu Mungu ili tusipigie magoti mbele ya mambo yanayopita na mantiki za ulaghai lakini na utupu wa ubaya. Baba Mtakatifu ameomba tufungue mioyo yetu kwa kutokuwa na utulivu, tuombe ujasiri wa kwenda kwenye njia na kuishia katika kuabudu: tusiogope! Ni njia ya Mamajusi, ni njia ya Watakatifu wote wa historia: kupokea wasiwasi, kujikita katika safari na kuabudu. Kwa maana hiyo tusiruhusu kuzima kwa kutotulia maswali ndani mwetu; tusisitishe mchakato wa safari yetu kwa kukubali kutojali au kustarehe; na,tukikutana na Bwana, tujisalimishe kwa mshangao wa kuabudu. Kisha tutagundua kwamba nuru huangaza hata usiku wa giza zaidi: ni Yesu, ni nyota ya asubuhi yenye kung'aa, jua la haki, mng'ao wa huruma ya Mungu, ambaye anapenda kila mtu na watu wote duniani.

Tukaabudu Kitoto kichanga Yesu aliyezaliwa huko Bethlehemu
Tukaabudu Kitoto kichanga Yesu aliyezaliwa huko Bethlehemu

Na wakati wa sala za waamini katika lugha ya kiswahili, kifaransa, kijerumani, kichina na kiingereza kwamba: Mwanga wa Mataifa, usindikize safari ya Kanisa lako: Waamini wawe wasikivu kwa utendaji wa Roho Mtakatifu, Mashuhuda wa daima wa upendo wa Baba, na watangaze kwa watu wote Injili yako ya wokovu. 

Tuombe: sala wakati wa Misa ya siku kuu ya Epifania
Tuombe: sala wakati wa Misa ya siku kuu ya Epifania

Kuwaombea watafiti wa ukweli: Hekima ya Aliye Juu, jioneshe kwa wale wanaotafuta uso wako: wanawaeza kuchunguze uumbaji wako kwa akili,  na watambue uwepo wako katika historia ya wanadamu, na waone uso wako kwa wale wanaoishi katika upendo.

Kuwaombe wale wote wanaoteseka: Nyota Inayochomoza upashe, joto mioyo ya wale wanaoteseka: uwafariji na upendo wa kaka na dada, waponye, majeraha ya mwili na roho, na uwajalie matumaini ya mapambazuko mapya ya asubuhi. Tuwaombee watu wote wa dunia. Kiongozi watu, uwasaidie wajenzi wa amani: wasielemewe na nguvu za uovu, wapambane  kwa ujasiri dhidi ya ukosefu wa haki na udhalimu wote, wazae matufan ya udugu na mapatano.

Misa ya siku kuu ya Tokeo la Bwana 6 Januari 2023
Misa ya siku kuu ya Tokeo la Bwana 6 Januari 2023

Tujiombee wenyewe na jumuiya zetu. Taa katika hatua zetu, angazia njia zetu: Neno lako liwe uhakika wa njia zetu za Maisha na lawama katika ukosefu wa imani, ujasiri katika majaribu

Kwa kuhitimisha na sala ya Papa ambaye ameomba: “Ee Kristu, nyota ya asubuhi yenye kung’aa, umwilisho wa upendo usio na kikomo, wokovu unaombwa na unangojewa kila wakati, sikiliza sala yetu na uwaangazie watu wote, ili waje kwako, waking’aa na nuru yako. Wewe unayeishi na kutawala milele na milele”.

Mahuri ya Papa katika kanisa Kuu la Mtakatifu Petro 6 Januari 2023
06 January 2023, 12:02