2023.01.30 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Kijeshi la Malta. 2023.01.30 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Kijeshi la Malta.  (Vatican Media)

Papa na Shirika la Malta:ukaribu na wanaoteseka na kazi zilizopangwa vizuri

Baba Mtakatifu Francisko akikutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Kijeshi la Malata katika hotuba yake alisisitiza dhamira ya sasa ya kushuhudia Injili na kuwasaidia wagonjwa na maskini:“unapokaribia kwa huruma na upeole katika jina la Yesu unakuwa kama msamaria mwema.”

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Papa Francisko, Jumatatu tarehe 30 Januari 2023, amekutana  Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Kijeshi la Malta  ambapo mara baada ya kuwasalimia ametoa  shukurani kwa  Kardinali Silano Tomasi kwa maneno ya hotuba yake na kuwashukuru wote  kwa kazi yao yote wanayofanya pamoja na  wawakilishi wake aliowatuma Yeye  na kundi kazi lililowasindikiza kwa miaka hii ya mwisho. Katika maamuzi yao Papa amewapongeza kufungua nyumba ya malezi na kwa haraka wataweza kufika wengine. Kwa hiyo anasali kwa Mungu na kuwaalika wote wasali naye ili Mungu atume miito mingi katika shirika lao si kwa ajili  ya wale wanafunga nadhiri tu, lakini hata wengine wanaohudumia na watawa hao. Ili kuweza kuhudumia maisha mengi ya kazi zilizoanzisha ni lazima kusali kwa Bwana ili awatume wafanyazi wema kwa kuongeza miito kwa kila hali, kwa namna ya pekee ya kitawa kufafanua ukamilifu wa miito kijana. Vile vile katika Mkutano wao mkuu Papa amesema kuwa  walikabiliana  na tema ya malezi ya mwanzo na ya kudumu kwa wajumbe wa shirika  kwa kuelekeza baadhi ya maelekezo ambayo yanaweza kusaidia katika muktadha wa sasa. Kwa nanma ya pekee ni lazima kuwa na mafunzo yanayostahili kwao kama vile hasa watawa wa  shirika  hilo la kijeshi na udhati wa ahadi ya utiii. Wasidharau mafunzo hata kwa waoblati wao hivyo ni matumaini ya Papa  Francisko kuwa inaweza kuzaa msimamo wa miito kwa ajili ya ukuu wote katika huduma ya shirika.

Papa aidha amebainisha jinsi ambavyo katika mkutano huo wanajipyaisha mwamko wa jitihada zao kwa kutoa bure kile ambacho walipokea bure na kushuhudia kwamba kumfauta Yesu katika huduma kwa maskini na kwa wagonjwa ni njia ambayo inajaza furaha roho. Kiukweli wanajiruhusu kukutana na Bwana kila wakati kwenye uso wa ndugu mwenye kuhitaji, kwa kila wanaye mpa mkono kumkaribisha  na kila hali ambapo wanaishi kwa upya wazo la Mwenyeheri Gerard, Mwanzilishi wa shirika hilo ambaye alilianzisha  kutoa maisha yake kwa huduma ya “Maskini wa Bwana wetu”. Papa Francisko kwa njia hiyo amependa kujikita kwa ufupi juu ya maneno ambayo tanatoa sifa ya shirika lao. Awali Wenye enzi. Hii ina maana ya enzi ya kipekee kabisa, iliyochukuliwa kwa karne nyingi na kuthibitishwa na mapenzi ya Mapapa. Hiyo inawaruhusu kutenda kwa ukarimu na kujishughulisha na ishara za mshikamano kwa kujifanya ukaribu zaidi na wale wanaohitaji, chini ya sheria ya kidiplomasia kimataifa.

Neno jingine jeshi. Kwa ajili ya kulinda wanahitajika jeshi na katika mahali patakatifu, zadiya kuwa ya kikristo, shughuli ya Shirika hilo iliandika sura tukufu. Leo hii ishara ile inaacha nafasi kwa ajili ya majadiliano ya kidini. Na zaidi imani katika Kristo na ufuasi wake, vinahitaji juhudi katika ushuhuda wa Injili na katika mapambano dhidi ya kile ambacho kinakwenda kinyume nayo.

Makaribisho katika Hospitali: Shirika linachota asili kutoka katika huduma ya Mwenyeheri Gerard aliyekuwa anatoa kwa wanahija wa Yerusalemu, katika Hospitali ambayo inaitwa jina Mtakatifu Yohane Mbatizaji, ambaye baadaye akawa msimamizi wao. Katika mahali hapo, Mwenyeheri Gerard na mabruda wa kwanza walikuwa wakiwapokea wanahija, na wenye kuhitaji msaada , na wakatoa kwao hata huduma za kiafya walizokuwa wanahitaji. Hiyo bado inapatikana leo hii katika wingi wa shughuli zao za shirika. Kwa kutibu wagonjwa wao wanajua kutambua kuwa kila mmoja wao uso wa mteswa Kristo, mahali popote atokako, kitaifa na imani kidini. Kwa hiyo wanapofanya ukaribu kwa huruma na upole wao hizo ndizo njia tatu za Bwana: ukaribu, huruma na upole na wao  wanapokaribia kwa huruma na upole, wao  mwenyewe wanajitambulisha na Yesu, Mchungaji Mwema, na Msamaria Mwema.  Papa amehimiza wasisahau kwamba jambo hilo ili kazi  ziweze kuandaliwa  vyema na kuendeshwa vema lakini   hasa  zaidi lazima siweze  kuwa ishara ya upendo wa Kristo ambayo ni kama utaratibu wa kazi zote unazopaswa kuzifanya.

Papa Francisko amewaeleza walivyoandika sura ya kuhistoria muhimu kwa ajili ya Shirika lao la Kijeshi la Malta, na wanaweza kujivunia hilo. Amewashauri wabaki waamini kwa Kristo, Mwalimu na Bwana ili kwenda mbele kwa kupeleka katika ulimwengu wote, ujumbe wa uponyeshaji kwa walio wagonjwa na wa faraja kwa walio kwenye migogoro. Kwa hayo ndiyo watakayo ulizwa mbele ya Mungu, kuwa waaminifu mashuhuda, kwa jirani na walio karibu nasi, bila kugubikwa na mambo ya kiulimwengu lakini wenye shauku katika huduma na katika kushuhudia Mfufuka. Kwa moyo Papa Francisko amewabariki wao, familia zao, wanachama, wafanyakazi, watu wa kujitolea na watu ambao wanawahudumia na kazi zao zote zilizopandwa ulimwengu mzima na katika sehemu zote za pembeni mwa maisha. Amewaomba tafadhali wasali kwa ajili yao.

Hotuba ya Papa kwa Shirika la Kijeshi la Malta
30 January 2023, 15:44