Papa:Tugundue mwamko mpya,twende na mshangao kuona siri ya mwaka mpya

Katika siku ambayo Mama Kanisa anasheherekea Bikira Maria Mama wa Mungu na Siku ya Amani duniani,Janauri Mosi 202,Baba Mtakatifu ameomba kusali kwa Mama kwa ajili ya watoto ambao wanateseka na hawana nguvu tena ya kusali,kwa ajili ya kaka na dada walioshambuliwa na vita katika sehemu mbali mbali za dunia.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Mama wa Mungu! Ndiyo tamko la shangwe la Watu wa Mungu Watakatifu ambapo lilisikika katika njia za Efeso mnamo mwaka 431, wakati Mababa wa Mtaguso walimtangaza kuwa ni Maria Mama wa Mungu. Hili ni tendo muhimu kwa imani, hasa kwa habari nzuri sana kuwa Mungu anaye Mama na hivyo basi kuna mshikamano daima wa ubinadamu wetu, kama ilivyo kwa watoto na mama, hadi kufikia kwamba ubinadamu wetu ni ubinadamu wake.  Ni ukweli wa kushangaza, na wa kufariji, kiasi kwamba Mtaguso wa mwisho, ulioadhimishhwa mjini Vatìcan ulithibitisha kuwa: “kwa kutungwa mimba Mwana wa Mungu, waliunganishwa kwa namna fulani kila binadamu. Alifanya kazi kwa mikono ya mtu, alifikiria kwa akili ya mtu, alitenda kwa utashi wa mtu, alipenda na moyo wa mtu. Kwa kuzaliwa na Maria Bikira, Yeye alijifanya kweli kuwa mmoja kati yetu kwa kila kitu, isipokuwa bila dhambi( Gaudium et spes, 22).

Misa ya  Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu Mosi Januari 2023
Misa ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu Mosi Januari 2023

Kwa maana hiyo tazama ni kitu gani alifanya kwa kuzaliwa na Maria: alijionesha upendo wake wa dhati kwa ajili ya ubinadamu wetu, kwa kuukumbatia kweli na kwa utimilifu. Baba Mtakatifu amebainisha kwamba Mungu hatupendi kwa maneno, lakini kwa matendo; sio kutoka juu, kutoka mbali, lakini kwa karibui, kutoka ndani ya mwili wetu, kwa sababu katika Maria Neno lilifanyika mwili, kwa sababu katika kifua cha Yesu kiliendelee kundunda moyo wa nyama, ambao unadunda kwa kila mmoja! Mama wa Mungu! Katika sifa hii wengi wameweza kuandika vitabu vingi na mambo makubwa. Lakini maneno hayo hasa yaliingia katika moyo wa Watu watakatifu wa Mungu, katika sala inayojulikana sana na ya nyumbani, ambayo inatundikiza hatua za siku; kwa wakati mgumu sana na kwa matumaini makuu, hiyo  ni “salamu Maria”. Baaada ya sentesi kutoka Neno la Mungu, sehemu ya pili ya sala inafunguliwa na maneno ya:“ Mtakatifu Maria, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu”. Hii ni sala ambayo mara nyingi inasindikiza siku yetu na iliruhusu kumkaribia Mungu maisha yetu na historia yetu kwa njia ya maombezi ya Maria.

Misa ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu Mosi Januari 2023
Misa ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu Mosi Januari 2023

“Mama wa Mungu utuombee sisi wakosefu” imesaliwa kwa lugha mbali mbali, kwa kutumia rosari na wakati wa mahitaji, mbele ya picha takatifu au njiani, kwa kusali sala hii kwa  Mama wa Mungu daima anajibu, anasikiliza maombi yetu, anatubariki na Mwanae aliye kwenye mikono yake, anatuletea huruma ya Mungu aliyejifanya mtu. Anatupatia neno moja la tumaini. Na sisi mwanzoni mwa mwaka huu, tunahitaji matumaini kama ardhi na mvua. Mwaka ambao unafunguliwa katika umbu la Mama wa Mungu na wetu, tunaambiwa kuwa ufunguo wa tumaini ni Maria, na katika wimbo wa katikati wa tumaini ni maombi kwa Mama wa Mungu. Baba Mtakatifu ameomba kusali kwa Mama kwa namna ya pekee kwa watoto ambao wanateseka na hawana nguvu tena ya kusali, kwa ajili ya kaka na dada walioshambuliwa na vita katika sehemu mbali mbali za dunia; ambao kwa siku hizi za siku kuu wanaishi gizani na katika baridi, katika umaskini na katika woga, wamemezwa na ghasia na sintofahamu! Kwa ajili ya wale ambao hawana amani tuombe Maria, Mwanamke aliyemleta Mfalme wa amani duniani. (Is 9,5; Gal4,4). Kwake yeye Malkia wa amani baraka tunaliyoisikia katika somo itaonekana: Bwana akubariki, na kukulinda; Bwana akuangazie nuru za uso wake, na kukufadhili; Bwana akuinulie uso wake, na kukupa Amani.(Hes 6,26). Kwa njia ya mikono ya Mama, amani ya Mungu inataka kuingia katika nyumba zetu, katika mioyo yetu, na katika ulimwengu wetu.  Je ni jinsi gani ya kuipokea?  

Tuache tushauriwe na walio mstari wa mbele katika Injili ya siku, wa kwanza walioona Mama na mtoto walikuwa ni wachungaji wa Bethlehemu. Hawa walikuwa ni watu maskini na labda hata wachafu, usiku ule walikuwa wanafanya kazi. Ni hao hasa na sio wajuzi na wala sio  wenye nguvu, walimtambua wakiwa wa kwanza Mungu pamoja nasi, Mungu aliyekuja maskini na ambaye anapenda kukaa na maskini. Kwa upande wa wachungaji, Injili inasisitiza hasa ishara mbili rahisi, ambazo lakini daima ni nyepesi. Wachungaji walikwenda na walioona kwa hiyo “kwenda na kuona.” Akifafanua juu ya hilo Papa amesema awali ya yote kwenda. Andiko linasema kuwa wachungaji walikwenda kwa haraka (Lk 2,16). Hawakusimama. Ilikuwa ni usiku, walikuwa na zizi lao la kulinda na kwa hakika walikuwa wamechoka: wangeweza kusubiri hadi asubuhi, kusubiri kuchomoza kwa jua ili kwenda kutazama mtoto aliyelazwa kwenye malisho. Kinyume chake walikwenda kwa haraka, kwa sababu mbele ya mambo muhimu lazima kutenda kwa utayari, bila kusubiri; kwa sababu neema ya Roho Mtakatifu haina mwendo wa upole (Tafakari ya Mt Ambrosi). Na hivyo walikuta Masiha, aliyetarajiwa kwa karne nyingi na aliyetafutwa na wengi.

Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa ili kuweza kumpokea Mungu na amani yake, haiwezekani kusimama na kubaki kwa kusubiri kuwa mambo yataboreka. Ni lazima kuamka, kupokea fursa ya neema, kwenda na kuthubutu. Tukiwa mwanzoni kwa mwaka, badala ya kukaa na kufikiria na kutumaini kuwa mambo yataboreka, itakuwa vizuri kujiuliza: “ Je mimi mwaka huu ninataka kwenda wapi? Kuelekea kwa nani na kufanya yaliyo mema? Walio wengi katika Kanisa na katika jamii wanasubiri wema ambao ni wewe tu unaweza kutoa, yaani huduma yako. Na mbele ya uvivu unaotugandamiza, na sintofahamu, mbele ya hatari ya kujizuia kubaki mbele ya kioo na mikono katika Computer, kwa wachungaji leo hii wanatuchangamotisha kwenda kutenda yaliyo mema, kujikatalia ukawaida na starehe zetu ili kujifungulia mapya ya Mungu ambaye anapatikana katika unyenyekevu wa huduma na katika ujasiri wa kutunza. Kwa njia hiyo ndugu ni vema kuiga wachungaji hao na kwenda.

Injili inasema kwamba wachungaji walipofika, walikuta Maria na Yosefu na mtoto amelazwa katika malisho. Baadaye inabainisha kuwa baada ya kumuona, walipatwa na mshangao wa kuelezea wengine juu ya Yesu na kumtukuza na kumsifu Mungu kwa yote ambayo walikuwa wamesikia na kuona ( 17-18.20). Mabadiliko yalitokea baada ya kuona. Ni muhimu kuona, kukumbatia kwa mtazamo, kubaki kama wachungaji mbele ya Mtoto aliye kwenye mikono ya Mama. Bila kusema lolote, bila kuomba lolote na bila kufanya lolote. Kutazama kwa kimya, kuabudu, kukaribisha kwa macho ya huruma yanayofariji ya Mungu aliyejifanya mtu, ya Mama yake na Mama yetu. Mwanzo mwa mwaka huu kati ya mapya ambayo tungetaka kufanyia uzoefu na mambo mengi ambayo tunataka kufanya, tujaribu kujikita muda mwingi wa kutazama, yaani kufungua macho na kuwa makini kwa kujali zaidi mbele ya kile ambacho ni Mungu na wengine.

Misa ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu Mosi Januari 2023
Misa ya Siku Kuu ya Bikira Maria Mama wa Mungu Mosi Januari 2023

Ni mara ngapi kwa sababu ya haraka hatukuweza kupata hata dakika moja kukaa mbele ya Bwana na kusikiliza Neno lake, kusali, kuabudu na kusifu… Jambo hilo pia linatokea kwa wengine, kwa kuwa na haraka au kimbele mbele, hatuna muda wa kusikiliza mke, mme, kuzungumza na watoto, kuuliza wao jinsi gani wanaishi ndani, si tu jinsi gani masomo yanakwenda, na afya. Ni jinsi gani ilivyo nzuri ya kujiweka katika usikivu kwa wazee, bibi na babu, kuwatazama kwa kina maisha na kugundua mizizi. Papa ameomba ni vema kujiuliza ikiwa kweli tunao uwezo wa kutazama yule anayeishi karibu, katika majengo yetu, yule tunayekutana naye kila siku katika njia. Kwa maana hiyo ndugu wote tuige mfano wa wachungaji wa kujifunza kutazama! Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko amesema ni Kwenda na kuona. Leo hii Bwana amekuja katikati yetu na Mtakatifu Mama wa Mungu amemweka mbele ya macho yetu. Tugundue kwa upya mwamko wa kwenda na wa mshangao wa kuona siri ili kuufanya mwaka huu kuwa kweli mpya. Na kwa wote pamoja tutamke mara tatu: Mtakatifu Mama wa Mungu! Mtakatifu Mama wa Mungu! Mtakatifu Mama wa Mungu!

Mahubiri ya Papa Mosi Januari 2023
01 January 2023, 10:44