Tafuta

Papa amewaeleza Sermig kuwa katika kujenga amani inahitajika mkutano na majadiliano. Papa amewaeleza Sermig kuwa katika kujenga amani inahitajika mkutano na majadiliano.   (Vatican Media)

Papa:Vijana wa Sermig msichoke kujenga amani,udugu na tumaini

Papa Francisko akikutana na wajumbe wa Huduma ya Kimisionari ya vijana(Sermig)mjini Vatican na waliounganishwa mtandaoni ameeleza kuwa wanawakilisha udugu wa amani kwa sababu wanahusiana na eneo la kiwanda cha amani mahali ambapo Vijana wanaweza kufanya uzoefu wa udugu,majadiliano na makaribisho yanayohitajika leo hii ulimwenguni.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Papa Francisko, Jumamosi tarehe 7 Januari 2023, amekutana mjini Vatican na wajumbe wa Huduma ya Kisimisionari ya vijana ijulikanayo kwa jina la (SERMIG) na kumshukuru mwanzilishi wake Bwana Ernesto kwa salamu zake. Amewashukuru wote kufika kwaona pia  wajumbe wote ambao hawakuweza kufika lakini walifuatilia tukio moja kwa moja kupitia mtandaoni. Papa Francisko katika hotuba yake amewaeleza kwamba siku hiyo wana fursa ya kumshukuru Bwana kwa ajili Sermig ambayo ni kama mti mkubwa uliokua kuanzia na mbegu ndogo. Na ndivyo hali halisi ya Ufalme wa Mungu. Mbegu ndogo ya Bwana, aliyopondwa Torino mwanzoni mwa miaka ya sitini. Katika kipinidi cha mavuno, inatosha kufikiri Upapa wa Mtakatifu Yohane XXIII na Mtaguso wa II wa Vatican. Katika miaka ile, uzoefu mwingi wa Kanisa ulichanua  ule wa huduma na maisha ya kijumuiya kuanzia na Injili.

Papa amekutana na Harakati ya SERMIG mjini Vatican
Papa amekutana na Harakati ya SERMIG mjini Vatican

Papa amebainisha kuwa mahali ambapo kuliendelezwa neema kwa baadhi ya miito ambayo ilipokea majibu kwa ukarimu na waamini, uzoefu huo umekuwa miundo na kukua kwa kutafuta kuendana na ishara za nyakati. Kwa njia hiyo Sermig, Huduma, ya Kimisionari ya Vijana, ni moja ya uzoefu huo. Ilizaliwa huko Torino na kikundi cha vijana; lakini ni vizuri pia kusema, kutokana na kikundi cha vijana pamoja na Bwana Yesu. Zaidi ya hayo Yeye mwenyewe aliwambia wazi mitume wake kwamba: “ Bila mimi hamwezi kufanya lolote (Yh, 15,5)”. Kutokana na matunda inaonesha wazi kwamba Sermig haikuwa mwanaharakati tu, lakini iliacha nafasi yake kwa Bwana; ambaye anaaombwa, anaabudiwa, anajulikana katika wadogo na katika maskini, na kwake Yeye amekubaliwa kwa waliobaguliwa.

Mkutano wa Papa na SERMIG
Mkutano wa Papa na SERMIG

Katika historia ya   Sermig kuna harakati nyingi, ishara nyingi ambazo zinaweza kutambuliwa kwa ishara kubwa na ndogo za Injili iliyo hai. Lakini kati ya hizo kuna moja ambayo katika wakati huu wa kihistoria, muhimu zaidi. Hiyo ni ile ya kubadilisha Kiwanda cha  wanajeshi wa Torino kuwa Kiwanda cha amani. Tendo hilo Papa amesema “linajizungumza lenyewe. Ni ujumbe ambao kwa bahati mbaya ni janga la sasa”. Hata hapa lazima kuwa makini ili wasitoke katika njia. Kiwanda cha amani kama harakati nyingi zilizofanya na Sermig na kwa ujumla wa shughuli zote za jumuiya ya Kikristo ni ishara ya Injili ambayo sio tu kwa sababu ya idadi inayofafanua kazi. Haipaswi kuzingatia hilo. Kiwanda cha amani ni tunda la ishara ya ndoto ya Mungu ambaye tunaweza kusema ya nguvu ya Neno la Mungu.

Mkutano wa Papa na SERMIG
Mkutano wa Papa na SERMIG

Ile nguvu ambayo tunahisi tunaposikiliza unabii wa Isaya “Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe.” Tazama ndio ndoto ya Mungu ambayo Roho Mtakatifu anapeleka mbele katika historia kupitia watu wake waaminifu. Na ndivyo wao, kwa njia ya imani na mapenzi mema ya Ernesto na mke wake na kikundi cha kwanza cha Sermig ambacho kimekuwa ndoto ya vijana wengi. Ndoto ambayo iliinua mikono na miguu, ikahuisha mipango, mataifa na kutimiza uongofu kutoka kiwanda cha silaha hadi kuwa kiwanda cha amani. Je ni kitu gani kinatengenezwa katika kiwanda cha amani? Ni nini kinajengwa? Kwa kawaida ni ujenzi wa silaha ya amani ambayo ni makutano, majadiliano na kukaribisha. Ni namna gani  inaundwa? Kwa njia ya uzoefu; katika kiwanda cha amani vijana wanaweza kujifunza kwa dhati kukutana, kujadiliana na kukaribisha. Hii ndio njia, kwa sababu ulimwengu unabadilishwa katika kipimo ambacho sisi tunabadilika. Wakati mabwana wa vita wanalazimisha vijana wengi kupambana  na kaka na dada zao, kunahitajika eneo ambalo inawezekana kufanya uzoefu wa udugu. Na ndiyo tazama neno la udugu linakuwa muhimu. Kiukweli Sermig inaitwa “udugu wa tumaini”.

Papa amekutana na SERMIG
Papa amekutana na SERMIG

Papa hata hivyo amesema inawezekana kusema hata kinyume yaani ‘tumaini la udugu’. Ndoto ambayo inahuisha mioyo ya marafiki wa Sermig ni tumaini katika ulimwengu wa kidugu. Ni ndoto ambayo papa amesema alitaka kuzindua katika Kanisa na katika ulimwengu kupitia Waraka wa ‘Fratelli tutti’, yaani ‘Wote ni ndugu’ (Ft, 8). Papa amesema wao wanashirikishan tayari ndoto hiyo na zaidi wao ni sehemu, wanachangia kumwilisha, kuunga mkono, macho, miguu na hivyo kuipatia maisha. Kwa njia hiyo  ameshukuru Mungu na wao, kwa sababu katika kazi yao ni ile ambayo huwezi kuifanya bila Mungu. Kwa sababu vita vinaweza kufanyika bila Mungu lakini amani inapatikana kwa njia ya Mungu tu. Papa Francisko amewaomba wasichoke kamwe kujenga Kiwanda cha amani. Hata kama kazi yao inaweza kuonekana imehitimishwa, kiukweli maeneo ya ujenzi daima yamefunguliwa.

Mkutano wa Papa na  SERMIG
Mkutano wa Papa na SERMIG

Wao  wanajua vizuri kwani katika miaka ya hivi karibuni wametoa maisha katika kiwanda cha Tumaini huko Mtakatifu Paulo nchini Brazil, kiwanda cha Mkutano huko Madaba ncini Jordan, kiwanda cha matumaini na maelewano huko Pacetto Torino. Lakini hali zote hizo, amani, tumaini, mkutano, maelewano, yanajengwa kwa njia ya Roho Mtakatifu, na Roho ya Mungu. Ni yeye ambaye anaunda amani, tumaini, mkutano na maelewano. Na maeneo ya ujenzi yatasonga mbele ikiwa wale wanaofanya kazi hiyo  wanaruhusu Roho afanye kazi ndani yao.  Na labda mtaniuliza je ni nani asiye amini? na ni nani ambaye si Mkristo? Hili linaweza kuonekana kama tatizo kwetu, lakini kwa hakika si la Mungu. Yeye, Roho yake inazungumza kwa kila roho ya mtu anayejua kusikiliza. Kila mwanamke na mwanaume mwenye mapenzi mema anaweza kufanya kazi katika kiwanda cha amani, tumaini, makutano na maelewano.

Licha ya hayo inahitaji mtu ambaye ameguswa na kusimika mizizi ndani ya moyo Injili. Inahitajika jumuiya ya imani na ya sala ambayo inashikilia moto huo kwa wote. Moto ambao Yesu alikuja kuleta duniani na ambao tayari na daima unawaka (Lk 12,49). Hapa inonekana hata kwa maana ya jumuiya ya watu ambao wanakumbatia kwa dhati wito na utume wa udugu na wanapeleka mbele kwa msimamo. Kwa kuhitimisha Papa Francisko ameashukuru sana kwa mkutano hu ona hasa kwa ushuhuda wa ona kazi zao. Waendelee mbele na Mama Maria awalinde na kuwasindikiza.

Mkutano wa Papa na SERMIG
07 January 2023, 16:30