Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini katika hotuba yake amegusia umuhimu wa hija ya uekumene wa amani Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini katika hotuba yake amegusia umuhimu wa hija ya uekumene wa amani   (Vatican Media)

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Sudan ya Kusini: Hotuba ya Rais Salva Kiir Mayardit

Rais Salva Kiir Mayardit amegusia umuhimu wa hija ya uekumene wa amani utakaosaidia kupyaisha mchakato wa haki, amani na upatanisho wa Kitaifa kwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa Mwaka 2018. Licha ya matatizo na changamoto zilizopo, lakini wadau wakuu wa Mkataba huo wanaendelea kushikamana ili kuhakikisha kwamba, Mkataba huu unatekelezwa kwa vitendo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Rais Salva Kiir Mayardit katika hotuba yake amegusia umuhimu wa hija ya uekumene wa amani utakaosaidia kupyaisha mchakato wa haki, amani na upatanisho wa Kitaifa kwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa Mwaka 2018. Licha ya matatizo na changamoto zilizopo, lakini wadau wakuu wa Mkataba huo wanaendelea kushirikiana, kujadiliana na kushikamana ili kuhakikisha kwamba, Mkataba huu unatekelezwa kwa vitendo, kwa kujenga miundo mbinu itakayoweza kusikiliza sauti za wananchi wa Sudan ya Kusini. Baba Mtakatifu Francisko kuanzia tarehe 31 Januari 2023 hadi tarehe 5 Februari 2023 anafanya Hija ya Kitume nchini DRC na Sudan ya Kusini. Lengo ni kutangaza na kushuhudia Neno la Mungu, Injili ya matumaini kwa wale waliovunjika na kupondeka moyo; amani na majadiliano katika ukweli na uwazi, kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya watu wa Mungu katika nchi hizi mbili. Baba Mtakatifu Francisko katika hija ya 40 ya Kitume akiwa ameambatana na Askofu mkuu Justin Welby, Kiongozi mkuu wa Kanisa Anglikani na Mheshimiwa Dr Iain Greenshields Mkuu wa Kanisa la “Presbyterian” la Scotland kama kielelezo cha ushuhuda wa majadiliano ya kiekumene yanayofumbatwa katika huduma, maisha ya kiroho, damu na sala, kuanzia Ijumaa tarehe 3 Februari hadi tarehe 5 Februari 2023 wanatembelea Sudan ya Kusini. Huu ni shuhuda wa hija ya uekumene wa amani na watu wa Mungu nchini Sudan ya Kusini.

Wananchi wa Sudan ya Kusini wana kiu ya haki, amani na maridhiano
Wananchi wa Sudan ya Kusini wana kiu ya haki, amani na maridhiano

Hija hii inanogeshwa na kauli mbiu “Wote wawe na umoja” Yn 17:21, hiki ni kielelezo cha ushuhuda wa kiekumene, mshikamano na udugu wa kibinadamu, mwaliko na changamoto ya kujizatiti katika mchakato wa upatanisho na ujenzi wa umoja wa Kitaifa, ili hatimaye, mamilioni ya wakimbizi, wahamiaji na watu wasiokuwa na makazi maalum waweze kurejea tena katika maisha yao ya kawaida, huku wakishiriki katika ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini katika hotuba yake amegusia umuhimu wa hija ya uekumene wa amani utakaosaidia kupyaisha mchakato wa haki, amani na upatanisho wa Kitaifa kwa kutekeleza Mkataba wa Amani wa Mwaka 2018. Licha ya matatizo na changamoto zilizopo, lakini wadau wakuu wa Mkataba wa Amani wa mwaka 2018 “Revitalised Agreement on the Resolution of Conflict in South Sudan” (R-ARCSS) wanaendelea kushirikiana, kujadiliana na kushikamana ili kuhakikisha kwamba, Mkataba huu unatekelezwa kwa vitendo, kwa kujenga miundo mbinu itakayoweza kusikiliza sauti za wananchi wa Sudan ya Kusini. Mwezi Septemba 2022 Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Mkataba wa Amani ulisogezwa mbele kwa muda wa miaka miwili, ili kuhakikisha kwamba uchaguzi unafanyika kwa kuzingatia misingi ya ukweli, uwazi, haki na amani. Serikali ya Sudan ya Kusini tayari imefanikiwa kuunda Kikosi cha Ulinzi na Usalama cha Kitaifa, kwa lengo la kulinda na kudumisha amani. Kwa hakika uwepo wa Baba Mtakatifu Francisko na ujumbe wa viongozi wakuu wa Makanisa ni kikolezo cha hija ya uekumene wa amani nchini Sudan ya Kusini.

Rais Sudan ya Kusini

 

04 February 2023, 15:40