Huzuni wa Papa kwa wahanga wa mafuriko nchini Brazil
Na Angella Rwezaula; – Vatican.
Papa Francisko ameelezea machungu wake kwa wahanga wa mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo ya pwani ya Mkoa wa kusini mashariki mwa Mtakatifu Paulo nchini Brazil katika siku za hivi karibuni. Idadi ya waliofariki kutokana na mafuriko iliongezeka na kufikia 57, lakini bado kulikuwa na wengi waliopotea. Uharibifu ni mkubwa: kwani inakadiliwa kuwa zaidi ya watu 4,000 wamehamishwa na kujikuta hawana makazi.
Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo alirekodi kwa njia ya video fupi, Jumatano baada ya katekesi yake akikutana na wasimamizi wa baadhi ya Harakati na Jumuiya mpya. Baba Mfrancisko kwa njia ya Hans Stapel, mwanzilishi wa Fazenda da Esperança, alimwomba amfikishie ujumbe huo.
Ukaribu wa Papa
Papa aliwakumbuka waathirika, na wengi waliopotea na walioathiriwa na mvua hizo mbaya zilizo sababisha maporomoko ya ardhi na mafuriko: "Ninataka kuwaonesha ukaribu wangu na uhakika wa maombi yangu. Mungu awabariki sana na Yesu awasindikize na kuwafariji. Na Bikira awalinde". Yalikuwa ni maneno machache yaliyojaa upendo, huku yakiambatana na baraka, ambayo iliyowafikia kama bembelezo kwa wale wanaoteseka.
Operesheni ya waokoaji hao kwa kutumia vitengo maalumu vya mbwa, walifanya kazi ili kuwatafuta watu ambao walikuwa bado hawajapatikana. Takriban majeruhi kumi na watano walilazwa hospitalini, mmoja wao akiwa katika hali mbaya. Huduma ya hali ya hewa ya Brazil MetSul ilikuwa imetangaza kuwa mvua iliyonyesha eneo hilo imekuwa kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Brazil.