Misa ya Papa Francisko Sudan Kusini:Tuweke chumvi ya msamaha katika majeraha
Na Angella Rwezaula;- Vatican.
Kuwa chumvi ya dunia ambayo uongeza ladha na kuyeyuka ili kuonja Sudan Kusini ile ladha ya kdugu ya Injili na jumuiya angavu za Kikristo ambazo hutoa mwanga wa mema kwa kila mtu na kuonesha kuwa ni nzuri na inawezekana kuishi, shukrani, kuwa na matumaini, kujenga mustakabali uliopatanishwa wote pamoja. Haya ndiyo matashi ambayo Baba Mtakatifu Francisko aliwatakia Wakristo wa Sudan Kusini ambao walikuwapo katika mija, mjini Juba, katika mahubiri ya Ibada ya Misa Takatifu kwenye uwanja wa makumbusho ya “John Garang”, baba wa nchi hiyo aliyefariki kabla ya kuona uhuru wake, kwa hiyo kulikuwa na zaidi ya Waamini 100,000 katika maadhimisho hayo ambao waliendelea kumiminika kwenye uwanja mkubwa na eneo linalozunguka mnara kwa muda mrefu.
“Tunaweka chumvi ya msamaha, ambayo huwasha lakini huponya kwenye majeraha. Hivyo sisi wanafunzi wa Kristo, Papa Francisko alifafanua, “hatuwezi kujizuia, kwa sababu bila hicho kidogo, bila kidogo chetu, kila kitu kinapoteza ladha yake”. Na wacha tuanze na hii kidogo, kutoka kwa kile kisichoonekana kwenye vitabu vya historia lakini hubadilisha historia”.
Katika jina la Yesu, na Heri zake tuweke chini silaha za chuki na kisasi ili kukumbatia maombi na mapendo; wacha tushinde machukizo hayo ambayo, baada ya muda, yamekuwa sugu na yanayopingana na makabila na tamaduni; tujifunze kuweka chumvi ya msamaha kwenye majeraha, ambayo yanawasha lakini yanaponya. Kwa hivyo, “moyo ukitokwa na damu kwa ajili ya makosa yaliyopokelewa itusaidie kuacha mara moja tu kujibu uovu kwa uovu, na tutajisikia vizuri ndani”. Tupendane kwa unyofu na ukarimu, kama Mungu anavyotutendea, na tulinde wema tulivyo, tusikubali kuharibiwa na uovu!”
Katika misa hiyo alikuwapo wasindikizaji wake wa kiekuemene Askofu Mkuu Welby, Msimamizi wa Kanisa la Scotland, Ian Greenshields na hata Rais wa nchi Bwana Kiir. Katika sala za waamini zinazosomwa kwa lugha ya Kiarabu, Kidinka, Kibari, Kinuer na Kizande, msaada wa Mungu umeombwa katika dhamira yao ya kujenga jumuiya zenye amani na wakuu wa nchi kuwa wakarimu katika kukabiliana na changamoto za ukarimu, uaminifu na uwajibikaji. Mwishoni mwa maadhimisho hayo, Askofu Mkuu wa Juba, Stephen Ameyu Martin Mulla, alimshukuru Papa Francisko kwa kuchukua uamuzi wa ujasiri wa kutembelea Sudan Kusini ambayo inateseka kwa sababu ya matokeo ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Ziara ambayo ni ishara ya mshikamano kwao na inaonesha nia ya kurejesha utulivu nchini.
Hatimaye Baba Mtakatifu ameagwa rasimi na kuanza kuandoka kurudi Roma baada ya kuwabariki wote na hata Rais wa nchi Kiir ambate amemwesha ishara ya Msalaba katika paji lake la uso.