Papa Francisko:Kutangaza,upole na huruma kama wanakondoo

Katika Katekesi ya Papa Francisko kwenye mwendelezo wa shauku ya kuinjilisha amejikita na hotuba ya Kimisionari ya Yesu kwa mitume wake ambapo amefanya uchambuzi juu ya kutangaza"kunakozaliwa na kukutana na Bwana na lazima imhusishe mtu kabisa akili,moyo na mikono."

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Jumatano tarehe 15 Februari 2023 wakati wa katekesi yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, ambapo ameendelea mada yake kuhusu shauku ya uinjilishaji, na ari ya utume. Papa amesema kwamba “kwa sababu kueneza Injili hakusemi kuwa  “tazama, blablabla” na si zaidi; kuna shauku inayohusisha kila kitu: akili, moyo, mikono, kwenda ... kila kitu, mtu mzima anahusika katika kutangaza Injili, na kwa sababu hiyo tunazungumza juu ya shauku ya kueneza Injili. Mara baada ya kuona mfano wa Yesu na mwalimu wa tangazo tunaweza kujikita juu ya mitume wa kwanza. Injili inasema kuwa Yesu aliwachagua kumi na mbili ambao wanaitwa mitume, ili waweze kukaa na Yeye na awatume kuhubiri (Mk 4,3, 14).

Papa akiingia kwenye Ukumbi wa Paulo VI kufanya katekesi yake 15 Februari 2023
Papa akiingia kwenye Ukumbi wa Paulo VI kufanya katekesi yake 15 Februari 2023

Kuna mantiki moja ambayo Papa amefikiria inapingana: “anaiwata ili waweze kukaa na Yeye na pia kwa sababu waweze kwenda kuhubiri.  Baba Mtakatifu ameongeza kuwa hiyo inataka kama kuuleza kitu moja au kitu kingine, kukaa au kwenda. Kinyume chake sio hivyo: kwa upande wa Yesu hakuna kwenda bila kukaa ,na hakuna kukaa bila kwenda.  Siyo rahisi kuelewa hilo lakini ndiyo hivyo. Kwa njia hiyo Papa Francisko alipenda kufafanua maana yake ambayo Yesu anasema mambo hayo. Kwanza kabisa, hakuna kwenda bila kukaa: kabla ya kuwatuma mitume katika utume, Kristo katika Injili inasema  aliwaita kwake (Mt 10,1). Tangazo linazaliwa  na kukutana na Bwana; kila shughuli ya kikristo, hasa utume, unaanzia hapo. Kumshuhudia, kiukweli kumuangaza; lakini ikiwa hatupokei mwanga wake, tutazimika; ikiwa hatwendi kwake mara kwa mara tunajipeleka sisi wenyewe badala ya Yeye na itakuwa kila kitu bure.

Papa akiwasalimia mahujaji wakati wa katekesi yake
Papa akiwasalimia mahujaji wakati wa katekesi yake

Kwa hiyo, ni wale tu wanaokaa naye wanaweza kupeleka Injili ya Yesu. Hata hivyo, kwa usawa, hakuna kukaa bila kwenda. Kiukweli, kumfuata Kristo sio ukweli wa karibu: bila tangazo, bila huduma, bila utume, uhusiano naye hukui. Tunaona kwamba katika Injili Bwana anawatuma wanafunzi kabla ya kukamilisha maandalizi yao: muda mfupi baada ya kuwaita, tayari anawatuma! Hii ina maana kwamba uzoefu wa utume  ni  sehemu ya malezi. Hebu basi tukumbuke nyakati hizo mbili za msingi kwa kila mfuasi: kukaa na kuondoka. Baada ya kuwaita wanafunzi kwake na kabla ya kuwatuma, Kristo aliwahutubia hotuba, inayojulikana kama mazungumzo ya kimisionari". Inapatikana katika sura ya 10 ya Injili ya Mathayo na ni kama kanuni ya tangazo.

Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa katekesi ya 15 Februari 2023
Picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa katekesi ya 15 Februari 2023

Kutoka katika hotuba hiyo, ambayo Papa amependekeza waisome amependa kuifafanua katika vingele vitatu: ‘kwa nini kutangaza, nini cha kutangaza na jinsi ya kutangaza’. Akianza na kwa nini kutangaza; Baba Mtakatifu amesema Msukumo upo katika maneno matano ya Yesu, ambayo yatatusaidia kukumbuka: “Mmepokea bure, toeni bure” (Mk4, 8). Tangazo halianzii kutoka kwetu, bali kutoka kwa uzuri wa kile tulichopokea bure, bila sifa: kukutana na Yesu, kumjua, kugundua kwamba tunapendwa na kuokolewa. Ni zawadi kubwa sana ambayo hatuwezi kuiweka kwetu wenyewe, tunahisi haja ya kuieneza; lakini kwa mtindo ule ule, kwa bure. Kwa maneno mengine: tuna karama, kwa hiyo tumeitwa kujitoa wenyewe; ndani yetu kuna furaha ya kuwa watoto wa Mungu, lazima ishirikishwe na kaka na dada ambao bado hawajui! Hii ndio sababu ya tangazo.

Makundi mbali mbali waliudhuria katekesi ya Papa
Makundi mbali mbali waliudhuria katekesi ya Papa

Ni kwanini, basi, kutangaza? Baba Mtakatifu Francisko katika kipengele cha pili amesema Yesu alisema: “Hubirini kwamba ufalme wa mbinguni umekaribia” (Mk 4, 7). Hili ndilo linalopaswa kusemwa, kwanza kabisa na katika kila kitu: Mungu yuko karibu. Lakini, msisahau kamwe hilo: Mungu daima amekuwa karibu na watu, Yeye Mwenyewe alisema na watu. Akasema hivi: “Tazama, ni Mungu yupi aliye karibu na Mataifa kama mimi nilivyo karibu nanyi?”. Ukaribu ni moja ya mambo muhimu zaidi kuhusu Mungu, ni mambo matatu muhimu: ukaribu, upolea na huruma. Usisahau hilo. Mungu ni nani? Jirani, Mpole, Mwenye huruma Huu ndio ukweli wa Mungu. 

Ukaribu, upole na huruma ni tabia za mmisionari

Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba  "Sisi katika kuhubiri amesisitiza mara nyingi tunawaalika watu kufanya jambo fulani, ni sawa; lakini tusisahau kwamba ujumbe mkuu ni kwamba Yeye yuko karibu: ukaribu, upole na huruma. Kukaribisha upendo wa Mungu ni vigumu zaidi kwa sababu sikuzote tunataka kuwa katikati, tunataka kuwa wahusika wakuu, tuna mwelekeo zaidi wa kufanya kuliko kujiruhusu wenyewe kufinyangwa, na  kuzungumza zaidi kuliko kusikiliza. Lakini, ikiwa tunachofanya kitatangulia, bado tutakuwa wahusika wakuu, badala yake, tangazo lazima limpe Mungu ukuu: kumpa Mungu ukuu wake , kwanza na kuwapa wengine nafasi ya kumkaribisha, kutambua kwamba yuko karibu. Na mimi, ninakuwa  nyuma yao".

Je ni jinsi gani ya kutangaza Yesu?

Je ni jinsi gani ya kutangaza. Katika kipengele hiki cha tatu, Baba Mtakatifu amebainisha kuwa ni kile ambacho Yesu alikaa zaidi juu yake: jinsi ya kutangaza, ni njia gani, ni lugha gani ya kutangaza. Ni muhimu kwa sababu  kinatuambia kwamba njia, mtindo ni muhimu katika kushuhudia. Kushuhudia hakuhusishi tu akili na kusema kitu, na dhana: hapana. Inajumuisha kila kitu, akili, moyo, mikono, kila kitu, lugha tatu za mtu: lugha ya mawazo, lugha ya upendo na lugha ya kazi. Mtu hawezi kuinjilisha kwa akili tu au kwa moyo tu au kwa mikono tu. Kila kitu kinahusiana na kingine. Na, kwa mtindo, jambo la muhimu ni ushuhuda, jinsi Yesu anavyotaka. Yeye alisema hivi: “Mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu” (Mk 4, 16).

Papa akisalimiana na kundi la watawa waliudhuria katekesi
Papa akisalimiana na kundi la watawa waliudhuria katekesi

Yeye hatuombi kujua jinsi ya kukabiliana na mbwa mwitu, yaani, kuweza kubishana, kupigana na kujitetea: hapana. Tunafikiria hivi kwamba tunakuwa muhimu, tutakuwa wengi, wa kifahari na ulimwengu utatusikiliza na kutuheshimu na tutashinda mbwa mwitu, na kumbe  hapana, sio hivyo! Yeye alisema kwamba “ninawatuma kama kondoo, kama wana-kondoo, hilo ndilo jambo la maana. Ikiwa hutaki kuwa kondoo, Bwana hatakulinda na mbwa mwitu. Kwa hiyo panga uwezavyo. Lakini kama wewe ni kondoo, uwe na hakika kwamba Bwana atakulinda na mbwa-mwitu. Kuwa mnyenyekevu. Yeye anatuomba tuwe hivyo, tuwe wapole na kwa nia ya kutokuwa na hatia, kuwa tayari kujitolea; na ndiyo kwa hakika  inawakilisha mwana-kondoo yaani mpole  na kutokuwa na hatia, kujitolea, huruma.

Mchungaji anawatambua kondoo wake na kuwalinda dhidi ya mbwa mwitu

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea amesema kwamba Naye, Mchungaji, atawatambua wanakondoo wake na kuwalinda dhidi ya mbwamwitu. Badala yake, wanakondoo waliovaa mavazi ya mbwamwitu hufichuliwa na kuraluriwa. Baba wa Kanisa aliandika hivi: “Maadamu sisi ni wana-kondoo, tutashinda na, hata kama tumezungukwa na mbwamwitu wengi, tutaweza kuwashinda. Lakini ikiwa tutakuwa mbwamwitu, wajanja, kwa kujihisi vizuri, tutashindwa, kwa sababu tutanyimwa msaada wa mchungaji. Yeye halishi mbwamwitu, bali anawalisha wanakondoo”. Nikiwa ninataka kuwa wa Bwana, sina budi kumwacha awe mchungaji wangu na yeye si mchungaji wa mbwa mwitu, ni mchungaji wa wana-kondoo, mpole, mnyenyekevu, mpole kwa Bwana.

Baadhi ya waamini wakimpatia Papa zawadi zao wakati wa katekesi ya siku
Baadhi ya waamini wakimpatia Papa zawadi zao wakati wa katekesi ya siku

Bado katika jinsi gani ya kutangaza, Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa  inashangaza kwamba Yesu, badala ya kuagiza kile cha kupeleka katika utume, anasema kile ambacho hakipaswi kupeleka. Wakati fulani, mtu anaona mtume fulani, mtu fulani anayehama, Mkristo fulani anayesema kwamba yeye ni mtume na alitoa maisha yake kwa Bwana, na anabeba mizigo mingi: lakini hiyo si ya Bwana, Bwana anakuwezesha kutokuwa na mzigo kwani anasema  “Msichukue, msiwe na dhahabu, wala fedha, wala fedha katika mishipi, wala mkoba, wala kanzu mbili, wala viatu, wala fimbo.” (Mk 4, 9-10). Yaani msichukue chochote. Hiyo anasema kwamba tusiegemee juu ya uhakika wa mali, kwenda katika ulimwengu bila mambo ya kidunia. Hili ndilo la kusema: Ninakwenda ulimwenguni si kwa mtindo wa ulimwengu, si kwa maadili ya ulimwengu, si kwa ulimwengu ambapo Kanisa kuangukia katika ulimwengu ni mbaya zaidi ambayo inaweza kutokea.

Papa akimbusu mtoto mdogo wakati wa kusalimiana na waamini na mahujaji katika ukumbi wa Paulo VI
Papa akimbusu mtoto mdogo wakati wa kusalimiana na waamini na mahujaji katika ukumbi wa Paulo VI

Badala yake ni kwenda kwa urahisi. Hivi ndivyo inavyotangazwa: kumwonesha Yesu, zaidi ya kuzungumza juu ya Yesu. Na tunamwoneshaje Yesu? Pamoja na ushuhuda wetu. Na hatimaye, kwenda pamoja, katika jumuiya: Bwana huwatuma wanafunzi wote, lakini hakuna mtu anayeenda peke yake. Kanisa la kitume ni la kimisionari kabisa na katika utume linapata umoja wake. Kwa hiyo ni kwenda wapole na wema kama wanakondoo, wasio na mambo ya kidunia, na kwenda pamoja. Hapa ndipo penye ufunguo wa tangazo, huu ndio ufunguo wa mafanikio ya uinjilishaji. Hebu tuikaribishe mialiko hii kutoka kwa Yesu: maneno yake yawe marejeo yetu, Papa amehimiza na kuhitimisha katekesi yake.

Tafakari ya katekesi na wito wa Papa 15 Februari 2023
15 February 2023, 15:23