2023.02.13 UNIAMO ni shirikisho la Italia la magonjwa adimu ambao wamekutana na Papa Francisko. 2023.02.13 UNIAMO ni shirikisho la Italia la magonjwa adimu ambao wamekutana na Papa Francisko.   (Vatican Media)

Papa Francisko,magonjwa adimu:mapungufu yao ni mahubiri halisi

Baba Mtakatifu amekutana na uwakilishi wa “UNIAMO”,Shirikisho la Italia la Magonjwa Adimu.Hotuba yake ilikatishwa na watoto na wagonjwa wengine waliomwendea ili kumsalimia na kupokea Rozari,ambapo aliweka kando hotuba iliyoandaliwa.'Mapungufu na magonjwa yao ni wito wa kwenda mbele'.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na wawakilishi wa UNIAMO, ambalo ni Shirikisho la Italia la Magonjwa adimu. Ameanza kushukuru kwa maneno  ya hotuba ya Rais wa Shirikisho hilo na  kwa yote wanayofanya. Amekumbusha jinis ambavyo amekuwa na fursa ya kuwasalimia mara nyingi, baada ya Sala ya Malaika wa Bwana na katika tukio la Siku ya Magonjwa Adimu ambalo hufanyika kila tarehe 28 Februari. Kwa maana hiyo katika mkutano huo alisema wangeweza kujuana vema na kushirikishana matumaini na mateso yao. Kushirikana kama kauli mbiu yao inavyosema  kwamba inajumuisha neno ufunguo na msingi unaostahili kutafakariwa.

Papa akisalimiana na watoto na kuwabariki
Papa akisalimiana na watoto na kuwabariki

Baba Mtakatifu Francisko amesema, thamani ya shirika lao kwa hakika ni lile kushirikishana. Tangu mwanzo amesema  inakuwa lazima lakini baadaye inageuka uchaguzi. Wakati baba na mama wanagundua kuwa mtoto anaugonjwa adimu, wanahitaji kukutana na wazazi wengine ambao waliweza kuishi na wanaishi na uzoefu huo huo. Ni lazima. Na kwa kuwa ugonjwa huo ni nadra, inakuwa muhimu kurejea chama ambacho kinaunganisha pamoja watu wanaoshughulikia ugonjwa huo kila siku: wanajua dalili, matibabu, vituo vya matibabu na kadhalika. Mwanzoni hiyo ni njia ya lazima, njia ya kutoka katika uchungu wa kuwa peke yako na bila silaha dhidi ya  adui. Polepole, hata hivyo, njia ya kushirikisga inakuwa chaguo, inayoungwa mkono na sababu mbili.

Watoto walimwendea Papa kupokea zawadi ya Rosari
Watoto walimwendea Papa kupokea zawadi ya Rosari

Ya kwanza ni kutambua kwamba ni muhimu, inatusaidia, inatupa ufumbuzi, angalau ya muda mfupi, inatuwezesha kujielekeza kidogo katika ukungu wa hali hiyo. Na msukumo wa pili unatokana na furaha ya mahusiano ya kibinadamu, kutokana na uzuri ambao urafiki unatufanyia na watu ambao hata hatukuwajua hadi jana yake na ambao sasa wanatuambia uzoefu wao ili kutusaidia kubeba hali nzito sana. Hii ndiyo thamani kuu ya kwanza ambayo Baba Mtakatifu ameina ndani mwao, katika ukweli wao wa shirikisho.

Hata hivyo Baba Mtakatifu ilibidi akatishe hotuba yake kwa sababu, watoto na wagonjwa wengine, walikuja kumsalimia wakisubiri kupata zawadi ya rosari. Katika hotuba iliyokuwa imebaki ambayo amewakabidhi, Baba Mtakatifu anaendelea kuelezea kuwa baadaye kuna thamani nyingine, muhimu sawa lakini tofauti, katika ngazi ya kijamii na pia kisiasa. Ni uwezekano kwamba chama kama chao kina mchango madhubuti kwa manufaa ya wote. Katika kesi hiyo, kuboresha ubora wa huduma ya afya ya nchi, mkoa, na wilaya. Hakika, siasa nzuri pia inategemea mchango wa vyama, ambavyo, kwa masuala maalum, vina ujuzi muhimu na tahadhari kwa watu ambao wana hatari ya kupuuzwa.

Watoto walikatisha hotuba ya Papa akaweka umakini kwao na kuzungumzia wao
Watoto walikatisha hotuba ya Papa akaweka umakini kwao na kuzungumzia wao

Hapa kuna jambo la kuamua Papa amesisitiza kwamba  sio suala la kudai upendeleo kwa kikundi cha mtu mwenyewe, hii sio siasa nzuri; lakini ni suala la kupambana ili mtu asitengwe kwenye huduma ya afya, mtu asibaguliwe, asiwe na adhabu. Na hiyo kuanzia uzoefu kama wao ambao uko katika hatari kubwa ya kutengwa. Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu katika hotuba yake aliyokuwa aiandaa na kuwapatia wajisomee baadaye akiwendelea ametoa mfano: hali halisi kama yao inaweza kuweka shinikizo kwa wengi kushinda vizuizi vya kitaifa na kibiashara kushiriki matokeo ya utafiti wa kisayansi, ili kuweza kufikia malengo ambayo leo  hii yanaonekana kuwa mbali sana.

Kwa hakika, ni vigumu kujitolea kwa kila mtu wakati tayari ni vigumu kukabiliana na tatizo lao mwenyewe. Lakini hapo kuna nguvu ya chama na hata zaidi ya shirikisho: ya uwezo wa kutoa sauti kwa wengi ambao, peke yao, wasingweza kusikika, na hivyo kuwakilisha hitaji. Kwa maana hiyo, itakuwa muhimu kuhusisha na kusikiliza wawakilishi wa wagonjwa kutoka hatua za awali za michakato ya kufanya maamuzi. Hakika, vyama sio tu vinaomba lakini pia vinatoa. Kuhusiana na taasisi, katika ngazi mbalimbali, wao hawana hilo la kuomba tu, lakini pia kutoa: ujuzi, mawasiliano, na juu ya watu wote, watu ambao wanaweza kuunga mkono kwa ajili ya manefaa ya kawaida ya pamoja, ikiwa wanafanya kazi kwa roho ya huduma na kiraia. Amehitimisha kwa kuwakabidhi kwa Mama maria huku akiwatia moyo waendele mbele na kuwashukuru kwa jitihada zao.

Papa na shirikisho la UNIAMO la italia la magonjwa Adimu
13 February 2023, 16:36