Papa Francisko:Upendo kwa Maria,Sala kwa ajili ya wafu&umakini kwa maskini!
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili, Ijumaa tarehe 17 Februari 2023, akianza kushukuru kwa maneno ya Mkuu wa Shirika na kuwasalimia wote. Wanaadhimisha Mkutano huo mkuu wakiwa katika muktadha wa kuadhimisha miaka 350 ya kuanzshiwa kwa Taasisi yao, iliyoanzishwa huko Krakow mnamo Desemba 1670 kwa njia ya Mtakatifu Stanislaus wa Yesu na Maria. Papa amebainisha jinsi ambavyo wanaelewa kuwa mwanzo haukuwa rahisi, iwe kwa kutafuta wenzake wanaostahili, na iwe kwa kukaa muda mrefu kabla ya kukubaliwa, lakini Mtakatifu Stanislaus, hakukata tamaa alikabidhi yote katika nguvu ya Roho Mtakatifu.
Na ndiyo maana ili kufanya tunu ya urithi kwa shauku yake aliyowaachia imemfanya Papa awakumbushe mambo matatu yake ya kufuata na tasaufi yao, ambayo imejikita katika mwendo wa shauku ya kusali kwa kina na kichungaji, hivyo ni: upendo kwa Bikira Maria, kuombea wafu; na umakini kwa maskini. Baba Mtakatifu Francisko akifafanua ya kwanza kuhusu Upendo kwa Maria, amesema inashangaza kuona kile ambacho Mtakatifu Stanslaus alifundisha kuhusu ibada ya Maria. Yeye alisema kwamba msingi wa ibada ya Moyo Safi wa Maria ni kuiga maisha ya kiinjili. Hii ni muhimu, kwa sababu ibada ya kweli kwa Mama wa Bwana inamwilishwa na kukua kwa usikivu na tafakari ya Neno la Mungu. Kwa hiyo Maria ni Mama wa Injili (Mt 12,46-50).
Mantiki ya pili ya Sala kwa ajili ya wafu ambayo ina tabia ya mwisho wa ulimwengu katika shirika lao. Mtakatifu Stanslaus lakini aliongeza mtazamo huo juu ya upeo wa mwisho wa sala kwa namna ya pekee kwa makundi mawili, makubwa ya maskini wa wakati wake ambao walikuwa ni wanajeshi,waliokufa katika vita na wafu wa janga la ugonjwa wa kuambukizwa. Papa ameongeza: je hao si sawa na leo hii, ni wanajeshi wangapi wako wanakufa kila sehemu. Tufikirie katika Karne ya 16 , kwamba karibia asilimia 60% ya watu wa Ulaya walihangamizwa na janga la ugonjwa wa kuambukizwa na vita! Kulikuwa na haja ya kusali wakati ule kwa ajili ya roho za marehemu, na kuwatia nguvu familia na jumuiya zilizokuwa na uchungu na maombolezo kwa ajili ya kupeteza wapendwa wao (Yh 11, 35-36).
Jambo la tatu ambalo Papa Francisko amependa kukazia ni umakini kwa maskini kwa namna ya pekee msaada wa maparoko. Watawa hao wa kiume wa Maria walikuwa wakichangia kujibu baadhi ya matatizo magumu ya wakati ule wa kudhoofika kwa imani, hasa kati ya tabaka la wanyonge, ukosefu wa miito ya kipadre na kitawa, hali ya umaskini wa sehemu kubwa ya watu (Mt 9,35-38). Mtakatifu Stanislaus alifuatilia mambo ya kiroho na matendo kwa ajili ya shirika lao ambalo limejumuishwa vyema katika historia thabiti ya wanaume na wanawake wa wakati wake. Ni muhimu kwao kuchukua kama kijiti kuendeleza kujibu kwa ubunifu changamoto ambazo zinakabili nyakati zetu, wasikate tamaa wakikutana na upinzani au matatizo! Wafikirie majaribu makubwa ambayo familia yao ya kitawa imekabiliana nayo kwa karne nyingi, kwa mfano ilipopungua miito na kubaki mshiriki mmoja tu mwanzoni mwa karne ya ishirini!
Kwa msaada wa Mungu lilipona, mpaka leo wanajikuta karibu na watawa mia tano ambao wapo katika nchi kumi na tisa ulimwenguni. Katika muktadha huo, tukumbuke sura ya Mwenyeheri George Matulaitis (1871-1927), Padre wa Maria, askofu na Balozi wa Vatican nchini Lithuania, mmoja wa wahusika wakuu wa kuzaliwa kwa shirika lao. Alijua jinsi ya kurejesha uhai kwa jumuiya kwa kuhuisha Katiba zake na kuendeleza kazi yake bila woga, hadi kufikia hatua ya kufanya mambo kwa siri na kuhatarisha kukamatwa, bila kukataa kamwe kuendeleza upendo na umoja kati ya watawa na waamini. Papa amewahimiza kuweka hai kwa uaminifu wa asili yao katika umakini huo wa kinabii hadi leo. Wamefanya hivyo katika siku za hivi karibuni kwa kuweka kati ya vipaumbele vyao vya kichungaji, uwazi kwa walei, ulinzi wa maisha tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo, umakini kwa wadogo na msaada kwa familia zilizo katika matatizo. Hii ni muhimu sana. Leo familia ziko hatarini. Hizi ni chaguzi ambazo zinaakisiwa, kwa mfano, katika kituo cha usaidizi cha Kiteknolojia na familia ambacho wameanzisha katika mahali patakatifu huko Licheń, nchini Poland; na katika maeneo mapya ya utume wa kimisionari ambayo wamefungua huko Asia na Afrika. Bwana awasaidie wasonge mbele katika njia hizo.
Papa amependa kuhitimisha mkutano huo kwa kuchukua sifa tatu za Maria ambazo Mtakatifu Yohane Paulo wa II aliwaalika watawa kuheshimu Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili. Bikira Maria Kikao cha Hekima, na ili ushuhuda wao wa Kiinjili uwe na msimamo na thabiti; Maria ni “Mfariji wa walioteswa”, ili watu wa wakati wetu wapate upendo na ufahamu ndani yao, na kuvutiwa kwa Mungu kwa upendo wao na utumishi wao usio na ubinafsi; na tatu: Maria ni “Mama wa Huruma”: ili wapate kuwa matajiri wa huruma ya kimama kwa ajili ya roho zilizo kombolewa kwa damu ya Kristo na kukabidhiwa kwao. Na kuhusu hilo, Papa amesisitiza kama kila wakati wa mikutano kama hiyo kwamba wasisahau mtindo wa Mungu wa ukaribu, huruma na upole. Mungu yuko hivyo: yuko karibu, ni mwenye huruma, ni mpole. Huyu ndiye Mungu wetu. Mtawa, na kuhani lazima awe karibu, awe na huruma, asamehe kila kitu, na awe mpole, asiye na fujo, upendo, mvumilivu kila siku. Na kutoka moyoni mwake Papa amewabariki wote waliokuwapo na washirika wao. Na wasisahau kumwombea hata Yeye.