Papa:Kuna haja ya kutoa ushuhuda ili kusaidia kujenga amani
Na Angella Rwezaula;-Vatican.
Majeraha ambayo yamesababisha michubuko ya kina katika wakati huu, kwa sababu ya vita vingi na uponyaji wake unawezekana kupitia kujitolea kuwa mafundi wa amani. Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko amefungua hotoba yake Jumamosi tarehe 25 Februari 2023, katika fursa ya uzinduzi wa mwaka wa 94 wa Mahakama ya Kitume. Mjini Vatican. Papa ambainisha kwa mara baada ya majaribu mabaya ya janga la ugonjwa wa Uviko na kuzuka kwa mzozo mpya nchini Ukraine na maendeleo yake ya kutisha, ulimwengu wote umegubikwa kwenye mzozo mkubwa, uliochochewa na milipuko mingi ya vita ambayo inaendelea kuzuka katika mataifa mengine mengi.
Kiukweli, kuna vita ambavyo wakati mwingine vinatugusa kwa ukaribu zaidi, lakini pia ni kwamba kuna migogoro mingi duniani na ni aina ya maangamizi binafsi (taz. Mkutano na waandishi wa habari kuhusu safari ya ndege ya kurudi kutoka Sudan Kusini, 5 Februari. 2023). Mbele ya kukabiliwa na hali hizi, hamu ya amani na haki ndani yetu inazidi kukua. Kuna haja ya kutoa ushuhuda ili kusaidia kujenga amani na haki ambayo inazidi kuimarishwa katika dhamiri zetu, hadi kufikia hatua ya kuwa ya lazima. Wakristo wanaitwa kupeleka ulimwenguni ujumbe ambao Yesu mara kadhaa alirudia kusema kwa wanafunzi wake kwamba: “Amani, amani kwenu”.
Akikumbusha maneno aliyotamka wakati wa Misa huko Kinshasa DRC mnamo tarehe Mosi Februari iliyopita, alisema kuwa “wanaitwa kufahamu amani ya ulimwengu”. Kila juhudi ya kujitolea kwa ajili ya amani kunamaanisha na kunahitaji kujitolea kwa ajili ya haki. Amani bila haki si amani ya kweli, haina misingi imara wala uwezekano wa siku zijazo. Na haki sio uzushi au utopia. Hapana. Katika Biblia, ni utimilifu wa uaminifu na uaminifu wa kila wajibu kwa Mungu ni kufanya mapenzi yake. Sio tu matokeo ya seti za sheria zinazopaswa kutumika kwa utaalam wa kiufundi, lakini ni fadhila ambayo tunampa kila mtu kile anachostahili, na umuhimu kwa utendakazi sahihi wa kila eneo la maisha ya kawaida na kwa kila mtu ili kuishi maisha ya amani.
Baba Mtakatifu akirejea mtazamo ambao shughuli za Mahakama ya kitume za Vatican unapaswa kuwa nayo, alikumbumsha kuwa migogoro ya kisheria na kesi zinazohusiana zimeongezeka. Kwa hiyo, katika matukio mengi, uzito wa mwenendo unaoangaziwa umeongezeka, hasa katika muktadha wa usimamizi wa mali na fedha. Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo amesisitiza kuwa: “hapa tunapaswa kuwa wazi na kuepuka hatari ya kuchanganya kidole na mwezi” kwani “tatizo sio mchakato wa taratibu, lakini ni ukweli na tabia ambazo huwaamua na kuwafanya kuwa uchungu wa lazima. Kwa hakika, tabia kama hizo kwa upande wa wajumbe wa Kanisa hudhuru sana ufanisi wake katika kuakisi nuru ya kimungu. Shukrani kwa Mungu, hata hivyo haikosekani, hamu kubwa ya nuru hiyo wala nia ya Kanisa kuikaribisha na kuishiriki, kwa sababu wanafunzi wa Kristo wameitwa kuwa 'nuru ya ulimwengu” (Mt 5, 14).
Kwa hiyo “hii ndiyo njia ambayo Kanisa linaonesha upendo wa wokovu wa Kristo ambaye ni Nuru ya ulimwengu (Yn 8:12).” Baba Mtakatifu akiendelea amesititiza kuwa: “Kanisa, linatimiza wajibu wake zaidi ya yote linaposhuhudia huruma. Upendo mkuu namna hii, huruma ya Mungu, ambayo daima inatutegemeza, hutuinua, na hutuongoza. Kwa mtazamo huo wa huruma na ukaribu tunaitwa kuwatazama ndugu zetu, hasa wanapokuwa katika shida, wanapofanya makosa, wanapopatwa na mtihani wa hukumu. Mtihani ambao wakati mwingine ni muhimu linapokuja suala la kuhakiki wa mwenendo unaoficha sura ya Kanisa na kusababisha kashfa katika jumuiya ya waamini”.
Kwa maana hiyo, Baba Mtakatifu amebanisha “zoezi la utambuzi mkali ni la manufaa, ambalo huzuia maendeleo ya maadili baridi katika kukabiliana na masuala ya mang’amuzi stahiki zaidi; pamoja na kukimbilia kwa busara kwenye kanuni ya usawa, ambayo inaweza kupendelea utafutaji wa usawa muhimu kati ya haki na huruma.” Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa “Huruma na haki sio mbadala bali hutembea pamoja, kwa usawa kuelekea mwisho huo huo, kwa sababu huruma sio kusimamishwa kwa haki, lakini ni utimilifu wake. Njia ya haki inawezesha udugu ambamo wote wanalindwa hasa walio dhaifu.”
Katika hotuba yake wakati wa salamu kwa Papa, mhamasishaji wa haki Bwana Alessandro Diddi alikumbusha kwamba Ofisi anayowakilisha inaitwa kufanya kazi kwa unyoofu na usiri, ili kuepuka ushawishi unaotokana na chuki na ushawishi wa vyombo vya habari. Shughuli nyingine, zisizo dhaifu zaidi kuliko zile ambazo tayari zimeshughulikiwa, zinaonekana kwenye upeo. Kwa hiyo umakini unaoongezeka ambao maoni ya umma huhifadhi kwa ajili ya shughuli zao na maoni ambayo wengi hueleza juu ya kazi yao kila siku, ambayo inawafanya wafahamu wajibu mkubwa ambao wamekabidhiwa na hitaji la kutimiza wajibu wao kwa uangalifu na kwa usahihi, lakini zaidi ya yote ni kwa heshima kubwa katika maadili yaliyo chini ya dhamana ya mchakato unaotazamiwa. Kwa maana hiyo wawakilishi kadhaa wa vyombo vya juu zaidi vya mahakama ya serikali ya Italia pia walishiriki katika mkutano huo.