Papa kwa wanasheria wa Kanisa:Watu wawe katikati ya shughuli kabla ya sheria!
Na Angella Rwezaula;-Vatican.
Katika hotuba ya Baba Francisko kwa washiriki wa Kozi ya huduma ya Kisheria iliyoandaliwa na Mahakama ya Kipapa ya Rota Romana kwa ajili ya waendeshaji wa sheria za kanoni na huduma za kichungaji za familia, aliokutana nao mjini Vatican, Jumamosi tarehe 18 Februari 2023, ameanza na ufunguzi kwa swali kwamba Je, kozi ya sheria inahusiana vipi na uinjilishaji? Kwa hiyo katika hotuba hiyo Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa kwa uhalisia hatupaswi kufikiria sheria ya kanoni na utume wa kueneza Habari Njema ya Kristo kama mambo mawili tofauti. Mtu anaweza kusema kimkakati: si sheria bila uinjilishaji, au uinjilishaji bila sheria. Kwa hakika, kiini cha sheria ya kanoni inahusu wema wa Kumunio, zaidi ya Neno la Mungu na sakramenti zote.
Kila mtu na kila jumuiya ana haki ya kukutana na Kristo na kanuni zote na vitendo vya kisheria vinaelekea kupendelea uhalisi na matunda ya haki hiyo, yaani, ya kukutana huko. Kwa hiyo sheria kuu ni wokovu wa roho, kama inavyothibitishwa na kanuni ya mwisho ya Kanoni ya Sheria ya kifungu cha (1752). Sheria ya kikanisa kwa hiyo inaonekana kuwa na uhusiano wa karibu na maisha ya Kanisa, kama mojawapo ya vipengele vyake vya lazima, ile ya haki katika kuhifadhi na kusambaza wema unaookoa. Uinjilishaji kwa njia hiyo ni dhamira ya kwanza ya kisheria, ya Wachungaji na ya waamini wote.
Ukweli wa haki daima lazima uangaze
Baba Mtakatifu Francisko, akinukuu maneno yaliyoandikwa na Papa Mstaafu Benedikto wa XVI mnamo mwaka 2010 katika barua kwa wanasemina, alikumbusha kwamba “jamii bila haki itakuwa jamii isiyo na haki”. Na kwa waendeshaji wa sheria za kanoni amewaonesha upeo huo kwamba shughuli yao inahusika na kanuni, taratibu na vikwazo, lakini haipaswi kamwe kupoteza haki, na kuwaweka watu katikati ya kazi yao, ambao ni fundisho na lengo la sheria. Haki hizi si madai ya kiholela, bali ni wema wenye lengo, linalo lenga wokovu, kutambuliwa na kulindwa, bila kusahau heshima ya wema asili wa ndani ya jumuiya ya kikanisa. Kwa hiyo wao kama watendaji wa sheria, wana wajibu wa kipekee wa kufanya ukweli, lakini je ukweli gani? Baba Mtakatifu Francisko ameuliza swali, na jibu ni kwamba wa haki katika maisha ya Makanisa mahalia. Katika kazi hiyo ni mchango wa uinjilishaji.
Utume wa mwanasheria
Kujua na kuzingatia kwa uaminifu kanuni za kisheria pia inamaanisha kukumbuka kila wakati wema ambao huko hatarini. Hili ni jambo la lazima, Papa alisisitiza kuwa ili kutafsiri na kutumia kanuni hizo kwa haki ni kwamba dhamira mwanasheria sio matumizi chanya ya kanuni kutafuta suluhishi zinazofaa kwa matatizo ya kisheria au kutafuta mizani au mambo ya aina hiyo, hapana. Kueleweka kwa njia hiyo, hatua yake ingekuwa ya manufaa yoyote, au angejaribu kunasa maisha katika mipango migumu ya kirasmi na ya ukiritimba ambayo inapuuza haki halisi. Kwa maana hiyp Papa ameeleza kuwa wasisahau daima kanuni iliyo kuu ya uinjilishaji kwa sababu ukweli ni bora kuliko wazo, halisi ya maisha ni bora kuliko rasmi. Kila mara ukweli ni bora kuliko wazo lolote, na ukweli huu lazima usaidiwe na sheria. Ukuu wa shughuli yao unaibuka kutoka na maono ambayo kanuni za kisheria, bila kusahau usawa wa kesi ya mtu binafsi, zinazotekelezwa kupitia fadhila za busara za kisheria ambazo hutambua haki halisi.
Njia ya hekima ya mahakama
Baba Mtakatifu Francisko akizungumza bila kusoma hotuba, alieleza kwamba njia ya hekima ya kimahakama lazima iendelee kulingana na mwongozo ambao unaruhusu kutoka katika ulimwengu wote hadi kufikia ulimwengu kamili na kwa uthabiti: Hukumu au msaada wa mahakama haufanywi kwa usawa bali unafanywa kwenye njia hii ya hekima. Inachukua sayansi, inachukua uwezo wa kusikiliza, juu ya yote inajikita katika maombi na kuhukumu vizuri. Kwa njia hiyo si mahitaji ya pamoja ya manufaa ya wote yaliyomo katika sheria wala taratibu zinazostahili za matendo zinazopuuzwa, bali kila kitu kinaangukia ndani ya huduma ya kweli ya haki.
Roho ya sinodi lazima iwe hai katika kila shughuli ya kisheria
Akikumbuka hotuba iliyotolewa mnamo mwaka wa 2022 wakati wa uzinduzi wa mwaka wa Mahakama ya Kitume ya Rota Romana, baba Mtakatifu alisisitiza kwamba sinodi ni kiini na inafungamana na mchakato wa ubatilisho wa ndoa: Uzingatiaji huo pia unatumika kwa wale wote wanaoshiriki katika utaratibu wa kutoa ruhusa ya ubatilisho wa ndoa iliyoidhinishwa na ambayo haijakamilika. Na roho ya sinodi lazima iishi katika kazi zao zote za kisheria. Kutembea pamoja, kusikilizana na kumwomba Roho Mtakatifu, ndiyo sharti la lazima kwa wanasheria katoliki kwa ajili uendeshaji sahihi wa sheria. Udhihirisho halisi wa hilo ni hitaji la kuomba ushauri, kukimbilia maoni ya wale ambao wana ujuzi zaidi na uzoefu, na shauku hiyo ya unyenyekevu na ya kudumu kujifunza daima ili kutumikia vyema Kanisa katika muktadha huo.
Huduma ya kichungaji ya familia na mahakama za kikanisa
Baba Mtakatifu akiendelea na hotuba yake aidha amewageukia wachungaji wa familia. Na kusema kuwa anakumbuka kwamba ufahamu wa mwingiliano kati ya huduma ya kichungaji ya familia na mahakama za kikanisa umeongezeka zaidi ya miaka hii: Kwa upande mmoja, huduma muhimu ya kichungaji ya familia haiwezi kupuuza maswali ya kisheria kuhusu ndoa. Inatosha kufikiria, kwa mfano, juu ya kazi ya kuzuia ubatili wa ndoa wakati wa awamu inayotangulia harusi, na pia kusindikiza wanandoa katika hali ya shida, pamoja na mwelekeo kuelekea mahakama za Kanisa wakati uwepo wa mkuu wa ubatili, au ushauri kuanza utaratibu wa utoaji kwa yale yasiyo ya matumizi.
Kwa upande mwingine, waendeshaji wa mahakama hawawezi kamwe kusahau kwamba wanashughulikia masuala ambayo yana umuhimu mkubwa wa kichungaji, ambayo mahitaji ya ukweli, upatikanaji na kasi ya busara lazima daima kuongoza kazi yao; na wajibu wa kufanya kila liwezekanalo kwa ajili ya maridhiano kati ya wahusika au uthibitisho wa muungano wao pia haupaswi kupuuzwa. Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko amekumbuka maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II katika hotuba yake kwa Rota Romana ya mnamo tarehe 18 Januari 1990. Alseima kwamba: “haki ya kweli ndani ya Kanisa, inayohuishwa na upendo na kuchochewa na usawa, daima inastahili sifa stahikii ya huduma ya kichungaji”; kwa hiyo amewakabidhi kwa Mama Maria “Kioo cha Haki”, huduma ya kila siku ya waendeshaji wa sheria za kanoni na utunzaji wa kichungaji wa familia.