Papa na Muungano wa Vyama vya Biblia Kimataifa:Ulimwengu mara nyingi ni kiziwi kusikia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Alhamisi tarehe 16 Februari 2023 amekutana na ujumbe wa kiekumene wa Muungano wa Vyama vya vya Biblia Kimataifa ulioanzishwa mnamo mwaka 1946. Akianza hotuba yake amemshukuru kwanza Mheshimiwa Dirk Gevers, Katibu Mkuu wa wa Umoja huo ulimwenguni. Amewakaribisha wote na Kardinali Kurt Koch ambaye aliwasindikiza. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe nanyi. “Upendo wangu uwe pamoja nanyi katika Kristo” (1Kor 16,24) ameongeza kusema Papa. Katika Kitabu cha Matendo ya Mitume kinaelezea kuenea kwa Neno la Mungu baada ya tukio la Pasaka. Baada ya Pentekoste, kwa nguvu na kwa ulinzi wa Roho Mtakatifu, mitume walienezea Kerygma, wakieleza maana ya Neno kwa mwanga wa fumbo la Yesu Kristo na kuweka umakini na wale ambao walikuwa wakitumia vibaya au kwa au kwa maslahi yao finyu.
Matukio ya Kanisa ambalo lilikuwa tu limezaliwa yanafanana na yale ya nyakati zetu. Neno linatangazwa, linasikilizwa na kuishi katika muktadha unaopendeza na usiopendeza, kwa njia tofauti na vielelezo tofauti, kwa kukabiliana na matatizo makubwa na mateso, katika ulimwengu ambao mara nyingi ni kiziwi kusikiliza sauti ya Mungu. Kanisa lililozaliwa linaishi. Kwa Neno, linatangaza, na kuteswa, linakimbia nalo kama mzigo wake wa kipekee. Kwa hiyo mateso yanageuka kuwa fursa ya kueneza Neno, na kamwe kulisahau. Muktadha huo ni kama wa Shemasi Filipo: Mateso yanamsukuma kwenda Samaria, na kufika hapo hazungumzi juu ya uchungu wake, lakini anahubiri Kristo na kuponesha wagonjwa na "kulikuwa na furaha kubwa katika mji huo” (Mdo 8,8).
Papa amefikiria wakristo ambao katika wakati wetu wanalazimika kukimbia nchi zao. Wanaume na wanawake ambao kama kwanza waamini, wanakimba wakiondoka na Neno walilo lipokea. Kuhifadhi imani yao kama ilivyo tunu ambayo inatoa maana katika muktadha huo mgumu, ambao wakati mwingine hauwesemeki na ambao lazima waweze kukabiliana nao, kwa kukumbatia msalaba wa Kristo kwa kuheshimu Neno la Mungu ambalo linadumu milele (Is 40,8:1Pet 1,23-25). Lakini hata kitabu cha Matendo ya Mitume kinatupatia onyo kwamba: Filipo, katika utume wake alikabiliana hata naukosefu wa uwezo wa kuelewa na kupokea Neno la Mungu na katika mazingira tofauti kabisa, wote wawili walipata Neno, lakini Simoni mgana wa kienyeji alijawa na nafsi yake kiasi kwamba alijizuia kupokea zawadi ya Mungu; Wakati huo huo Mwethiopia, kwa upande mwingine, alikuwa na kiu ya Mungu na sio tu kuelewa Neno kupitia huduma ya Filipo, lakini alimwomba apate Ubatizo, na alipokea, na kuendelea na safari yake kama Mkristo.
Baba Mtakatifu Francisko amesema, mbio za Neno la Mungu zinaendelea hata leo hii, na kwao katika shughuli yao, wanajikita juu ya huduma yao. Uenezaji wa Biblia kwa njia ya kuchapisha makala mbali mbali katika lugha tofauti na ugawaji wake katika mabara tofauti ni kazi ya kupongezwa. Takwimu zilizotangazwa zina maana, na Papa amefurahi kuelewa kuwa kazi Muungano wa Vyama vya Biblia wanayojikita nayo daima na zaidi katika ushikiano kwa wakatoliki wengi katika nchi Nyingi. Baba Mtakatifu ameomba Roho Mtakatifu aongoze na kusaidia daima katika kazi yao huduma. Kiukweli Yeye anaweza kuonesha wazi kwa kina Mungu, kwa namna ya kwamba wale wanaokaribia katika maandiko matakatifu yanafika kwa utiii wa imani (Rm16,26) kukutana na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo.