Papa:Vita vinaharibu wote na tupande mbegu ndani mwetu ya amani
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
“Kwa nini hatuwezi kuishi kwa amani? Ni rahisi hivyo…. Ni swali la kuhuzunisha katika hali hii, kwa sauti ya msisimko, ambapo msichana wa Kiukrene aliuliza Papa, Kanisa, ulimwengu katika filamu yenye kichwa “Uhuru motoni:Mapambano ya Uhuru wa Ukraine”. Kazi hiyo, iliyohamasishwa na mkurugenzi Evgeny Afineevsky, ilioneshwa alasiri tarehe 24 Februari 2023 katika Ukumbi wa Sinodi Mpya, jinini Vatican katika siku ya kumbukumbu ya kile ambacho Papa Francisko amekuwa akikifafanua kuwa vita vya “upuuzi”, yaani baada yam waka mzima wa vita nchini Ukraine ambavyo vinaendelea.
Papa mwenyewe, aliyeketi katika safu ya mwisho, alishiriki katika afla hiyo na alikutana na baadhi ya wahusika wakuu wa filamu hiyo mwishoni mwa maonesho hayo. Miongoni mwao alikuwa ni Bi Anya Zaitseva, mke wa askari aliyetekwa, huko Ukraine kwa upande wa kulia wa Papa akiwa na Sviatoslav mtoto mdogo, mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi minne mikononi mwake, ambaye alicheza na kunyonya fimbo ya Papa wakati akitazama filamu au kumpa mabembelezo.
Baba Mtakatifu Francisko pia alitaka kuwasalimu baadhi ya wageni takriban 240 ambao walikuwa ni watu wenye kuhitaji, wakimbizi na wanachama wa jumuiya ya Kiukrene ya Roma, walioalikwa na mkurugenzi huyo. Hao walikuwa pamoja na wawakilishi wa vyama mbali mbali vinavyotoa usaidizi na Kadinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Huduma ya Kipapa ya Upendo, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya vyombo vya habari vya Vatican.
Kwa maana hyo Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya filamu hiyo kuhusu Ukraine alikuwa na ya kusema kwamba: “Mungu alipoumba mwanadamu, alisema tuichukue dunia, tuifanye kukua na kuwa nzuri. Roho ya vita ni kinyume chake, cha kuharibu,na hivyo tusiruhusu, kuharibu kila mtu, wanaume, wanawake, watoto, wazee, kila mtu. Leo ni mwaka wa vita hivi. Tutazame Ukraine, tuiombee Ukraine na tufungue mioyo yetu kwa uchungu. Tusione aibu kuteseka na kulia, kwa sababu vita ni uharibifu, vita inatupunguza siku zote. Mungu atujalie kuelewa hili”.
Na kabla ya kuwabariki Papa aliongeza sala kwamba: “Baba Mtakatifu uliye mbinguni, tazama taabu zetu, tazama majeraha yetu, tazama maumivu yetu, pia tazama ubinafsi wetu, masilahi yetu duni na uwezo tulionao wa kujiangamiza wenyewe. Uponye mioyo yetu, ponya akili zetu, ponya macho ili waone uzuri ulioufanya na usiuharibu kwa ubinafsi. Panda mbegu ya amani ndani yetu”.
Kabla ya kurudi Nyumbani huko Mtakatifu Marta, Papa Francisko alikutana na mwanamke, mama wa mmoja wa askari waliozuiliwa katika kiwanda cha chuma cha Azovstal huko Mariupol, alitekwa na askari wa Urussi na kwa sasa bado ni mfungwa. Kwa msaada wa kuhani mkalimani, mwanamke huyo alimwambia Papa kuhusu kilo 40 ambazo mtoto wake amepoteza katika miezi ya hivi karibuni na alishirikisha maombi yao kwamba yeye na askari wengine ambao wanapambania kutetea uhuru wanaweza kuwa huru mapema iwezekanavyo. Hu mama limpatia Papa zawadi tatu: ua, ishara ya upinzani mpaka uhuru unapatikana; bendera ya njano na bluu ya Ukraine, ambayo Papa Francisko alibusu na kubariki; mfuko wa chumvi, ambayo ni zawadi ya kawaida kwa utamaduni wa Ukraine.
Wakati wa kumkabidhi alisema: “Ni chumvi ya dunia, na ni ishara ya nguvu: kile kinachohitajika katika vita kali sana, mbaya sana”. Papa pia alimsalimia mmiliki wa Azovstal, ambapo alipokea zawadi ya mfano kutoka kwake bangili iliyotengenezwa kwa chuma kutoka katika kinu cha chuma. Papa Fransisko alivaa kwenye mkono wake, kisha kama kawaida aliomba kwa ajili yake mwenyewe, akimwakikishia mamombi hayo kwa ajili ya watu waliouawa.