Podcast zinazo husu Benedikto XVI baada ya miaka kumi ya kujizulu

Tangu tarehe 11 Februari,kupitia ukursasa wa Vaticannews.va,kuna matukio matatu ya “Il pastore Benedetto”.'Mchungaji Benedikto'.Tangu siku zake za mwisho wa upapa na tangazo la ghafla la kujiuzulu na kukaa miaka kumi kama Papa Mstaafu,hadi simulizi za siku za hivi karibuni baada ya kifo chake.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Sauti za Mapapa, Sauti ya kumbukumbu na mahojiano ambayo hayajachapishwa ili kukumbuka kurasa za historia ya Kanisa. “Baba, mikononi mwako tunaiweka roho yake”. Ni maneno ya mnamo tarehe 5 Januari 2023, ambapo Papa Francisko alikabidhi kwa Bwana roho ya mtangulizi wake Papa Benedikto XVI, ambaye aliaga dunia mnamo tarehe 31 Desemba 2022 katika nyumba ya watawa ya Mater Ecclesiae, jijini Vatican, ambapo alikuwa akiishi kama Papa,  Mstaafu  kwa miaka kumi, mara baada ya kujuzulu kwake mnamo tarehe 11 Februari 2013.

Chaguo lake lililotangazwa katika ulimwengu kwa Kilatino, katika ukumbi wa Mkutano mbele ya Baraza la Makardinali, katika ufahamu wa mvuto wake na kwa uhuru kamili, ili kutoa muda wake timilifu wa  uzee wake  kuombea Kanisa. Miaka kumi baada ya tukio lisilo tarajiwa ambalo halikutokea kwa karne sita katika historia ya Kanisa, na zaidi ya mwezi mmoja na nusu baada ya  kutoweka kwa Papa Benedikto XVI, wafanyakazi na wahariri wa Radio Vatican,  Vatican News wamechagua kuielezea kwa njia ya podcast inayoitwa, “Il pastore Benedetto”,  yaani “Mchungaji Benedikto”. Vipindi vitatu ambavyo, kupitia mahojiano ya kumbukumbu na mengine ambayo hayajachapishwa, kwa mfano, siku zake za mwisho za Joseph Ratzinger, kifo chake na mazishi yake yaliyongozwa na Baba Mtakatifu Francisko.

Kwa miaka kumi aliishi kama Papa mstaafu “Siri katika Ulimwengu”, na “katika uzio wa Petro  na kisha siku za kuondoka kwake mnamo tarehe 11 Februari 2013,  kwenda na helikopta huko Castelgandolfo, na mnamo tarehe Februari 28, siku ya mwisho ya Upapa wake. Katika podcasts tatu, kuna ushuhuda na maoni ya Makardinali Marcello Semeraro na Gianfranco Ravasi, Askofu Mkuu Georgia Gänswein, Padre Federico Lombardi, Andrea Tornielli, Andrea Monda, Elio Guerriero na Padre  Roberto Regoli. Lakini pia rmarudio ya sauti na sauti za Papa Francisko na Papa Mstaafu Benedikto  na maoni ya mtaalamu wa mambo ya Vatican,  Valentina Alazraki, John Allen na Giovanna Chirri, baadaye  kukutana katika chumba cha waandishi wa habari cha Vatican, na tafakari za Askofu Mkuu Rino Fisichella, kati ya washirika au wahudumu wakuu wa Benedikto XVI

Kwa kuelezea suala la kujiuzulu,  Kardinali Angelo Sodano kama alivyofafanua, kusikiliza maneno wazi kwa upya, yenye nguvu na ya kusonga mbele, ambayo Papa Benedikto XVI  yaliichochea, wakati wa katekesi  yake ya mwisho ya kusisimua, kuwa fursa pia ya kusafisha uwanja, mara moja zaidi, kutoka katika mawazo ya kufikiria juu ya sababu zake na ulemavu wake. Kukusanya muafaka wa mikutano kadhaa na mikumbatio kati ya Papa Francisko na Papa Mstaafu Benedikto XVI, kati ya 2013 na 2023, inasaidia kuelewa jinsi Nyumba ya Mtakatifu Marta na Monasteri ya Mater Ecclesiae hazijawahi kuwa mbali bali karibu sana.

Taarifa za Papa katika mahojiano ya hivi karibuni alisema: “Pamoja na kifo cha Benedikto  XVI nilipoteza baba” yanapata mwangwi katika safu za matukio ya kuheshimiwa na mapenzi na katika Azimio la Ratzinger la mwezi Juni 2016 alipomwambia kuwa: “Baba Mtakatifu, wema wako ni mahali ninakoishi ”. Ni kusikiliza maneno ya shukurani ambayo kamwe hayana mpangilio au ya hali, ambayo Papa alimkumbuka mtangulizi wake baada ya kifo  kwamba “mtu mzuri na mtu mwenye fadhila, Mwalimu  wa katekesi kutoka katika mawazo ya papo hapo na ya heshima” , hiyo inamaanisha kuthamini ushirika na mwendelezo kati ya  Papa Francesko  na Benedikto XVI.

Moja ya podcast kuhusu Papa Mstaafu Benedikto XVI
12 February 2023, 11:46