Tamko la uwakilishi wa kisheria katika Baraza la Kipapa la Uinjilishaji
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Fransisko amesasisha sheria iliyokuwa ya Papa Paulo VI katika usimamizi wa ndani wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji ambayo, pamoja na Katiba ya Praedicate Evangelium imeundwa kwa Sehemu mbili zinazoongozwa na wenyeviti wawili na wakati Papa mwenyewe ndiye anayehusika zaidi na sehemu hiyo. Tangu nyakati za Papa Montini yaani Paulo VI, na kabla ya Katiba ya Kitume iliyotolewa mwaka mmoja uliopita, mmiliki wa uwakilishi wa kisheria “kamili na kabisa” wa Propaganda Fide ya kale, ambayo kwa Papa Yohane Paulo II baadaye ilikuja kuwa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu Mwenyekiti alikuwa yeye mwenyewe.
Kuwajibika kwa masuala yote ya kiuchumi na kiutawala
Katika tamko lililotolewa Ijumaa tarehe 17 Machi 2023 , Papa anabainisha kwamba, bila ya kuathiri wajibu wa kutoa maelezo yanayostahili kwa Sekretarieti ya Uchumi, “uwakilishi kamili wa kisheria wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji katika kitengo cha II ambacho(zamani kilikuwa ni Baraza la Uinjilishaji wa Watu na Baraza la Takatifu la Uinjilishaji wa Watu au de Propaganda Fide) kwa mambo yote ya kiuchumi, kiutawala, mazungumzo na warithi ambayo yanawahusu, iwahusishe wenyeviti wa Kitengo cha uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya ya Kanisa kwa ajili ya Uinjilishaji, kwa nguvu zote na uwezo wote wa sheria”.
Uwakilishi huu, katika tamko hilo unathibitishwa na kupanuliwa pia kuhusiana na mali zinazokusudiwa kwa ajili ya utume wa vyombo vingine vinavyokabidhiwa au kutegemewa na Kitengo cha Pili cha Baraza la Kipapa kama vile Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa(PMS), Shirika la Kipapa la Uenezaji wa Imani, Shirika la Kipapa la Mtakatifu Petro Mtume, Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu wa Kimissionari na Umoja wa Kimissionari wa Kipapa, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana, Mfuko wa “Domus Missionalis” na Mfuko wa “Domus Urbaniana”.
Makatibu wasaidizi wawili
Zaidi ya hayo, pamoja na maandishi baada ya mkutano na Kadinali Luis Antonio G. Tagle, ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza aliamuru kwamba Kitengo cha kwanza cha Uinjilishaji wa kwanza na Makanisa mapya ya Kanisa la Uinjilishaji yawe na makatibu wasaidizi wawili wa Kwanza ma rais wa Mashirika ya Kimissionari ya Kipapa, yenye dhamana ya kusimamia masuala ya kiuchumi yanayokusudiwa kwa ajili ya ushirikiano wa kimisionari na mgawanyo wake sawa; na wa Pili katika wadhifa wake kama mkurugenzi wa Ofisi maalum ya Baraza la Kipapa hilo anayesimamia usimamizi wa urithi unaokusudiwa katika utume. Wote wawili kwa mujibu wa maadhiko ya Dikirii hiyo watafanya marejeo ya moja kwa moja kwa Mwenyekiti wa Kitngo cha Pili cha Baraza la Kipapa ambalo limepewa uwakilishi wa Baraza la Kipapa katika masuala ya kiuchumi.