Papa Franisko na Askofu Mkuu  Justin Welby wa Canterbury Papa Franisko na Askofu Mkuu Justin Welby wa Canterbury 

Miaka 10 ya Papa:Matashi mema kutoka kwa Askofu mkuu Justin Welby

Askofu Mkuu wa Canterbury na Mkuu wa Kanisa la Kianglikani amemtumia matashi mema Papa Francisko kwa kutimiza miaka 10 ya upapa wake. "Kuna ukina ambao ni Baraka kwa Kanisa lote na si tu kwa ajili ya Kanisa Katoliki la Roma".

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Katika fursa ya kufanya kumbu kumbu ya miaka kumi ya upapa wa Papa Francisko, Askofu Mkuu wa Canterbury na Mkuu wa Kanisa la Kianglican, Justin Welby amemtumia matashi mema Papa Francisko. Katika matashi hayo Askofu Mkuu anaandika kuwa: “ kwa mara ya kwanza nilipokutana na Papa Francisko ilikuwa ni miezi miwili au mitatu mara tu baada ya kuanza utume wangu na nilikuwa nimechanganyikiwa. Nilikuwa sijawahi kukutana na Papa, na sikujua nifikirie nini, sikujua ni mtu wa aina gani. Tuliingia ndani na kukaa na yeye aliniambia: “Mimi ni mkubwa kuliko wewe”… na mimi nilifikiri:  “oo mama yangu, atakuwa ni mmoja wa wale…”. Na yeye aliongeza: “… kwa siku tatu”. Kwa sababu alikuwa ameanza upapa wake siku tatu kabla ya kuanza jukumu langu. Mwanzo huo ulinionesha mengi ya Papa Francisko na uliweka mengi, juu ya tabia yangu na uzoefu wake”.

Askofu Mkuu Welby anabainisha: “Nilifanya uzoefu wa ubinadamu maalum wa kina ambao hakuna ambaye anashuka ahadi ya ukweli na ambaye anachangia juu ya kuwa binadamu katika thamani isiyohisha. Wengi wanasema,  lakini na mimi ninamwambia, yeye anaishi”. Jambo la pili ni ufunguzi wa juu katika umoja wa kimaadili. “Yeye anatafuta kutazama matatizo kwa njia ya lenzi tofauti, kwa namna tofauti. Labda ndio chimbuko la kijesuit. Sijuhi, inatokea mara nyingi na wajesuit, lakini matokeo ambayo ni katika  kukabiliana na matatizo, ya pembeni yanayoshangaza”.

Askofu Mkuu Welby amesema “Ikiwa unazungumza naye masuala mengi ambayo Kanisa linapaswa kukabiliana nayo, yeye anatazama katika moyo wa mtu na kupata njia ya kupenda ambayo inasaidia kutoa kizuizi cha sehemu ya moyo uliomgumu. Jambo la tatu ambao ninapenda kusema juu yake ni ule urahisi wake ambao unajionesha wazi, mambo hayo matatu: uwezo mkubwa kiakili na kutambua, ukina wa moyo wake na urahisi wake ambao unamsaidia kufikia kwa kila hali na maalum wale ambao wako mbali na Kanisa, kama alivyokuwa anafanya Yohane Paulo II”. Kwa kuhitimisha amebainisha kuwa: “Kuna ukina ambao ni Baraka kwa Kanisa lote na si tu kwa ajili ya Kanisa Katoliki la Roma”.

12 March 2023, 16:38