Papa Francisko akiwa amekaa karibu na  Al Tayyeb wakati wa Ziara yake ya kitume  katika Ufalme wa Bahrain Papa Francisko akiwa amekaa karibu na Al Tayyeb wakati wa Ziara yake ya kitume katika Ufalme wa Bahrain  (ANSA)

Miaka 10 ya Upapa,Al-Tayyeb:Ziara za Papa za kujenga madaraja ya udugu

Matashi ya heri kutoka kwa Imamu Mkuu wa al-Azhar kwa Papa katika kumbukumbu ya miaka kumi ya upapa wake:“Ninamuomba Mwenyezi Mungu azibariki juhudi zako katika kutafuta amani na atusaidie pamoja na watu wenye mapenzi mema kutimiza wajibu wetu wa kidini na kimaadili wa kuendeleza amani,kuimarisha maelewano na mshikamano wa pamoja”

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Katika barua ya matashi mema kutoka kwa Ahmad Al Tayyeb Imamu Mkuu wa Al-Azhar anaaza kumtuma salamu kwamba “Mpendwa rafiki na kaka Papa Francisko, salamu njema. Ninafurahi kutuma pongezi zangu za dhati kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka kumi ya uongozi wako kama Papa na Mkuu wa Kanisa Katoliki. Ninajivunia kuthamini safari yako adhimu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, ambapo ulitaka kujenga madaraja ya upendo na udugu kati ya wanadamu wote, na juhudi zako za kuhimiza maadili ya udugu wa kibinadamu na kuanzisha mazungumzo kati ya wafuasi wa dini, kama msingi wa kupata amani ambayo sote tunaitamani”.

Imamu wa Alzhar, aidha aandika kuwa: “Ndugu yangu Baba Mtakatifu Francisko, Dunia yetu ya leo imejaa changamoto, migogoro na matatizo katika ngazi zote za kimaadili, kiuchumi na kijamii, jambo ambalo linaongeza mateso ya watu wengi; kwa hili, wajibu wa viongozi na kielelezo thabiti kama wewe katika  kupunguza mateso ya watu na wanyonge unakuwa mkubwa. Ninamuomba Mwenyezi Mungu azibariki juhudi zako katika kutafuta amani na atusaidie pamoja nanyi na wote wanaopenda wema na watu wenye mapenzi mema, ili kutimiza wajibu wetu wa kidini na kimaadili wa kuendeleza amani na kuimarisha maelewano na mshikamano wa pamoja”. Kwa kuhitimisha Imam Al Tayyeb anaandika kuwa: Kaka yangu mpendwa na uweze kubarikiwa na afya njema, ustawi na furaha na Mungu Mwenyezi akubariki daima. Ninakaribisha kwa furaha mpango wowote wa kufanya kazi pamoja ili kufikia udugu wa kibinadamu ili usalama, utulivu, kuishi pamoja na utulivu viwepo katika ulimwengu wetu”.

Matashi Mema kutoka kwa Iman Mkuu Al Tayeeb
12 March 2023, 20:18