Papa Francisko wakati akitoa baraka ya kwanza mnamo tarehe 13 Machi 2013. Ni miaka kumi imepita Papa Francisko wakati akitoa baraka ya kwanza mnamo tarehe 13 Machi 2013. Ni miaka kumi imepita 

Miaka 10 ya Upapa wa Papa Francisko:Ad multos annos,Baba Mtakatifu

Papa Francisko anapoadhimisha kumbukumbu ya miaka 10 ya upapa,Mkurugenzi wetu wa Tahariri na Mkurugenzi wa Osservatore Romano wanaeleza jinsi Vyombo vya Habari vya Vatican kufafanua hatua hii muhimu ya kihistoria na kumtakia heri na baraka Baba Mtakatifu.

Na Andrea Tornielli na Andrea Monda

Jioni ya tarehe 13 Machi  2013, Jorge Mario Bergoglio alionekana, kwa mara ya kwanza, kwenye loggia ya katikati ya Kanisa Kuu la Mtakatifu  Petro akiwa amevaa nguo nyeupe. Pamoja na heshima ya upendo kwa mtangulizi wake aliyestaafu, salamu yake ya awali tayari ilikuwa na vipengele kadhaa muhimu vya Upapa wake: mkazo wa kuwa Askofu wa Roma wa Kanisa “mwenye kusimamia kwa upendo juu ya Makanisa yote”; katikati ya watu waamini wa Mungu ambao Mchungaji mpya aliomba baraka kabla ya kuitoa mwenyewe; na maombi kwa ajili ya “udugu mkubwa” katika ulimwengu uliosambaratishwa na ukosefu wa haki, vurugu na vita.

Siku zilizofuata, Papa alieleza maana ya jina alilolichagua, akihusisha na ndoto ya “Kanisa lililo maskini na la maskini”. Francis wa Assisi, alisema, ni “mtu wa umaskini, mtu wa amani, mtu anayependa na kulinda uumbaji”. Miezi michache baadaye, mnamo Novemba mwaka huo huo, Papa alichapisha Waraka wake wa Kitume wa Evangelii Gaudium, ambao ulitoa mwongozo wa  kweli wa upapa wake. Pamoja na hayo, aliwataka Wakristo kushuhudia furaha ya Injili kwa maisha yao, pamoja na kuleta kila mahali, hasa kwa wale wanaoteseka zaidi, ukaribu na huruma ya Mungu wetu anayesamehe, kukaribisha na kukumbatia.

Miaka kumi baadaye, sisi katika Baraza ya kipapa la Mawasiliano Vatican tulijiuliza ni kwa namna gani tunaweza kusherehekea ukumbusho huu katika vyombo vyetu mbalimbali vya habari. Hatua kwa hatua, wazo lililoibuka ambalo halikuwa likizungumzwa sana juu ya Papa Francisko, lakini la kutoa nafasi kwa kile ambacho ushuhuda wake na Majisterio yake yamechochea au kusaidia kuhamaisha. Kwa hiyo tulichagua kutoa nafasi kwaajili ya  shuhuda mbalimbali za watu kutoka katika hali mbalimbali duniani: kwa wale ambao kila siku wanatambua uso wa Mnazareti kwa wale wanaoteseka, kukataliwa, au walio mbali; na, kwa wale wanaosimulia historia za ajabu zinazoandika nguvu ya upendo na muujiza wa msamaha katika mazingira ya chuki au kutojali.

Kila moja zinaelezea kurudiwa kwa moja ya mada kuu za Papa Francisko, ikiunganisha mawe ya mapambo mazuri ambayo yainafufua matumaini. Tumaini hili linawezekana, licha ya ishara nyingi za huzuni tunazoshuhudia kwa bahati mbaya, ya kwanza ambayo ni hatari kubwa zaidi kwa wanadamu kujiangamiza. Kutoa sauti kwa ushuhuda kulionekana kwetu kuwa njia mwafaka zaidi ya kuwasikiliza watu wa Mungu wanaompenda Fransisko na kuendelea kumwombea. Watu hawa wanamfuata Papa, na wanamgeukia, pamoja naye, kwa Yesu kwa maneno ya Petro, wakitambua chanzo cha matumaini na wokovu: “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai”.

Tornielli e Monda wanamtakia heri nyingi Papa Francisko
13 March 2023, 09:52