Tafuta

2020.03.12 kuchaguliwa kwa Papa Francisko   13 Machi 2013 2020.03.12 kuchaguliwa kwa Papa Francisko 13 Machi 2013 

Papa Francisko:miaka 10 ya ari ya kimisionari na njia za huruma

Miaka kumi imepita tangu mnamo tarehe 13 Machi 2013,siku ambayo Jorge Mario Bergoglio alichaguliwa katika kiti cha Mtume Petro.Yeye ni Papa aliye na shauku ya uinjilishaji na njia ya kudumu ya kulirekebisha Kanisa katika maana ya kimisionari.Ni muongo wenye vipimo viwili tofauti:Katika maendeleo na michato yake ni utajiri wa mawazo na moyo.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Wakati ni mkuu kuliko nafasi": hakuna uthibitisho wa Papa Francisko, uliomo tangu mawaidha yake ya kwanza ya kitume, Evangelii gaudium, ambayo kwa maana zaidi yanajumuisha miaka kumi ambayo imepita tangu mwanzo wa upapa wake. Kwa Jorge Mario Bergoglio, kwa kweli - Papa Yesuit wa kwanza, mzaliwa wa kwanza wa Amerika ya Kusini, wa kwanza kuchagua jina la Francis na, katika nyakati za kisasa, kuchaguliwa baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake - "kutoa kipaumbele kwa nafasi kunamaanisha kuibua michakato na kujaribu kuizuia." Kinyume chake, "wakati huagiza nafasi, huangazia na kuzibadilisha kuwa viungo katika mnyororo unaokua kila mara, bila kurudi nyuma, ukionyesha wakati ujao na kutuhimiza kutembea kwa matumaini. Ni katika maana hiyo  kwamba inawezekana kuwa ufunguo wa kuelewa Upapa wa sasa ambao unajitokeza kwa njia mbili ya kwanza ju yamaendeleo na mwingine kuhusu kiroho.

Katiba ya Kitume "Praedicate evangelium

Katika Katiba ya Kitume Praedicate kuhusu uinjilishaji  juu ya Curia  Romana na huduma yake kwa Kanisa na kwa ulimwengu iliyotangazwa mnamo 2022, waraka huu unatoa muundo zaidi wa kimisionari kwa Curia Romana. Miongoni mwa uvumbuzi inaotanguliza, ni kuanzishwa kwa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo na na Baraza jipya la Uinjilishaji unaoongozwa na mwenyewe. Katiba mpya pia inazingatia ushiriki wa walei wanaume na wanawake pia katika majukumu ya serikali na wajibu wa ndani ya Curia Romana  na kukamilisha marekebisho mengi yaliyotekelezwa, katika muongo mmoja, na Papa Francisko katika nyanja ya kiuchumi na kifedha, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa sekretarieti ya  uchumi  mnamo mwaka 2015

Michakato yenye matunda iliyoanzishwa na Papa Bergoglio pia inahusu aina tatu maalum za safari za Kanisa: uekumene, mazungumzo ya kidini na sinodi. Eneo la kwanza ni alama, kwa mfano, mwaka 2015 na kuanzishwa kwa Siku ya Dunia ya Maombi kwa ajili ya Utunzaji wa  kazi ya Uumbaji, ambayo inaadhimishwa kila mwaka mnamo Septemba 1 pamoja na Kanisa la Kiorthodox, ili kuwahimiza Wakristo juu ya uongofu wa kiikolojia. Wito huohuo unasikika, kwa sauti kubwa na wazi, katika waraka wa pili wa Papa (wa kwanza, Lumen fidei, unashirikishwa na mtangulizi wake, Papa Benedikto XVI), Laudato si',  kuhusu utunzaji wa nyumba yetu pamoja, uliochapishwa pia mwaka wa 2015, msingi wa hati ni himizo la mabadiliko ya kweli ili mwanadamu achukue jukumu la kujitolea kutunza nyumba ya pamoja yaani mazingira. Ahadi ambayo pia inajumuisha kutokomeza umaskini, umakini kwa maskini na ufikiaji wa haki kwa wote kwa rasilimali za sayari.

Mkutano na Patriaki Kirill

Ilikuwa mnamo tarehe 12 Februari  2016, hata hivyo, huko Cuba, mkutano ulifanyika kati ya Francisko na Patriaki wa Moscow na Urussi yote, Kirill. Tukio  muhimu la wakati ambali lilinaona kutiwa saini kwa tamko la pamoja ili kutekeleza kile  ambach Papa anakifafanua kama Uekumene wa  upendo, yaani, dhamira ya pamoja ya Wakristo kujenga ubinadamu wa kindugu zaidi. Miaka sita baadaye, ahadi hiyo ni ya hali ya kuhuzunisha, kwa sababu ni baada ya Urussi kuivamia Ukraine, vita katikati ya Ulaya, vilivyowashikisha na Wakristo walioshiriki ubatizo uleule.

Mikutano wa Kiekumene

Pia sio rahisi  kusahaulika hija ya kiekumene ya amani nchini Sudan Kusini, iliyofanywa mwezi mmoja uliopita Papa pamoja na Askofu mkuu wa Canterbury, Justin Welby, na msimamizi wa mkutano mkuu wa Kanisa la Scotland, Iain Greenshields. Kuhusu mazungumzo ya kidini, hatua muhimu inawakilishwa na kutiwa saini, mnamo tarehe 4 Februari 2019, kwa hati ya udugu wa binadamu kwa ajili ya amani duniani  na kuishi kwa pamoja, iliyotiwa saini na Papa na Imamu Mkuu wa Al-Azhar Ahamad al-Tayyib, huko  Abu dhabi. Maandishi hayo ni hatua msingi katika mahusiano kati ya Ukristo na Uislamu, kwani yanahimiza mazungumzo baina ya dini na inalaani ugaidi na ghasia bila shaka.

Mikutano ya Sinodi

Kwa kwa upande wa sinodi,  papa Fransisko anatekeleza mabadiliko muhimu: Mkutano mkuu ujao wa kawaida, wa 16, uliopangwa kufanyika mjini Vatican mwaka 2023 na ule wa mwaka 2024, kwa kuongozwa na mada: "Kwa ajili ya Kanisa la Sinodi: Ushirika, Ushiriki na Utume", itakuwa ni hatua ya mwisho ya safari ya miaka mitatu inayojumuisha kusikiliza, kupambanua, kushauriana na kushirikishana katika awamu tatu, yaani jimbo, bara, na ulimwengu.

12 March 2023, 16:26