Papa ataadhimisha'masaa 24 kwa Bwana',huko Mtakatifu Maria wa Neema,Roma
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kwa mujibu wa Baraza la Kipapa katika kitengo cha masuala msingi ya Uinjilishaji ulimwenguni, kimetoa taafa kuwa toleo la X, la sala ya kuabudu kwa masaa 24 kwa Bwana, linarudiw tena mnamo tarehe 17 na 18 Machi 2023, ambalo ni mpango wa Kwaresima wa maombi, kuabudu na upatanisho ulioanzishwa na Papa Francisko. Kwa maana hiyo hata mwaka huu, tukio hilo litaadhimishwa katika majimbo yote ulimwenguni, katika mkesha wa Dominika ya 4 ya Kwaresima, ambayo ni Ijumaa na Jumamosi. Kwa hiyo katika maandalizi ya Pasaka ya Ufufuko wa Bwana, Makanisa yote ulimwenguni yatabaki yamefunguliwa kwa siku nzima kwa namna ya kuwapatia uwezekano waamini wote na mahujaji kuwa na fursa ya kukaa muda wowote ule wa kuabudu na fursa ya kuungama dhambi binafsi.
Katika fursa hiyo Mwaka huu, tabia kuu ya uwepo wa jumuiya za kiparokia, ni kwamba Papa Francisko ataadhimisha masaa 24 kwa ajili ya Bwana, mnamo tarehe 17 Machi 2023 saa 10.30 jioni katika Parokia ya Mtakatifu Maria wa Neema huko Trionfale, Roma katika na wakati huo katika uwanja wa Mtakatifu Maria wa Neema, maadhimisho hayo yatakuwa na uwezekano kwa waamini wote wanaopenda kutubu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kitengo cha Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wanabainisha kuwa tiketi za ushiriki wa maadhimisho hayo zitakuwapo hadi kikomo cha kujaza Kansa la Kiparokia na wanaweza kuomba kwa kujaza fomu kupitia ukurasa huu: http://www.evangelizatio.va/content/pcpne/it/attivita/24ore/24-ore-per-il-signore2023/biglietti.html. Tiketi hizo zinaweza kuchukuliwa katika jengo lilipo, Via della Conciliazione 7, Jumatano 15 na Alhamisi 16 Machi kuanzia saa 2.30 hadi 7.30 na kuanzia saa 9.00 alasili hadi saa 11.30, au Ijumaa 17 Machi kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi saa 7.30 mchana.
Matayarisho na ushauri wa sala mbele ya kuabudu Yesu
Milango iliyofunguliwa ya makanisa ni alama ya upendo wa Mungu wa huruma. Katika maandalizi ya masaa 24 kwa Bwana, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, limechapisha miongozi ya kichungaji ambayo imetayarisha sala binafsi na ushauri kwa ajili ya maadhimisho katika jumuiya. Kwa hiyo ni kupyaisha mapendekezo kwa majimbo na maparokia, nchini Italia na katika ulimwengu wote wa maadhimisho katika wakati wa sala hata katika jumuiya binafsi. Mwongozo uliochapishwa na Shalom, unaweza kununuliwa katika toleo la karatasi katika maduka ya vitabu na maduka ya mtandaoni. Katika matoleo ya Kiingereza, Kihispania na Kireno, maandishi yanaweza kupakuliwa kutoka kwenye tovuti hii:sito