Papa atia moyo jumuiya ya Termoli baada ya miaka 40 ya ziara ya Wojtyla!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Ilikuwa tarehe 19 Machi 1983 wakati Papa Wojtyła (Yohane Paulo II) alipotembelea jiji la Termoli nchini Italia na kufika huko helikopta kwenye bandari ya jiji, ambapo alitembelea Kanisa kuu, akisimama katika sala mbele ya masalio ya mwili wa Mtakatifu Timotheo, na kisha alifikia eneo kubwa, ambalo baadaye limewekwa jina la Uwanja wa Yohane Paulo Paolo II, mahali alipoadhimisha Misa Takatifu. Kwa hiyo tarehe 19 Machi baada ya miaka 40 Jimbo hilo la Termoli-Larino limetayarisha wiki ya matukio na mikutano ya kuadhimisha wakati huo wa kihistoria. Katika siku ya mwisho ya sherehe, hiyo Dominika 26, jiwe la msingi la kwanza la kazi ya sherehe pia litawekwa, katika “Villaggio Laudato si'”, ambacho ni kituo kinachokusudiwa kuwakaribisha watu wenye ulemavu. Pia atakuwepo Kardinali Giovanni Battista Re, Dekano wa Baraza la Makardinali, ambaye ataongoza Misa katika Kanisa la Mtakatifu Timoteo siku hiyo asubuhi.
Jiwe la msingi kubarikiwa na Papa
Jiwe la msingi kwa ajili ya kituo kipyya lilibarikiwa mnamo tarehe 14 Machi 2023 na Baba Mtakatifu Francisko, wakati wa mkutano wa faragha mjini Vatican kwa wawakilishi wa eneo hilo ambao walikuwa ni pamoja na Askofu Gianfranco De Luca, Meya wa Termoli, Bwana Francesco Roberti, na Paroko wa Mtakatifu Timoteo, Padre Benito Giorgetta. “Niliona kuwa mna mipango mingi, ya maendeleo, ya huduma kwa jamii yenu” alisema Baba Mtakatifu katika ujumbe kwa video kwa ajili ya Jimbo hilo la Termoli-Larino iliyorekodiwa kwenye fursa hiuo ya mkutano kwa ajili ya wanajimbo. “Asante kwa uchangamfu wenu. Kanisa ambalo halipo hai si Kanisa, ni Kanisa la uongo. Na ninaona mnachangamka. Haya ndiyo maisha: msipoteze furaha yenu na enenda mbele na kusali, daima”. Na kuhusiana na pingamizi za wale ambao hawataki kusali kwa sababu wanahisi kuwa ni wenye dhambi, Papa alisema “Ombeni zaidi, Bwana awapenda, Bwana amekuja kwa ajili ya wenye dhambi. Hakuna anayehisi kutengwa na Bwana, kwa hiyo kuweni na ujasiri, na Bwana awabariki wote na mniombee” alihitimisha.
Kumbatio la huduma ya kudumu
Katika ratiba ya sherehe hiyo yenye ishara ya “kumbatio ambalo hudumu ni kwa muda’ wa kudumu kama ilivyoandikwa kwenye bango, unazingatia uharaka wa mkataba mpya wa elimu. Kwa sababu, Askofu De Luka ameeleza kuwa walifikiri kutoa juma moja la mikutano na tafakari kuanzia pendekezo la “Mkataba wa Elimu”, uliozinduliwa na Papa Francisko mnamo tarehe 12 Septemba 2019, ambao pia unahusishwa na mahubiri yaliyotolewa mnamo 1983 na Mtakatifu Yohane Paulo II, ambapo alitaja jamii isiyo na baba, ambayo ni kitovu cha kumbukumbu zinazohitajika na zenye uwezo wa kuelimisha, kuunganisha na kujenga mahusiano mazuri katika kila mazingira ya jamii, kutoa mitazamo na miongozo yenye mamlaka na nyeti kwa vizazi vipya”. Katika ufahamu kwamba kamwe kama wakati huu sasa, kuna haja ya kuunganisha juhudi katika muungano mpana wa elimu kwa ubinadamu wa kindugu zaidi, kwa hivyo matukio yalibuniwa, pamoja na Ishara ya Kazi Kituo cha “Villaggio Laudato si'”, yaani Kijiji cha Laudato.
Mtakatifu Yohane Paulo II aliacha ishara
Kwa maana hiyo Mtakatifu Yohane Paulo II aliacha alama katika jiji la Termoli kwa mujibu wa maelezo ya Askofu De Luca. Na kwamba maadhimisho hayo ya miaka 40 yanaacha ishara nyingine, yaani ndogo, isiyo na mvuto, lakini katikati ya jiji. Askofu alirejea kwa usahihi juu ya muundo mpya ambao, kutokana na mchango, utatumika kuwakaribisha, kuwatunza na kuwasindikiza watu wenye ulemavu ambao wamepoteza wazazi wao, pamoja na kubaki wazi kwa wote dhaifu. Hata paroko Padre Giorgetta alitoa shukrani zake kwa Papa: "kwamba Pamoja na umri wake na matatizo, Papa Fransisko ni mtu asiyejizuia, anajitolea, hasa linapokuja suala la ishara za tahadhari na kwa ukweli kwamba yeye mwenyewe ni mdhaifu zaidi.' Katika ujumbe huo wa kwa njia ya video, Papa alisifu uchangamfu wa Kanisa mahali hapo kwamba kwao Papa ni sura ya baba anayetambua wema wa watoto wake na kuwahimiza kusonga mbele. Ushauri wake ni sindano ya uaminifu, mapenzi, ubaba na faraja.