Maandamamo makubwa huko Ugiriki mbele ya Bunge baada ya ajali kubwa ya teni huko Athene . Maandamamo makubwa huko Ugiriki mbele ya Bunge baada ya ajali kubwa ya teni huko Athene .  (ANSA)

Papa Francisko:Mawazo kwa wanafunzi waliopata ajali huko Ugiriki

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa amewaombea wanafamilia wa waathirika wa janga la ajali ya treni iliyotokea Mosi Machi na kumwomba Mama Maria ili awe faraja.Dominika 5 Machi ni maandamano makubwa ya kupinga serikali huko Athene

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Mawazo ya kwanza ya Papa Francisko  katika salamu zake baada ya  Sala ya Malaika wa Bwana Dominika Machi 5 yamewaendea wahanga na familia zao za mkasa wa treni nchini Ugiriki. Papa amesema “Siku hizi, mawazo mara nyingi yaligeuka kwa waathika wa ajali ya Treni huko Ugiriki: wengi walikuwa wanafunzi vijana. Ninawaombea marehemu; Niko karibu na majeruhi, wanafamilia, Mama Yetu awafariji”.

Jamaa ya wathirika wakiweka maua mahali pa tukio huko Larissa
Jamaa ya wathirika wakiweka maua mahali pa tukio huko Larissa

Wakati huo huo, nchi imepokea samahani kutoka kwa waziri mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis. “Ninaomba radhi kwa jamaa wa waathirika" ni Maneno ya mkuu wa serikali siku tano baada ya mkasa wa treni, huko Larissa, kati ya Thessalonike na Athene, ambayo ilisababisha vifo vya watu 57, vilivyotokana na makosa ya kibinadamu na uzembe, ambao bado leo hii wanashughulikia. Nchi nzima lakini, zaidi ya yote, kwa familia za wale waliouawa katika janga hilo, wanaandamana  wakiomba “kujua kwa kile kilichotokea na kueleza kwamba huko Ugiriki mnamo 2023, haiwezekani kwa treni mbili kusafiri kwa njia tofauti kwenye mstari huo huo na usitambuliwe na Mtu.

Maandamamo  dhidi ya serikali ya Athene kufuatia na ajali ya treni.
Maandamamo dhidi ya serikali ya Athene kufuatia na ajali ya treni.

Wakati huo huo, maandamano hayo yanaendelea, Dominika tarehe 5 Machi  asubuhi wanafunzi, wafanyakazi wa reli na wafanyakazi wa sekta ya umma walikusanyika kwa maandamano muhimu dhidi ya serikali katikati ya jiji, katika uwanja wa Syntagma, mbele ya Bunge, ambapo zaidi ya watu elfu saba walikusanyika lakini pia kutokea mapigano kati ya polisi na waandamanaji. Jamaa wa waathiriwa badala yake walikusanyika karibu na eneo la mkasa. Wakati huohuo kikao cha mkuu wa kituo mwenye umri wa miaka 59 anayedaiwa kufanya kosa la vifo kilichosababisha ajali ya magari hayo mawili kugongana kimeahirishwa. Jaji mchunguzi wa Larissa atalazimika kuamua kama atapinga uhalifu wa kuua bila kukusudia.

Ilifanyika hata mkesha wa maombi kwa ajili ya marehemu wa ajali ya treni mbili zilizogongana
Ilifanyika hata mkesha wa maombi kwa ajili ya marehemu wa ajali ya treni mbili zilizogongana
Wito wa Papa na maombi
05 March 2023, 13:02