Tafuta

Papa Francisko:Uso wa Yesu ni uzuri wa Baba hata ukiharibika msalabani!

Papa akitafakari Injili ya Dominika ya II ya Kwaresima,ameshauri waamini kuona uzuri wa watu walio karibu nao.Upendo wao unashuhudia uwepo wa Mungu na kujaza mioyo kwa huduma ya ukarimu zaidi kwa wengine.Uzuri na fahari iliyooneshwa kwa wanafunzi wake ni sawa na ule atakapokuwa msalabani na kuharibika.

Anangella Rwezaula, - Vatican.

Katika Dominika ya II ya Kwaresima Injili inaeleza juu ya Kugeuka Sura. Yesu aliwapeleka juu ya mlima Petro, Yakobo na Yohane na anajionesha kwao uzuri wake wote wa Mwanga wa Mungu (Mt 17, 1-9). Tusimame kidogo katika tukio hili na kujiuliza: uzuri huu ni wa kitu gani? Wanafunzi  waliona nini? Je ni matokeo ya kitamasha? Ndivyo Baba Mtakatifu Francisko ameanza tafakari yake kabla ya Sala yas Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 5 Machi 2023 kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican. Akiendelea amejibu maswali hayo kwamba “Hapana sio hivyo. Waliona mwanga wa utakatifu wa Mungu anayeng’aa katika uso na katika mavazi ya Yesu, picha kamili ya Baba. Anajionesha fahari ya Mungu, uzuri wa Mungu. Lakini Mungu ni Upendo na kwa hiyo wanafunzi waliona kwa macho yao uzuri na mwanga wa upendo wa mungu aliyejifanya mtu katika Kristo.”  Kwa njia hiyo waliona utangulizi wa mbingu! Ni mshangao kwa wanafunzi! Waliokuwa wamepata kumwona kwa macho yao kwa muda mrefu uso wa upendo na wakati huo  hawakuwa wamegutuka kuelewa jinsi gani  usu huo ulikuwa  mzuri! Ni sasa tu ndipo wanaelewa kwa furaha kubwa.

Umati wa waamini katkka sala ya Malaika wa Bwana 5 Machi 2023
Umati wa waamini katkka sala ya Malaika wa Bwana 5 Machi 2023

Baba Mtakatifu Francisko amesema “Kiukweli Yesu katika uzoefu huu yupo anawaunda, anawaandaa hatua ambayo itakuwa muhimu zaidi. Tangu hapo, taratibu wao kiukweli wanapaswa kuanza kumjua katika Yeye uzuri na fahari iliyooneshwa kwenye Mlima Tabor ule ule uzuri wa uso wake atakapopanda msalabani na kuharibika na hautatamanika. Kwa upande wa Petro inakuwa vigumu kuelewa. Anataka kusimamisha muda na kuuweka mapumziko, kukaa hapo kuongeza muda huo wa uzoefu wa ajabu, lakini Yesu hakumruhusu. Mwanga wake, kiukweli hauwezi kupunguzwa na wakati wa kimazingaombwa! Kwa kufanya hivyo ingekuwa isio kweli, ya kijujuu. Ambayo inapotea kwenye ukungu wa hisia za kijujuu. Kinyume chake Kristo ni mwanga ambao unaelekeza safari kama nguzo ya moto kwa watu wa huko kwenye jangwa (Kut 13,21). Papa ameongeza kusema kuwa “Uzuri wa Yesu hauwatenganishi wanafunzi na uhalisia wa maisha, bali unawapa nguvu ya kumfuata Yerusalemu, msalabani. Uzuri wa Kristo sio kutengwa, siku zote unakupeleka mbele, haukufanyi ujifiche bali una songa mbele!”

Umati wa waamini kutoka sehemu mbali mbali za dunia wakisali na Papa
Umati wa waamini kutoka sehemu mbali mbali za dunia wakisali na Papa

Baba Mtakatifu Francisko kwa maana hiyo amesema Injili inaweka njia hata kwa ajili ya njia yetu: inatufundisha ni jinsi gani ilivyo muhimu kukaa na Yesu, hata ikiwa ni ngumu kulewa yote ambayo yeye anasema na anafanya kwa ajili yetu. Ni kukaa na Yeye, kiukweli ambamo tunajifunza kujua, juu ya uso wake, uzuri angavu wa upendo ambao unajitoa, hata kama unapelekea ishara za msalaba. Ni pale katika shule yake tunajifunza kupokea uzuri sawa wa nyuso za watu ambao kila siku wanatembea karibu nasi: wanafamilia, marafiki, wafanyazi wenzetu, na ambaye kwa namna nyingine anatujali. Ni nyuso ngapi angavu, ni tabasamu ngapi, ni makunyazi mangapi, ni machozi gani na makovu ambayo yanazungumza juu ya upendo unaotuzunguka!

Waamini na mahijaja katika uwanja wa Mtakatifu Petro kusali sala ya Malaika wa Bwana
Waamini na mahijaja katika uwanja wa Mtakatifu Petro kusali sala ya Malaika wa Bwana

Baba Mtakatifu anasisiza kuwa tujifunze kuyatambua na yajaze moyo. Na baadaye tuondoke ili kuwapelekea hata wengine mwanga ambao tumeupokea, kwa matendo ya dhati ya upendo (1Yh 3,18) kwa kupiga mbizi na ukaribu zaidi katika shughuli zetu za kila siku, kwa kupenda, kuhudumia na kusamehe kwa ari mpya na uwezekano. Tunaweza kujiuliza: je tunajua kutambua mwanga wa upendo wa Mungu katika maisha yetu? Tunautambua kwa furaha na shukrani katika sura za watu ambao wanatutakia mema?  Je tunatafuta karibu nasi ishara za mwanga huo, ambao unatujaza moyo na kufunga upendo na katika huduma? Au tunapendelea moto wa nyasi za miungu, ambazo zinafunda na kutufunga sisi binafsi?  Papa ameongeza kusema: “Tafakari ya maajabu ya Mungu, kuutafakari uso wa Mungu, wa uso wa Bwana, ni lazima utusukume kuwatumikia wengine”. Maria aliyetambua kuhifadhi katika moyo wake mwanga wa Mwana wake hata katika giza la Kalvari atusindikize daima katika njia ya upendo. Baba Mtakatifu amehitimisha.

Tafakari ya papa
05 March 2023, 12:51