Papa Francisko-waseminari watembee pamoja na kushuhudia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 6 Machi 2023 amekutana mjini Vatican na Jumuiya ya Siminari ya Jimbo ya Mtakatifu Maria wa Cleveland (Ohio - USA) Katika hotuba yake baada ya kuwakaribisha na kuwasalimia mapadre, mashemasi, waseminari. wakufunzi na wanafanyakazi wa seminari hiy,o amemshukutu Askofu Malesic kwa maneno ya hotuba yake kwa niaba yao. Ziara ya jijini Roma katika moyo wa Kanisa umewadia katika muktdha wa kusheherekea maiaka 175 tangu kuaznishwa kwa seminari yao. Kwa hiyo ni fursa ya kumushukuru Mungu kwa idadi kubwa ya mapadre waliofundwa katika Taasisi hiyo kwa miaka yote. Papa amewapongeza kwa sababu seminari yao inaendelea kujibu mahitaji ya sasa ya Kanisa, kwa kuelimisha, kufunda mashemasi na wahudumu walei ili kuwasadia wajumbe wa Watu wa Watakatifu wa Mungu katika kuishi wito wao wa kuwa wamisionari. Wito huu unachukua maana yake daima iliyo kubwa kwa mwanga wa mchakato wa kisinodi wa Kanisa zima ulioanzishwa.
Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amependa kushirikishana nao kwa ufupi tafakari kuhusu tabia tatu za mchakato wa kisinodi ambazo ni muhimu hata kwa ajili ya mafunzo yao kama makuhani wajao na wahudumu wa Injili. Kwanza kabisa tabia ni usikivu, hasa wa Bwana. Tunajua kwamba peke yetu hatuwezi kufanya lolote kwa sababu: “Bwana hasipojenga nyumba. Waijengao wafanya kazi bure(Zab 127,1). Utambuzi huu unatualika kufanya nafasi kila siku katika maisha yetu kwa Bwana, kutafakari neno lake, kutafuta nuru ili mchakato wetu wa safari kwa msaada wa msindikizaji wa kiroho, hasa kwa kupitia kipindi na Bwana katika sala, kwa kumsikiliza kwa ukimya mbele ya Tabernakulo.
Baba Mtakatifu kwa maana hiyo amewaomba wasisahau kamwe, umuhimu wa kujiweka mbele ya Bwana ili kusikiliza kile ambacho anapenda kuwapa. Kiukweli kusikiliza sauti ya Mungu katika ukina wa moyo wetu na kuwa na utambuzi wa mapenzi yake ni wa lazima sana katika maisha ya ukuaji wa ndani, hasa tunapojikuta mbele ya zoezi kubwa na gumu. Katika kupendekeza kwa maisha ya seminarini tayari yanawapa uwezekano wa kukuza tabia ya sala ambayo inawasaidia katika huduma ya baadaye. Na wakati huo huo kusikiliza Bwana kunapelekea hata jibu la imani kwa kile ambacho Yeye alifunua na ambacho Kanisa linaonesha, ili waweze kufundisha, na kuwatangazia wengine, ukweli na uzuri wa Injili kwa namna ya dhati na furaha.
Tabia ya Pili ambayo ni ya mchakato wa kisinodi, aliyopendekeza kwao ni kutembea pamoja. Katika wakati wao wa mafundo seminarini ni fursa ya kujikita kwa kina katika roho ya umoja kindugu, na sio tu wao kwa wao, bali hata na Askofu wao, Ukleri mzima wa Kanisa mahalia, watawa na waamini walei, kwa namna ya kuwa kama Kanisa la ulimwengu. Hii lazima wajitambue kuwa sehemu moja pekee kubwa ya watu ambao walipokea ahadi ya Mungu kama zawadi na kama neema. Wakati huo huo, wito wao ni “zawadi ya kuweka katika huduma ya ujenzi wa mwili wa Kristo”(Ef 4,12). Kwa hakika mchungaji mwema anatembea pamoja na zizi, wakati mwingine mbele ili kuelekeza njia; mara nyingine katikati ili kutia moyo na wakati mwingine nyuma ili kuwasindikiza wale ambao wanapata ugumu. Baba Mtakatifu amewaomba wakumbuke daima kuwa ni muhimu kutembea pamoja kama zizi na kamwe wasitengane nalo.
Hatimaye tabia ya tatu, ambayo Baba Mtakatifu ameeleza ni ushuhuda. Kusikiliza Mungu, kutembea pamoja na wengine, inapelekea kuzaa matunda na kugeuka kuwa ishara hai ya uwepo wa Yesu katika ulimwengu. Kwa njia hiyo inawezekana kupitia miaka katika seminari wakijiandaa kujitoa kabisa kwa Mungu na wakati huo huo kwa watu watakatifu wa Mungu, katika upendo wa usafi wa moyo, na kwa muoyo usio gawanyika. Kanisa linahitaji ari yao, ukarimu wao na kwa bidii yao ya kuonesha kila mtu kwamba Mungu yu pamoja nasi daima, katika kila hali ya maisha. Papa anawaombea kwa mungu kwa aina nyingi za utume wa elimu na upendo ambazo wao tayari wanajibidisha,ili weweze kuwa ishara ya Kanisa linalotoka nje ( Evangelii gaudium, 20) wakishuhudia, na kushirikisha upendo wa huruma ya Yesu kwa wajumbe wote wa familia ya binadamu, hasa maskini na wenye kuhitaji.
Kwa kuhitimisha Papa amerudia kusema kuwa kusikiliza, kutembea pamoja na kushuhudia ndizo harakati za mchakato wa kisinodi wa Kanisa na hata amchakato wao kuelekea daraja la ukuhani. Ni imani yake Papa kwamba wakati wanaendelea katika njia hiyo ya mafunzo na katika malezi ya seminari ya Mtakatifu Maria, inawaruhusu kukua katika upendo mwaminifu kwa Mungu na katika huduma ya kinyenyekevu kwa kaka na dada zao. Baba Mtakatifu amewakabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria Msimamizi wa Seminari yao; kwa moyo amewabariki kila mmoja wao, familia zao na Makanisa mahalia.Amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.