Papa:katika uso wa vita vya chuki na kulipiza kisasi,tuzidisha toba ya ndani!
Na Angella Rwezaula, - Vatican
Katika tukio la Kozi ya XXXIII kuhusu 'Foro Interno' yaani Toba ya kina ya Sakramenti ya upatanisho ambayo imehitimishwa Roma tarehe 24 Machi jijini Roma, washiriki wake Alhamisi tarehe 23 Machi 2023, wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko ambapo mara baada ya hotuba ya Mkuu wa Idara ya Toba ya Kitume, Kadinali Mauro Piacenza, na yale ya Monsinyo Nykiel Baba Mtakatifu Francisko aliwachekesha kidogo katika salamu zake mwanzoni kwa kuwa hapakuwapo na wanawake na kwa sababu hawaungamishi. Kwa hiyo alisema kwamba ni zaidi ya miongo mitatu sasa, Idara ya Toba ya Kitume inaandaa wakati huu muhimu na wa thamani wa malezi, ili kuchangia katika maandalizi ya waungamashaji wema, wakifahamu kikamilifu umuhimu wa huduma katika huduma ya waungamaji. Papa amepyaisha shukrani yake kwa Idara hiyo na kutia moyo kuendelea katika ahadi hiyo ya malezi, ambayo ina manufaa mengi kwa Kanisa kwa sababu inasaidia kusambaza kiini cha rehema kamili ya huruma.
Papa Francisko kwa kusisitiza zaidi alisema: “Ikiwa mtu hajisikii kuwa mtoaji wa huruma anayempokea Yesu, hasiende kwa mtu kuja kuungama. Katika moja ya Makanisa Makuu ya Kipapa, kwa mfano, alimwambia Kadinali kwamba “Kama kuna mtu anayesikia na kukemea, kushutumu na kisha kutoa toba ambayo haiwezi kufanyika, ni bora hasifanye kazi, kwa sababu huruma inasimama pale ili kusamehe na kutoa neno kusudi mtu aondoke akiwa na msamaha mpya. Kwa hiyo kuhani yuko pale kwa ajili ya kusamehe na wanapaswa kuweka hayo moyoni mwako. Waraka wa Kitume Evangelii gaudium unasema kwamba Kanisa linaloondoka na linaishi shauku isiyokwisha ya kutoa huruma, matunda ya kuwa na uzoefu wa huruma ya Baba isiyo na kikomo na nguvu zake za kuenea (Eg. 24). Kwa hiyo kuna kifungo kisichoweza kutenganishwa kati ya wito wa kimisionari wa Kanisa na sadaka ya rehema kwa watu wote. Kwa kuishi kwa huruma na kuitoa kwa wote, Kanisa linajitambua na kutekeleza matendo yake ya kitume na kimisionari. Tunaweza karibu kusema kwamba rehema imejumuishwa katika tabia za Kanisa, hasa hufanya utakatifu na utume wa kung'aa.
Kanisa daima limeonesha utambulisho huu wa huruma kwa mitindo tofauti katika enzi mbalimbali, iliyoelekezwa kwa mwili na roho, ikitamani, pamoja na Bwana wake, wokovu kamili wa mtu. Na kazi ya huruma ya Mungu kwa hiyo inaendana na tendo la kimisionari la Kanisa lenyewe, na uinjilishaji, kwa sababu uso wa Mungu unang'aa ndani yake kama vile Yesu alivyotuonesha. Kwa sababu hiyo haiwezekani, hasa katika kipindi hiki cha Kwaresima, kuachilia uangalifu usitishwe kutolewa kwa zoezi la mapendo ya kichungaji, ambayo yanadhihirishwa kwa njia madhubuti na ya hali ya juu kwa usahihi kabisa katika upatikanaji kamili wa mapadre bila kusitasita, zoezi la huduma ya upatanisho. Baba Mtakatifu alisema “Upatikanaji wa muungamishi unadhihirika katika baadhi ya mitazamo ya kiinjili. Zaidi ya yote katika kukaribisha kila mtu bila upendeleo, kwa sababu Mungu pekee ndiye anayejua ni neema gani inaweza kufanya kazi katika mioyo, wakati wowote; kisha katika kuwasikiliza ndugu kwa sikio la moyo, lililojeruhiwa kama moyo wa Kristo; katika kuwasamehe waliotubu, kwa kutoa kwa ukarimu msamaha wa Mungu; katika kuisindikiza safari ya toba, bila kulazimisha, kwenda sambamba na waamini, kwa subira na sala daima.”
Baba Mtakatifu Francisko kwa hiyo ametoa mfano wa kumfikiria Yesu, ambaye alichagua kunyamaza mbele ya mwanamke mzinzi, ili kumwokoa asihukumiwe kifo (taz. Yn 8:6); vivyo hivyo kuhani katika maungamo anapaswa kupenda ukimya, kuwa na moyo mkuu, akijua ya kuwa kila mwenye kutubu humkumbusha hali yake binafsi ya kuwa mdhambi na mhudumu wa rehema. “Huu ndio ukweli wao. Ikiwa mtu hajisikii kama mwenye dhambi, tafadhali hasiende kwenye kuungamisha. Mwenye dhambi na mhudumu wa huruma, pamoja”. Ufahamu huu utahakikisha kwamba waungamaji hawakuachwa na kwamba mapadre hawakosi kupatikana. Utume wa uinjilishaji wa Kanisa unapita katika sehemu kubwa kutoka kwa ugunduzi upya wa zawadi ya Kuungama, pia kwa mtazamo wa Yubile inayokaribia ya 2025.
Papa amefikiri juu ya mipango ya kichungaji ya Makanisa fulani, ambayo kamwe ameomba kusiwe na ukosefu wa nafasi kwa ajili ya huduma ya Sakramenti ya Upatanisho. Hasa, amefikiria toba hiyo kwa kila kanisa kuu, toba katika mahali patakatifu pa Mungu; Kwa hiyo juu ya uwepo wa kawaida wa muungamishi, mwenye masaa ya kutosha, katika kila eneo la kichungaji, na pia katika makanisa yanayohudumiwa na jumuiya za kitawa, kwamba daima kuna huduma ya maungamo kwa zamu. Ametoa mfano kuwa kuna wengine wanasema kwamba “Siku zote, kamwe katika maungamo ni kutupu! Kwa sababu watu hawaji…” lakini ushauri Papa akasema basi wasome jambo fulani, wasubiri tu, watakuja. Iwapo huruma ni utume wa Kanisa, hatuna budi kuwezesha kwa kadiri iwezekanavyo waamini kupata “mkutano huu wa upendo”, kuutunza tangu kuungama kwa watoto kwa mara ya kwanza na kupeleka mazingatio hayo katika maeneo ya matunzo na mateso. Wakati mengi hayawezi kufanywa tena kuponya mwili, mengi yanaweza na lazima yafanyike kila wakati kwa afya ya roho! Kwa maana hiyo, Kuungama kwa mtu binafsi huwakilisha njia ya upendeleo ya kuchukua, kwa sababu inapendelea kukutana kibinafsi na Rehema ya Mungu, ambayo kila moyo wa toba unangojea.
Kila moyo uliotubu unangoja rehema kamili hiyo. Katika Kuungama kwa mtu binafsi, Mungu anataka kibinafsi, kwa huruma yake, kila mwenye dhambi: Mchungaji, ni yeye tu, anayejua na kuwapenda kondoo mmoja baada ya mwingine, hasa wale walio dhaifu na waliojeruhiwa zaidi. Na sherehe za jumuiya zinapaswa kuthaminiwa katika baadhi ya matukio, bila kukataa Kuungama kwa mtu binafsi kama njia ya kawaida ya kuadhimisha sakramenti. “Duniani, kwa bahati mbaya tunaiona kila siku, haikosi milipuko ya chuki na kulipiza kisasi. Sisi tunaokiri lazima basi kuzidisha kitoweo cha huruma. Tusisahau kwamba tuko katika pambano lisilo la kawaida, pambano ambalo linaonekana kuwa kali sana katika wakati wetu, hata ikiwa tayari tunajua matokeo ya mwisho ya ushindi wa Kristo juu ya nguvu za uovu, lakini pambano hilo bado lipo. Ushindi huu kweli hufanyika kila wakati kwa mtubu anaposamehewa. Hakuna kinachofukuza na kushinda uovu zaidi ya rehema ya kimungu”.
“Na juu ya hili, ningependa kuwaambia jambo moja: Yesu alitufundisha kwamba tusizungumze kamwe na shetani! Katika majaribu jangwani alijibu kwa Neno la Mungu, lakini hakuingia katika mazungumzo. Kwa hiyo kuweni waangalifu katika kukiri na msiwe na mazungumzo na uovu, kamwe!” Papa aliongeza kusema “Ni kutoa haki ya msamaha na kufungua baadhi ya milango kwa ajili yake na kusonga mbele; lakini msiingie kamwe kuwa daktari wa magonjwa ya akili, tafadhali, msiwe wataalamu wa magonjwa ya akili na msiingie kamwe katika mambo haya. Ikiwa yeyote kati yenu ana wito huo, afanye mahali pengine, lakini si katika huduma ya ndani ya sakramento ya kitubio. Na haya ni mazungumzo ambayo hayana uwezo wa kufanya na wakati wa huruma. Ni ninyi tu mnapaswa kufikiria juu ya kusamehe na jinsi gani mnavyoweza kuingia ...” Papa amewashauri na kuwapa Onyo kali la kutochimba chimba mioyo ya watu,bali kuhurumia, kuwa na huruma tu mtu anapokuja kuungama.
Papa kwa kutambua kuwa tarehe 24 Machi wanahitisha kozi na kuwa na maadhimisho ya toba alisema hiyo ni jambo zuri na la maana katika kukaribisha na kusherehekea kibinafsi zawadi ambayo tumeitwa kuwaletea kaka na dada zetu; kuonja wema wa upendo wa Mungu wenye rehema. Yeye Hachoki kutuonesha moyo wake wenye huruma. “Hachoki kusamehe. Sisi ndio tunachoka kuomba msamaha, lakini hachoki kamwe". Papa anawasindikiza katika sala na anawashukuru kwa shughuli hiyo ya toba wanaayoifanya bila kuchoka kwa ajili ya Sakramenti ya kitubio na msamaha. Amewaalika wagundue tena, uenezaji kwa kina kitaalimungu na kichungaji pia kwa mtazamo wa Jubilei 2025, ile ya upanuzi wa asili wa huruma ambao ni msamaha, kulingana na mapenzi ya Baba wa mbinguni kuwa nasi daima na tu pamoja naye, katika maisha haya na katika uzima wa milele. Asante kwa kujitolea kwako kila siku na kwa mito ya rehema ambayo, kama mifereji ya unyenyekevu, unamimina na kuimwaga ulimwenguni, kuzima moto wa uovu na kuwasha moto wa Roho Mtakatifu. Ninawabariki nyote kutoka moyoni mwangu, ninyi nyote. Na ninawaomba tafadhali mniombee.