Tafuta

Papa:Kila mbatizwa anaitwa kuwa mtume wa Kanisa Katoliki Takatifu la mitume

Katika katekesi yake Jumatano 15 Machi,Papa ameendelea tafakari juu ya ‘ari ya kuinjilisha’:Mapadre,watu waliowekwa wakfu na walei wana kazi tofauti lakini wito wao ni sawa na utume hata wale wanaoshika nyadhifa za juu zaidi katika Kanisa.Kanisa limeitwa kutumikia kama ilivyo kwa Mkristo kuwa mtume mnyenyekevu na sio mpandaji na ubatili.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu  Francisko ameanza tafakari yake, Jumatano tarehe 15 Machi 2023 kwa waamini na mahujaji waliofika katika katrkesi hiyo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican katika mwendelezo wa tafakari juu ya ‘ari ya kuinjilisha’ na kufafanua maana ya kuwa wanafunzileo hii hasa kwa kuongozwa na katiba ya Kitume ya Mtaguso wa Pili wa Vatican. Papa akinza amesema: “Tuendelee na katekesi kuhusu ari ya uinjilishaji: si tu juu ya uinjilishaji, ari ya uinjilishaji  na katika shule ya Mtaguso wa II wa Vatican, tukitafuta kujua vema, nini maana ya kuwa mitume leo hii!

Papa akisalimia waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa akisalimia waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Baba Mtakatifu amesema Neno mtume linatupeleka akilini mwetu katika kile kikundi cha Mitume kumi na wawili waliochaguliwa na Yesu. Wakati mwingine tunaita mtume, kwa mtakatifu mmoja au zaidi kwa ujumla wa Maaskofu. Ni mitume kwa sababu wanakwenda kwa jina la Yesu. Lakini je tunatambua ya kuwa,  kuwa mtume unatazama kila mkristo? Yaani kila mmoja wetu? Kiukweli tunaitwa kuwa mitume wa Kanisa ambalo katika sala ya Nasadiki tunakiri jinsi tulivyo mitume. Kwa hiyo basi ni ni maana ya kuwa mtume? Maana ya kutumwa kwa ajili ya utume.

Katekesi ya Papa Francisko
Katekesi ya Papa Francisko

Mfano mzuri na msingi wake ni tukio ambalo Yesu Mfufuka aliwatuma mitume wake ulimwenguni, ili kueneza uwezo ambao Yeye mwenyewe aliupokea kutoka kwa Baba na kuwazawadia wao Roho yake. Tunasoma katika Injili ya Yohane: “Yesu aliwambia tena: “Amani iwe nanyi! Kama Baba alivyonituma mimi, nami ninawatuma ninyi. Baada ya kusema hayo aliwavuvia na kuwambia: “Pokeeni Roho Mtakatifu” (Yh 20,21-22). Mantiki nyingine msingi ya kuwa mtume ni wito, yaani kuitwa. Ilikuwa hivyo tangu mwanzo wakati Bwana Yesu alipowaita kwake wale ambao walikuwa wanakwenda na yeye (Mk 3,23). Aliunda kama kikundi, na kuwapatia wao jina la Mitume, ili waweze kukaa na Yeye na kuwatuma katika utume(Mk 3,14; Mt 10,1-42).

Mtakatifu Paulo katika barua zake anajiwakilisha kama: “Paulo aliyeitwa kuwa mtume (1Kor1,1) na bado: “ Paulo mtumishi wa Yesu Kristo, mtume kwa wito, aliyechaguliwa kwa ajili ya kutangaza Injili ya Mungu (Rm1,1)”. “Na anasisitiza juu ya kuwa mtume kwamba sio kwa upande wa watu na wala si kwa njia ya binadamu, lakini ni kwa njia ya Yesu Kristo na Mungu Baba ambaye alimfufua katika wafu(Gal 1,1); Mungu alimwita tangu tumboni mwa mama yake ili kutangaza Injili katikati ya watu (Gal 1,15-16). Uzoefu wa Mitume kumi na wawili na ushuhuda wa Paulo unaomba hata sisi. Unatualika kutathimini tabia zetu, shughuli zetu, maamuzi yetu, juu ya misingi ya mambo yenye msimamo, ammbayo yote hayo yanategemea na mwito wa bure wa Mungu; Mungu anatuchagua hata katika huduma ambayo wakati mwingine zinaweza kuonekana kuwa juu ya uwezo wetu au kuzidi matarajio yetu; Wito uliopokelewa kama zawadi ya bure unahitaji kujibiwa bure”, Papa amesisitiza.

Makundi mbali mbali katika Katekesi ya Papa
Makundi mbali mbali katika Katekesi ya Papa

Mguso ulisema kuwa: “Wito wa Kikristo (...) kwa asili yake pia ni wito wa utume” (rej. Apostolicam actuositatem, 2). Papa ameongeza kusema “ Ni suala la wito ambalo ni la kawaida, “kama vile hadhi ya washiriki kwa kuzaliwa upya katika Kristo ilivyo kawaida, na neema ya kufanywa wana ni ya kawaida; wito wa ukamilifu ni wa kawaida;  na kuna wokovu mmoja tu, tumaini moja na upendo mmoja bila migawanyiko” (LG, 32). Ni wito unaowahusu wale wote waliopokea sakramenti ya Daraja Takatifu na watu waliowekwa wakfu na kila mwamini mlei, mwanamume au mwanamke, kwa maana hiyo ni wito kwa wote. “Wewe,  na hazina uliyopokea kwa wito wako wa Kikristo, unalazimishwa kuutoa: ni nguvu ya wito, na  ni nguvu ya maisha”, Papa Francisko ameongeza.

Baba Mtakatifu akifafanua amebainisha kwamba “Ni wito unaomwezesha mtu kutekeleza kazi yake ya kitume kwa njia iliyo hai na yenye ubunifu ndani ya Kanisa ambamo “kuna huduma mbalimbali lakini kwa umoja wa utume. Mitume na wafuasi wao walipokea kutoka kwa Kristo shughuli ya kufundisha, kutawala na kutakasa katika jina lake na kwa mamlaka yake. Lakini pia waamini: yaani watu wote (ninyi nyote; wengi wenu ni watu wa kawaida), akigeukia umati wote katika uwanja. Kwa hiyo hata walei, wanaoshiriki katika huduma ya  Kristo ya ukuhani, ya kinabii na ya kifalme, ndani ya utume wa watu wote wa Mungu wana shughuli yao wenyewe katika Kanisa na katika ulimwengu” (AA, 2).

Ndani ya mfumo wa umoja wa utume, utofauti wa karama na huduma haupaswi kusababisha, ndani ya kiungo cha kikanisa, makundi ya upendeleo kwa sababu ndani yake  hakuna hupandishwaji cheo na unapofikiria maisha ya Kikristo kama kupandishwa cheo, kwa yule aliye juu anayewaamuru wengine maana amepandishwa cheo, huu sio ukristo. Huu ni upagani mtupu. Wito wa Kikristo si kupandishwa cheo cha kwenda juu, la! Ni jambo jingine. Na kuna jambo kubwa kwa sababu, ingawa wengine kwa mapenzi ya Kristo mwenyewe wamewekwa mahali pa maana zaidi, labda, madaktari, wasambazaji wa mafumbo na wachungaji kwa ajili ya wengine, hata hivyo kuna usawa wa kweli kati ya wote kuhusu hadhi na  ambalo ni tendo la kawaida kwa waamini wote katika kuujenga mwili wa Kristo” (LG, 32).

Kila mara katika katekesi ya Papa waamini wanapenda kumletea zawadi Papa
Kila mara katika katekesi ya Papa waamini wanapenda kumletea zawadi Papa

Kwa hiyo basi ni nani aliye na heshima zaidi katika Kanisa, Papa ameuliza swali je: ni Askofu, Padre? Hapana … kwa kijibu amesema “sisi sote ni Wakristo katika huduma ya wengine. Aidha amerudia tena je ni nani aliye muhimu zaidi katika Kanisa: mtawa au mtu wa kawaida, aliyebatizwa, asiyebatizwa, mtoto, askofu…?  Kwa kujibu tena amesema “Kila mtu ni sawa, sisi sote ni sawa na wakati sehemu mmoja inajiamini kuwa muhimu zaidi kuliko wengine na kuinua pua yake kidogo, kwa namna hiyo anakosea. Huo sio wito wa Yesu”. Baba Mtakatifu amesema “ Wito Yesu  ambao anautoa, kwa kila mtu, lakini pia kwa wale wanaoonekana kuwa katika nafasi za juu, ni huduma, kuwatumikia wengine na kujinyenyekeza”. Papa Francisko kwa hili ameongezea: “Ikiwa utamwona mtu ambaye ana wito wa juu zaidi Kanisani na ukamwona ni batili, utasema: “Maskini mwenzetu”;  kwa hiyo mwombeeni maana hajaelewa nini  maana ya  wito wa Mungu. Wito wa Mungu ni kumwabudu Baba, kuwa na upendo kwa jumuiya na kutoa huduma. Hilo ndilo la kuwa mitume,  huo ndio ushuhuda wa mitume”! Papa amesisitiza.

Papa akisalimiwa mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa akisalimiwa mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro

Suala la  ukosefu wa usawa katika hadhi yam tu  linatutaka tufikirie kwa upya vipengele vingi vya mahusiano yetu ambavyo ni muhimu kwa ajili ya uinjilishaji, Baba Mtakatifu amesema. Kwa mfano, je, tunafahamu  ya kwamba kwa maneno yetu tunaweza kudhuru hadhi ya wa wat una  hivyo kuharibu mahusiano ndani ya Kanisa? Tunapojaribu kufanya mazungumzo na ulimwengu, je, tunajua jinsi gani ya kujadiliana sisi kwa sisi kama waamini? Au parokiani mmoja anakwenda kinyume na mwingine, je, mmoja anamsengenya mwenzake ili apande zaidi? Aidha Je! tunajua jinsi ya kusikiliza ili kuelewa sababu za mwingine, au tunajilazimisha, labda hata kwa maneno laini? Kwa hiyo kusikiliza, kujinyenyekeza, kuwahudumia wengine hiyo ndiyo maana ya kutumikia, hiyo ndiyo maana ya kuwa Mkristo, hidi ndiyo maana ya  kuwa mtume. Kwa kuhitimisha, Papa Francisko amebainisha kwamba: “Tusiogope kujiuliza maswali haya. Tuukimbia ubatili, na ubatili wa nafasi. Maneno haya yanaweza kutusaidia kuthibitisha jinsi tunavyoishi wito wetu wa ubatizo, jinsi tunavyoishi njia yetu ya kuwa mitume katika Kanisa la kitume ambalo liko katika huduma ya wengine”.

Katekesi ya Papa na wito baada ya katekesi
15 March 2023, 11:18