Papa:Kuombea tena Ukraine na wahanga wa kimbunga huko Mississippi
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Dominika tarehe 26 Machi 2023, mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena amegeuza mawazo yake kwa ajili ya ardhi inayoteswa ambayo imekuwa na migogoro kwa zaidi ya mwaka mmoja. Aidha kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Vatican amekumbusha ambao wamefanya makusanyo ya matoleo ya sadaka katika makanisa yote ya Italia kwa ajili ya wakazi wa Siria na Uturuki walioathirika na tetemeko la ardhi tangu tarehe 6 Februari iliyopita na wakati huo huo anaonesha mshikamano na Mississippi inchini Marekani liyoharibiwa na mafuriko na kimbunga.
Baba Mtakatifu akianza kumbukizai maneno yake yamerudisha katika siku kuu ya tarehe 25 Machi kwamba: “Jana, ilikuwa siku kuu ya hupashanaji wa habari ambapo tulifanya kwa upya wakfu wetu kwa Moyo Safi wa Maria, kwa uhakika kwamba ni uongofu wa mioyo pekee yake ambao unaweza kufungua njia iendayo kwenye amani. Tunaendelea kuwaombea watu wa Ukraine waliouawa.”
Papa Francisko aidha ametoa mwaliko wa kuunga mkono makusanyiko kwa ajili ya Siria na Uturuki. Kwa hiyo ni idadi ya watu wa Uturuki na Siria walioathiriwa na tetemeko la ardhi la tarehe 6 Februari iliyopita kuwa: “Na pia tunasalia karibu na wahanga wa tetemeko la ardhi la Uturuki na Siria. Mkusanyiko maalum wa matoleo ambayo hufanyika leo katika parokia zote za Italia imekusudiwa kwao”. Kabla ya kuwasalimia waamini waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Papa alihimiza maombi pia kwa ajili ya watu wa jimbo la Mississippi, nchini Marekani waliokumbwa na kimbunga kikali.
Katika salamu zake pia Papa hakusahau kutaja hali ya wasiwasi nchini Peru kwamba “Ninawasalimu mahujaji wa Peru, nikifanya kwa upya sala zangu za amani na upatanisho nchini Peru. Ni lazima tuombee Peru, ambayo inateseka sana”. Na, zaidi ya hayo, kwa namna maalum amewageukia ujumbe wa Jeshi la Anga la Italia, ambalo linaadhimisha miaka mia moja tangu kuundwa kwake: “Ninawatakia heri ya maadhimisho haya na ninawahimiza kila wakati kufanya kazi kwa ajili ya ujenzi wa haki na amani”.
Habari za hivi karibuni kutoka nchi iliyovamiwa na Urussi, zinaona tangazo la Rais wa Urussi Putin kuhusu kutumwa kwa silaha za kimkakati za nyuklia huko Belarus linazidisha mvutano wa kimataifa juu ya mzozo wa Ukraine. Mkuu wa Ikulu ya Kremlin alieleza kuwa si suala la kuhamishwa kwa silaha za nyuklia kwa serikali ya Belarusi bali ni suala la kupelekwa kwenye ardhi ya Belarusi iliyokamilika na mafunzo ya kijeshi kama vile Marekani inavyofanya Ulaya. Baadaye Putin alitoa maoni yake kuhusu usafirishaji wa London wa risasi za uranium zilizopungua hadi Ukraine, akionya kwamba Urussi ina mamia ya maelfu ya aina hii ya silaha. Hatimaye, alonesha kwamba Urussi tayari imewasilisha mfumo wa makombora wa Iskander kwa Minsk na pia ilitangaza kwamba itazalisha zaidi ya mizinga 1,600 ndani ya mwaka mmoja.
Silaha ya atomiki ya Urussi, kubwa zaidi ulimwenguni
Urussi inashikilia Minsk kama mateka wa nyuklia: hii ni jibu linalotoka kwa serikali ya Kyiv, kulingana na ambayo uhamisho wa silaha za nyuklia za mbinu inawakilisha hatua kuelekea uharibifu wa ndani wa Belarus. Wakati huo huo, kutoka Pentagon, wanaripoti kuwa utawala wa Marekani hauna taarifa zozote za kijasusi zinazoonesha nia ya Urussi kutumia silaha za nyuklia na kwamba wataendelea kufuatilia hali hiyo. Ikumbukwe kwamba silaha za atomiki za Russia, zenye vichwa 6,000, ndizo kubwa zaidi duniani, zikifuatiwa na za Marekani yenye zaidi ya 5,400.