Tafuta

2023.03.09 Papa na washiriki wa Mkutano uliohamasishwa na watawa wa Fraterna Domus wa Sacrofano, Roma 2023.03.09 Papa na washiriki wa Mkutano uliohamasishwa na watawa wa Fraterna Domus wa Sacrofano, Roma  (Vatican Media)

Papa:mhamiaji akubaliwe kama mtu na sio mnyonyaji

Kwa washiriki wa kongamano la mafunzo kuhusu "Ukarimu" lililohamaishwa na watawa wa Fraterna Domus,linaloendelea hadi 10 Machi,Papa Francisko kwa mara nyingine amezungumza juu ya wale wanaoondoka katika nchi yao kutafuta maisha bora zaidi na kuhusu wale wanaosita kupokea kutokana na utaifa uliofungwa.Uhuru ni muhimu ili kuzalisha udugu na urafiki wa kijamii.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, alhamisi 9 Machi 2023 amekutana na washiriki wa semina kuhusu makaribisho iliyohamasishwa na Fraterna Domus, kwa kushukuru maneno ya Sr. Milena Pizzoli na washiriki wote, wa semina hiyo. Awali ya yote amawapongeza watawa hao kwa mpango ambao wao wameweka karama yao yao, uzoefu wao na hata muundo wa hudumia katika muktadha wa namna nyingi wanayojikita nayo katika nyanja ya makaribisho. Ni muktadha tajiri wa thamani na kiroho, lakini pia kwa njia ya janga la wakati wetu. Papa amewashukuru tena na juhudi zao, na hata vyama vingine, taasisi, mifuko ya usaidizi na jumuhia ambazo zinashirikiana na kozi hiyo kuhusu makaribisho.

Papa na washiriki wa semina kuhusu makaribisho
Papa na washiriki wa semina kuhusu makaribisho

Papa amependa kushirikishana na baadhi ya tafakari kuhusiana na Hati ya Fratelli tutti (Ft). Makaribisho ni moja ya sura ambayo inaelezea kile ambacho alikiitia “ulimwengu wazi (Ft, III). Waraka huo ni wito wa kufikia kutengeneza ulimwengu ulio wazi na ambao unaendana na wito huo, kwa hiyo wafanya kazi ili kupeleka mbele kila siku bila kelele, bila kuwasha taa na wafanye  hivyo hata kwa ajili ya mikutano ya mafunzo. Kiukweli ili kuweza kufanya kazi  kuwezesha makaribisho, inahitajika  hata kufikiria makaribisho.

Papa amekutana washiriki wa semina kuhusu makaribisho
Papa amekutana washiriki wa semina kuhusu makaribisho

Thamani muhimu za wakati kama huu ambapo kwa pamoja wanajikita kwa kina katika mantiki mbali mbali ya kiathlopolojia, kiadili, kidini, kihistoria na mengine. Lakini mafunzo yao sio katika mahabra ya mambo ya kudhaniwa kinyume chake ni wakati wa kutafakari bila kutengenua kazi juu ya kambi yenyewe. Ni wakati wa  kusali  na kujifunza, hivyo wazingatie wakati uliopo sura na  historia, matatizo ya dhati na kushirikishana na watoe  mada na makundi kukabiliana nayo.

Kwanza kabisa inaweza kupatikana katika sura ya tatu,  ya waraja wa Fratelli tutti chini ya kichwa cha "ufunguzi unaoendelea wa upendo”. “Upendo hutufanya tuelekee kwenye ushirika wa ulimwengu mzima. Hakuna anayekomaa au kufikia utimilifu wao kwa kujitenga. Kwa mienendo yake yenyewe, upendo unahitaji uwazi unaoendelea, uwezo mkubwa wa kuwakaribisha wengine, katika tukio lisiloisha ambalo huleta pamoja vitongoji vyote kuelekea hisia kamili ya kuheshimiana. Yesu alituambia: "Nyinyi nyote ni ndugu" (Mt 23,8),(FT, 95).

Hotuba ya Papa kuhusu makaribisho
09 March 2023, 18:05